Social Icons

DR LOVE

DR LOVE ANAWALETEA.........


HOW TO LOVE A MAN/WOMAN....

 
 
HOW TO MAKE A MAN HAPPY

1. Feed him
2. Sleep with him
3. Leave him with peace
4. Don't check his phone (Msgs)
5. Don't bother him with his movements
So whats so hard about that?

HOW TO MAKE A WOMAN HAPPY

It's really not too difficult but.... To make a woman happy, a man only needs to be:

1. a friend
2. a companion
3. a lover
4. a brother
5. a father
6. a master
7. a chef
8. an electrician
9. a plumber
10. a mechanic
11. a carpenter
12. a decorator
13. a stylist
14. a sexologist
15. a gynecologist
16. a psychologist
17. a pest exterminator
18. a psychiatrist
19. a healer
20. a good listener
21. an organizer
22. a good father
23. very clean
24. sympathetic
25. athletic
26. warm
27. attentive
28. gallant
29. intelligent
30. funny
31. creative
32. tender
33. strong
34. understanding
35. tolerant
36. prudent
37. ambitious
38. capable
39. courageous
40. determined
41. true
42. dependable
43. passionate

WITHOUT FORGETTING TO:
44. give her compliments regularly
45. Go shopping with her
46. be honest
47. be very rich
48. not stress her out
49. not look at other girls
AND AT THE SAME TIME, YOU MUST ALSO:
50. give her lots of attention
51. give her lots of time, especially time for herself
52. give her lots of space, never worrying about where she goes.

BUT MOST OF ALL IT IS VERY IMPORTANT
53. never forget
*birthdays
*anniversaries
*valentine
*arrangements she makes.

What are your thoughts about this folks

 MBINU ZA KUIMARISHA MAHUSIANO...Watu Wengi Ambao Wako Kwenye Uhusiano Wanalalamika Kuwa Wenzi Wao Hawawaoneshi Upendo Kama Ilivyokuwa Siku Za Mwanzo Za Uhusiano Wao. Wanaeleza Kuwa Wanaona Uhusiano Wao Unalegalega Na Mapenzi Yanapungua Taratibu Kama Barafu Iyeyukavyo Juani.

Ili Kuepuka Yote Haya, Hauna Budi Kujifunza Njia Za Kuwasha Upya Moto Wa Upendo Kila Wakati Kwa Kuongeza Ukaribu (Intimacy) Kati Yako Na Mwenzako.

Zifuatazo Ni Mbinu Zitakazokusaidia:

1. Kucheka Pamoja

Kicheko Ni Mlango Wa Ukaribu, Kama Mwaweza Kucheka Pamoja Basi Mwaweza Kulia Pamoja, Na Hapa Mwaweza Kuaminiana Zaidi Katika Kuwasiliana Hisia Zenu, Kama Waweza Kuitofuta Furaha Katika Kila Kitu Basi Unaweza Kupenya Katika Vyote. Usiwe Mgumu Na Mwenye Msimamo Mkali Katika Kila Kitu. Jifunze Kujizuia Pale Unapoanza Kuelekea Kwenye Kukasirika Na Badala Yake Tumia Kucheka Kama Mlango Wa Kutokea. Kama Utaanza Kujizoeza Hivi Ukiwa Nyumbani, Taratibu Utaweza Ukiwa Ofisini Na Hata Kwingine Kokote.

 
2. Jifunzeni Kutiana Moyo

Kila Mmoja Awe Msaada Na Tegemeo Kwa Mwenzake. Jifunze Kumtia Moyo Na Kumwezesha Mwenzako. Sikiliza Na Kufuatilia Vile Mwenzako Afanyavyo Au Apendavyo.

Onyesha Heshima Katika Vitu Hivyo Pia. Kila Upatapo Nafasi Mpongeze Mbele Za Watu Au Hata Unapokua Nae Peke Yenu. Mjenge Mwenzako Mbele Ya  wengine Na Kubali Pongezi Zote Za Mafanikio Yenu Zimwendee Yeye. Mruhusu Mpenzi Wako Ajue Kuwa Una Mkubali Katika Kila Afanyalo. Zaidi Tunavyo Wainua Wapenzi Wetu Ndivyo Wanavyotuthamini Na Kutunyanyua Na Sisi Pia.

