Social Icons

Tuesday 31 December 2013

NI NDEFU LAKINI UTAJIFUNZA KITU....






Inawezekana umeshaiona mahali ujumbe huu, lakini leo ikiwa siku ya mwisho wa 2013 ningependa kushare na wewe hili.....
 
 
iStock 000005012679XSmall Is it irresponsible to trust God too much?
 
 
Katika kijiji cha Matare wilaya ya Mugumu Serengeti, Bwana Wambura alikamatwa kwa kesi ya kusingiziwa na kuhukumiwa kwenda jela miaka mitatu. Huku nyuma akiacha mke na watoto wanne waliokuwa wanasoma. Hukumu hiyo ilimtesa sana kichwa chake, alitamani kila mtu anayemhisikuwaana makosa aingie katika moyo wake na kuupata ukweli.
 
 Alilia na umaskini wake, labda angepata wakili mzuri angeweza kumtetea, kumkosa wakili kukahalalisha kifungo hicho!!Alikwenda gerezani huku akiumia
sana rohoni. Aliyaanza maisha mapya kwa shida sana, akawa mnyonge kila mara na mwili
ukapoteza afya kiujumla. Huko gerezani alifanikiwa kupata rafiki aliyekuwa na cheo ama
jukumu la uzikaji wa wafungwa hasa hasa ambao hawakuwa nandugu ama ambao ndugu zao huwa
hawajitokezi pale gerezani.

Mzikaji alijaribu sana kumtia nguvu Wambura na kumwaminisha kuwa hiyo ilikuwa hatua tu ya maisha anapaswa kuizoea na siku moja ukweli utajulikana tu! Bwana Wambura maneno ya mzikaji
hayakumuingia kabisa.. alizidi kunyong’onyea. “Siwezi kuvumilia kukaa gerezani miaka mitatu…..kama unajali kilio changu nisaidie nitoroke kwa namna yoyote ile ndugu yangu!!”Wambura alimsihi mzikaji.

SIKU MOJA mzikaji akamwambia Wambura kuwa msaada umepatikana. Lakini yataka moyo!!“Nipo tayari kwa lolote ilimradi tu nitoke humu!!” alijibu kwa msisitizo huku akimtegea sikio mzikaji. “Msaada pekee wa kukutorosha humu ndani ni kwa njia ya jeneza…yaani mfungwa akifa mimi nakuunganisha naye kwenye jeneza…..” akashusha pumzi kisha akaendelea “Wewe ukisikia kengele ya msiba, njoo mara moja kwenye chumba cha maiti, utakuta tayari sanduku liko katikati ya chumba linakuwa halijafungwa, funua kifunioko ingia ndani yake ulale pembeni ya maiti kwani sanduku huwa kubwa la kutosha kila aina ya maiti na hata miili miwili inaingia.

Kisha nitakuja na kulipigilia misumari. Baada ya muda tutalipakia kwenye gari na kutoka kwenda nje ya gereza makaburini nikiongozana na baadhi ya wafungwa na maaskari magereza. Tutakuzika huko lakini baada ya dakika 20 hadi 30 nitarudi kukufukua. Hautaweza kushindwa kupumua kwa dakika hizo, utatoka ukiwa huru.”
 
JAPOKUWA wazo lilikuwa zuri lakini lilimtisha sana Wambura. Hata hivyo akaona afadhali afanye hivyo kuliko kukaa gerezani miaka mitatu bila kosa. Siku moja akasikia kengere ya msiba. Akafanya kama alivyoelekezwa na mzikaji. Akaenda na kuingia chumba cha maiti. Kweli akalikuta sanduku, akiwa na hofu kuu akaingia na kulala pembeni ya maiti iliyokuwepo. Mara akasikia mtu ameingia na kulipigilia msumari sanduku. Muda mfupi baadaye sanduku likainuliwa na kuwekwa kwenye gari.
Gari ikatoka nje ya gereza hadi makaburini. Sanduku likashushwa na kuwekwa kaburini na kuanza
kufukiwa.Wambura alijitahidi sana kuvumilia japo hofu ilizidi kutanda. Alimtegemea sana mzikaji na
alianza kumuona mkombozi wa maisha yake. Kama alivyoambiwa, akasubiri dakika kumi, ishirini.. zikapita kimya!! Dakika thelathini kimya. Joto nalo likazidi kuongezeka. “Nitavumilia hadi afike…”
alijisemea kisha akajiongezea kauli ya ujasiri. “Kama nilitakiwa kuishi gerezani miaka mitatu kivipi dakika kadhaa za hapa kaburini”
 
KWA kuwa alishakaa gerezani kwa muda kiasi akatamani kujua aliyekufa ni nani… ni kweli aliogopa kuitazama maiti lakini aliona kama inatisha zaidi ikiwa imefunikwa vile kuliko ikiwa wazi.
Akaifunua upande wa usoni Kwa kuwa kulikuwa na giza nene alikodoa sana macho kuitazama.
LAHAULA!!! MACHO YAKAKUTANA NA SURA YA MZIKAJI!!!
MZIKAJI ALIKUWA AMEKUFA NA
AMEZIKWA NA AHADI ZAKE ZA UKOMBOZI!!
________________
FUNZO::
Usimtegemee sana mwanadamu katika maisha yako, kwanza ni dhambi!!
Pili mwanadamu anakumbana na vikwazo kama unavyokumbana navyo wewe hadi kumwendea yeye.
Hivyo kumpatia maisha yako ni kuzidi kuyaweka hatarini zaidi!!
Umeonewa umesingiziwa unanyanyaswa….. mwachie Mungu
afanye maamuzi…
_______________
Haya mzikaji aliyetegemea atamfukua naye ni maiti. Tazama mateso atakayoyapata hadi kufa
kwake…..
Bila shaka atatamani kurudi gerezani kwa miaka mingine kumi
lakini haitawezekana tena!!!



3 comments:

  1. Oh my what a shocking end but a truly important lesson. Oh my!!!

    ReplyDelete
  2. Dah! hyo ctory inacktsha.

    ReplyDelete
  3. Mydia umebadilisha maisha yangu.Be blessed.

    ReplyDelete