Social Icons

Friday 1 June 2012

How To Select Hair Styles according to face shape.....


Nimepata maombi ya kuandika article inayoongelea jinsi ya kuchagua aina ya nywele kulingana na uso wa mtu. Karibuni.......

Nywele ni moja ya mapambo ya muhimu sana kwa mwanamke na muonekano wake. Kila mwanamke anapenda kuwa na nywele zinazopendeza na kuvutia. Napenda kubadili style yangu ya nywele kadiri muda unavyoruhusu na nikiwa smart kichwani nakuwa ninajiamini zaidi.

Tunapoenda saloon au kwa wasusi huwa mara nyingi tunategemea ujuzi wao utupendezeshe sio wote tunaojua nini tunachokitaka na nini kinatupendeza. Jinsi ninavyopenda kubadili style zangu za nywele kila mara nimejifunza mengi kuhusu jinsi ya kuchagua hairstyle inayoendana na uso wako.



Hii picha inatupa idea ya aina ya sura zetu na muonekano wake.

  • Round face/Uso wa Duara:

Ukiwa na uso wa duara style ya nywele itakayokupendeza ni ile:

  • Isiyoleta nywele usoni kama kuweka fringe
  • Isiyoongeza ukubwa wa kichwa chako kwa kukusanya nywele katikati ya kichwa chako
  • Nywele ndefu zenye mawimbi/curls zitakupendeza
  • Kama unatumia weaving lisiwe refu zaidi ya kupita mabega

  How to Select Hairstyles According to Face Shape


  • Oval face:

Ukiwa na uso wa oval kila aina ya style itakupendeza hawana limitations ziwe fupi, ndefu, straight, curly, zimebanwa au zimeachiwa





  • Square face:
Ukiwa na square face unapendeza ukiacha nywele ndefu na zinazopepea zinaweza zikawa straight au zenye mawimbi/curly. Ukiwa na nywele fupi ziweke kwenye mawimbi/curly muonekano wako utapendeza zaidi.

  How to Select Hairstyles According to Face Shape





  • Heart Face:
Uso wa shape ya moyo ni mpana kwenye juu na mwembamba kuelekea kwenye mataya. Acha nywele zipepee mpaka karibu na taya hii inafanya paji la uso kuonekana jembamba kiasi na inabalance na kidevu. Style ya bob inapendeza sana wenye uso wa aina ya heart face.






  • Diamond face:
Uso wa shape ya diamond huwa na mifupa ya taya inayoonekana vizuri na kidevu chembamba inapendeza wakiweka style za nywele za kupepea ila hata style fupi wanapendeza mradi kuwe na balance ya taya na kidevu katika style hiyo.



  • Oblong face:
Uso wa shape ya Oblong ni mrefu wakiwa na paji la uso refu na kidevu kilichotokeza. Style ya nywele ni ile itakayoufanya uso uonekane una balance ya urefu na upana wake. Nywele straigtht na ndefu hazipendezi ila zenye mawimbi kiasi au hata kama straight ziwe na layers za kutosha. Ukiwa wa style fupi nywele ziwe na mawimbi zitapendeza zaidi.

  How to Select Hairstyles According to Face Shape


Natumai aliyeniuliza nimecover swali lake.....karibuni.......



0 comments:

Post a Comment