3. Jifunzeni Kupenda Kugusana

Nguvu Ya Mguso Wa Ukaribu Kamwe Haiwezi Kulinganishwa Na Chochote. Lazima Mjifunze Kujenga Tabia Ya Kugusana Mara Mpatapo Nafasi Sio Tu Mnapokuwa Mmelala. Kugusana Huku Ni Pamoja Na Kushikana Mkono Mkiongea Au Mkitembea, Kukumbatia Bega, Kugusa Au Kuchezea Nyewele Za Mwenzako Na Njia Nyingine Zozote Za Kuonyesha Ukaribu Kimwili. Wengi Wetu Huweza Kufanya Haya Kidogo Tunapokuwa Peke Yetu Na Kamwe Sio Mbele Ya Watu, Je, Ni Aibu, Nidhamu Mbaya? Dhambi?
Kugusana Ndiyo Mwanzo Wa Kuamsha Hisia Za Kuhitajiana, (Hebu Jiulize Kisirisiri, Lini Uligusana Na Mwenzako Nje Ya Chumba?). Kumgusa Umpendaye Hukuzuia Kutowaza Kumgusa Yeyote Katika Ulimwengu Uliojaa Wengi Walio Wapweke.

Mguso Huu Wa Upendo Haumaanishi Mguso Wa Tendo La Ndoa, Ingawa Pia Ni Vyema Kujifunza Kuijenga Lugha Ya Mguso Wa Tendo La Ndoa Katika Uhusiano Wenu.


 


 4. Zungumzeni Hisia Zenu

Kati Ya Vikwazo Vikubwa Katika Ustawi Wa Uhusiano Mengi Hususan Ya Wanandoa Ni Kutokuwepo Kwa Majadiliano. Lazima Wapenzi Wajifunze Kuzungumza Kuhusu Hisia Zao. Kama Vile Maisha Yasivyo Na Ukamilifu, Uhusiano Na Hata Ndoa Pia Hazina Ukamilifu. Mpenzi Wako Hayuko Kamili Na Wala Wewe Pia Siyo Mkamilifu. Jifunze Kuzungumza Na Umpendaye Jinsi Unavyojisikia Na Nini Kinachokusumbua. Kuendelea Na Migogoro Isiyosuluhishwa Husababisha Moyo Kuwa Baridi Juu Ya Mwenzako. Jiwekeeni Muda Kila Wiki Wa Kutoka Ili Kuzungumza Mambo Yenu. Mwambie Umpendaye Yapi Yanayojiri Kila Siku Na Zipi Ni Changamoto Zako Mkiweza Kujifunza Kuwekeza Katika Muda Wa Kuwa Pamoja Taratibu Hata Muda Wenu Wa Maongezi Ya Simu Utaongezeka.

5. Samehe Na Kubali Kusamehewa

Kamwe Tusiache Maumivu Na Machungu Yatawale Uhusiano Wetu. Lazima Tujifunze Kuwasamehe Tuwapendao Na Kujisamehe Sisi Pia. Kutofautiana Katika Uhusiano Kupo Sana, Na Lazima Tuwape Tuwapendao Nafasi Ya Kuelezea Vile Vinavyowaudhi Dhidi Yetu. Kila Hisia Za Mmoja Wetu Zina Umuhimu. Huwezi Kujiona Vile Ulivyo, Mruhusu Mwenzako Akwambie Yanayomuumiza Na Msameheane.

6. Linda Mwonekano Wa Mpenzi Wako

Mara Nyingi Hatari Hii Hutokea Tunapokuwa Katika Mizunguko Ya Huku Na Huko. Ukaribu Na Mpenzi Wako Hauendelezwi Tu Bali Unalindwa. Mwonekano Wetu Lazima Uwe Halisi Na Siyo Bandia . Vile Tunavyoviona Katika Tamthiliya Na Filamu Siyo Ukaribu Ulio Halisi. Kama Tunataka Tuonekane Sawa Na Vile Tunavyowaona Wengine Wanavyopendana Basi Tunakosea Na Kujizuia Kuwa Na Mtazamo Bora Katika Uhusiano Wetu. Ukianza Kupata Ukaribu Wa Kweli Baina Yako Na Mwenzako, Utapoteza Hisia Ya Kuhitaji Ukaribu Huo Na Mwingine Yeyote, Na Badala Yake Utaanza Kuulinda Ukaribu Mlionao.

Lengo Liwe Kuvitafuta Vile Vyote Mpenzi Wako Alivyonavyo Ambavyo Ni Kukuza Ukaribu Wenu. Mwenzako Awe Ndiyo Mtu Wa Muhimu Kuliko Wote Katika Maisha Yako.


MWANAMKE ANAHITAJI NINI........MWANAMKE ANAHITAJI MALEZI MAKUBWA SANA YA KUTHAMINIWA ZAIDI YA YAI… JITAHIDI KUMPENDA, KUMUHESHIMU, KUMBEMBELEZA, KUMJALI, KUMSIKILIZA, KUMUELEWA, KUMSAMEHE MAKOSA YAKE NA KUMFANYA AWE PEKEE DUNIA NZIMA, HII NDIO DAWA PEKEE YA KUISHI NAYE NA KUMFANYA AKUPENDE KILA WAKATI, LAKINI…

Mwanamke Ana Upendo 98.8999% Kwa Mwanaume…Mwanamke Mpaka Kufikia Hali Ya Kukubaliana Na Wewe Na Akakuheshimu Kwa Kukuvulia Kilakitu Alichonacho Yeye Kwa Kukupa Kile Wewe Unachohitaji Kutoka Kwake Na Amekupa Heshima Wewe Kama Mpenzi Wake Umtumie Unavyokata Na Kutokana Na Mapenzi Anayokupa Anaamua Kukuamini Na Kukupa Siri Zake Zote Wewe Kama Wake Mpenzi Na Mpaka Anawatambulisha Rafiki Zake Kuwa Wewe Ni Shemeji Yao Na Hawezi Ambiwa Chochote Juu Yako Kibaya Akaacha Kukwambia, Then Leo Hii Unamdharau “Aahgghr! Hana Lolote Huyo Kwanza Malaya Tu” …(Mbaya Sana Hii, Jifunze Kuishi Kiutu Uzima Hata Kama Ana tofauti Usiwe Na Hofu Kumweleza Na Ninaimani Atakuelewa)

Usimtese Kijinsia , Usije Thubutu Kumuacha Na Kasoro Zake , Ninamaanisha Kwamba Kama Anatatizo Au Wakati Wa Mambo Yetu Yale Kuna Kitu Unataka Ufanyiwe Na Yeye, Labda Yawezekana Hajui Au Anajua Lakini Ana Walakini Kukifanya, Basi Ni Lazima Umweleze, Muweke Wazi Kumbuka Huyo Ni Mpenzi Wako Ukiwa Kimya Ukasubiri Raha Ukapewe Na Kimada Wa Nje Basi Utajikuta Siku Ya Mwisho Unaleta Ugonjwa Ndani Au Wewe Kukusababishia Kukosa Nguvu Za Kiume Unapokutana Naye Mara Nyingi Kwa Sababu Ni Chanzo Kingine Cha Kusababisha Kukosa Nguvu Unapotembea Na Wanawake Wasiohesabika, Ukikutana Naye Mara Inalala Hii Ni Kutokana Na Uchapaji Wa Too Much Nje, Kwa Sababu Unapokuwa Naye Huwezi Ku Feel Kuwa Naye. Na Badala Yake Utaanza Kuwawaza Wengine Wa Nje Ambao Hawatakusaidia Katika Kujenga Uhusiano Mwema Na Mpenzi Wako. (Kumbuka: Hata Ukibadilisha Kuni, Moto Ni Ule Ule)
Mwanamke Akikupenda Usimdharau Kama Yeye Ni Malaya… Na Mwanamke Mpaka Ukiona Hajatulia Basi Jua Tatizo Lako Wewe, Fanya Juu Chini Ili Kuweza Kumbadilisha Kwa Sababu Kumbadilisha Mwanamke Ni Kitu Kidogo Sana Kwa Sababu Umekaa Naye Muda Mrefu Na Ni Lazima Utajua Tu Umguse Wapi Aweze Kuwa Kama Mwanzo, Kama Umeshanifuatilia Kwa Mada Zangu Ninazokupa Kupitia Hapa . Na Usijeomba Mwanamke Akulilie Machozi Mbele Zako, Ameshindwa Kumlilia Baba/Mama Yake Aliyemzaa Na Amekuja Kukulia Wewe… Wewe Una Nini? Epukana Na Hili Na Utunze Heshima Yake Na Umpe Penzi Lako, Hakuna Mwanamke Mbaya/Malaya/Kicheche Ila Wewe Ndio Utafanya Awe Hivyo… Wengi Wao Wameshawahi Kufanya Haya Na Sasa Wanalia Na Kusaga Meno Kwa Sababu Walijisahau Na Mwishowe Sasa Hawajielewi Kutokana Na Maisha Wayoishi Ya Kutokua Na Chaguzi Zilizo Za Halali…

Mwanamke Anapenda Kupendwa! Mara Nyingi Wanawake Ndiyo Hasa Huwa Na Mapenzi Ya Dhati Zaidi Kuliko Wanaume. Mwanamke Anapoamua Kuwa Na Mpenzi Wake, Humpenda Kwa Moyo Wake Wote, Hivyo Hupenda Kuwa Salama Katika Penzi La Dhati Kwako.

Anapenda Uhuru, Anapenda Kujisikia Wazi Kwako Mahali Popote. Mwanamke Anajisikia Vibaya Sana Anapokuwa Hana Uhuru Hata Wa Kukushika Mkono Mnakuwa Barabarani Pamoja. Anapenda Penzi La Uwazi!

Maana Mwingine Utakuta Akikutana Na Rafiki Yake, Badala Ya Kumtambulisha Vizuri Kama Mpenzi Wake, Anaanza Kupatwa Na Kigugumizi. Utamsikia Akisema: “Ah! Huyu Ni Rafiki Yangu Bwana, Anaitwa Latipha....”Hili Ni Kosa Kubwa Linalofanywa Na Wanaume Wengi Bila Kujua Ni Kosa.

Mwanamke Anakosa Amani Ya Moyo Kutokana Na Unavyomtafsirisha Mbele Ya Rafiki Zako. Anahisi Hayupo Salama. Lazima Atajiuliza Maswali, Kwanini Hataki Kunitambulisha? Kwanini Anashindwa Kusema Mimi Ni Mpenzi Wake? Sifananii? Sina Mvuto Au Nina Tatizo Gani?

Hayo Yanaweza Kuwa Maswali Yatakayomuumiza Sana Kichwa Mpenzi Wako, Ambaye Si Ajabu Akafanya Maamuzi Ambayo Hutayapenda. Kidonda Hiki Hubaki Moyoni Mwa Mwanamke, Huwa Vigumu Sana Kuonyesha Wazi Kwamba Amechukia Kutokana Na Uliyomfanyia, Lakini Atabaki Akiugulia Moyoni Mwake Kwa Uchungu.
Hata Hivyo, Kinachokuja Akilini Mwake Ni Kutafuta Mwanaume Mwingine Ambaye Atakuwa Wazi Kwake Ili Aweze Kufurahia Mapenzi Badala Ya Kuendelea Kuumia Moyoni Mwake. Ni Dhahiri Kwamba Uamuzi Huu Hautaufurahia Hakika.
1. UNAVYOJALI...
Mwanamke Anapenda Awe Wa Pekee Kwako, Umsikilize, Umjali Na Umpe Kipaumbele Katika Kila Unachokifanya . Wanawake Wengi Wanapenda Kudekezwa, Lakini Hawapendi Kuweka Hilo Wazi Kwa Mwanaume Wake. Kwa Kumtazama Tu Utagundua Mpenzi Wako Anahitaji Nini Zaidi Kwako!

Wakati Mwingine Anaweza Kukupa Mitihani Ili Kupima Kiwango Cha Penzi Lako. Anaweza Kukuambia Anaumwa Au Anauguliwa Na Mtu Wake Wa Karibu, Lengo Ni Kuangalia Ni Jinsi Gani Unakuwa Makini Anapokuwa Na Matatizo.

Vile Utakavyochukulia Tatizo Lake Kwa Ukaribu, Uchungu Na Kuona Kama Lako, Ndivyo Utakavyomfanya Aone Thamani La Penzi Lako Kwake, Ikiwa Vinginevyo Basi Humuacha Na Machungu Moyoni, Huku Akijutia Kuwa Na Mpenzi Wa Aina Yako.

Hii Ni Siri Ambayo Si Rahisi Mwanamke Wako Akueleze Moja Kwa Moja. Atatumia Lugha Ya Ishara Kuonesha Jinsi Ambavyo Anahitaji Kuwa Wa Pekee Kwako.

2. JIFUNZE SIRI HIZO.....

Hapa Ndipo Mwanaume Mwerevu Anatakiwa Kuwa Makini, Ni Lazima Ufahamu Siri Zilizopo Moyoni Mwa Mpenzi Wako. Jifunze Kusoma Hisia Za Mpenzi Wako Kwa Nje, Kabla Ya Kufanya Kitu, Fikiria Mara Mbili, Lakini Baada Ya Kufanya, Msome Kupitia Uso Wake.

Analifurahia Au Umemchukiza? Ni Vizuri Kugundua Hilo Ili Uweze Kufunga Hisia Za Kumfanya Aanze Kufikiria Kukusaliti. Hata Mnapokuwa Faragha Ni Vizuri Kuwa Makini Na Kila Unachokifanya! Chunguza Kama Anafurahia Penzi Lako Na Manjonjo Yote Unayomfanyia.

Kumbuka Kwamba Ni Vigumu Sana Mwanamke Kukueleza Moja Kwa Moja Kwamba Hujamfurahisha Au Kuna Kitu Umekikosea, Hii Husababishwa Na Hofu Ya Kuogopa Kukufanya Ujisikie Vibaya.

Kwa Maneno Mengi WEWE Mwanaume Ndiye Mwenye Kazi Ya Kuangalia Mwanamke Wako Anapenda Nini Na Nini Hapendi Ili Uweze Kuwa MWANAUME Wake Bora, Maana Hata Hisia Zake Za Ndani Utakuwa Unazifahamu. Ni Rahisi Sana, Soma Kupitia Macho Yake Kila Unachomfanyia, Utaujua Ukweli. Unajua Hata Ukimwita Kwa Jina Ambalo Hana Msisimko Nalo Lakini Ukiwa Unamtazama Usoni Ni Rahisi Sana Kugundua Kitu Fulani, Kama Hajakipenda Utaona Kwenye Macho Na Akikipenda Pia Utaona.

Unapokuwa Naye Faragha, Tumia Uwezo Wako Wote, Lakini Kumbuka Kwamba Si Kila Utakachokifanya Utamfurahisha. Hii Inamaanisha Kwamba, Baada Ya Kumchunguza Jinsi Anavyosisimka, Utaweza Kugundua Wapi Kuna Msisimko Zaidi Kuliko Sehemu Nyingine.

Hapo Sasa Unaweza Kuibuka MSHINDI Maana Utakuwa Umeziweka Siri Zake Hadharani, Kwa Maneno Mengine Kama Yeye Aliona Siri, Basi Umeweza Kuzigundua Na Angalau Umeanza Kuzifanyia Kazi. Nawapenda Sana Rafiki Zangu, Ndio Maana Nawapeni Mambo Mazuri Na Yenye Sifa Ili Msiweze Kusababisha Kitu Kinaitwa..."UMENITENDA/AMENITENDA" (KUTENDANA NI DHAMBI KUBWA SANA) NIWATAKIE SIKU NJEMA..

WAZO LA LANGU LEO:

WANAWAKE: Napenda Kuwashauri Wanawake Wote Ambao Wapo Katika Mahusiano Ya Kimapenzi Wajaribu Kuwa Wabunifu Katika Mapenzi, Mpe Mpenzi Wako Mapenzi Yote Toka Moyoni Mwako. Usidanganywe Kuwa Mapenzi Ni Mitishamba Hakuna Dawa Ya Mapenzi Kwa Mganga Ila Dawa Unayo Wewe Mwenyewe Mridhishe Mpenzi Wako Kwa Kumpa Vitu Vipya Katika Mapenzi Halafu Uone Je, Penzi Lako Kwa Mwenza Wako Utachangia Na Wenzako?!

WANAUME: Siku Zote Uwapo Katika Mapenzi Fahamu Kuwa Unapaswa Kumridhisha Mpenzi Wako Katika Tendo Mfanye Ajisikie Raha Pindi Muwapo Chumbani Inakubidi Uwe Mwanamke Wa Kileo Ujitahidi Kuwa Mbunifu Katika Mapenzi Kwa Kujituma Pindi Mnapokuwa Chumbani Na Mpenzi Wako, Jaribu Kushughulika Tumia Viungo Vyako Vya Mwili Katika Kuamsha Hisia Za Mwandani Wako Kabla Ya Kuanza Nae Kufanya Mapenzi Ili Kuhakikisha Mpenzi Wako Anapata Raha Na Inakuwa Ni Njia Nzuri Ya Wewe Kumfanya Mpenzi Wako Ahisi Kuwa Wewe Ni Muhimu Kwake Kutokana Na Mahaba Unayompa... Ehh! Habari Ndio Hiyo...mpaka muda ujao ungana na mimi Dr. Love....


LEO NAPIGA 2 IN ONE 

 ZIJUE SIFA ZA "MWANAUME ANAYETAKA KUWA SERIOUS NA WEWE" NA "MWANAUME ANAYEKUCHEZEA''


ATAKAYEKUOA SIFA ZAKE NI KAMA IFUATAVYO...

1. ANABADILIKA

 Mwanaume Ambaye Ana Malengo Ya Kuoa Hubadilika Kitabia. Muda Mwingi Hutaka Kuonekana Mtu Mzima Mwenye Sifa Nzuri. Hatakuwa Mtu Wa Kulewa Kupita Kiasi Na Kutapanya Mali Na Wanawake Wengine. Tabia Zake Mbaya Za Zamani Ataziacha

Kisa Cha Mabadiliko Hayo Kinatajwa Na Wataalamu Wa Masuala Ya Ndoa Kuwa Ni Pamoja Na Kumshawishi Mwanamke Aliyemchagua Aitikie Mwito Wa Kuwa Pamoja Katika Maisha. Lakini Pia Ni Kuwapa Kielelezo Chema Ndungu Au Wazazi Wake Wamuunge Mkono Katika Harakati Zake Za Kuoa.

2. ATAONGEZA JITIHADA ZA KUJITEGEMEA

Mara Nyingi Wanaume Walio Makini Na Tayari Kufunga Ndoa, Wanahitaji Kuwa Na Kipato Cha Kutosha Kuweza Kuwahudumia Wake Zao Na Familia Ambazo Watakuwa Nazo Hapo Baadaye Hivyo Wanajitahidi Kutafuta Njia Za Kupandisha Hali Yao Kiuchumi.

Kama Ni Muajriwa Anaweza Akaanza Kutafuta Miradi Mingine Nje Ya Kazi Yake Ili Imsaidie Kuongeza Kipato Cha Kujikimu Na Hali Ya Maisha. Kama Alikuwa Anaishi Na Wazazi Atapanga Chumba Na Ataanza Kujitemea.

3. ANAGUNDUA KWAMBA ANAHITAJI KUITWA BABA
Njia Nyingine Ya Kugundua Mwanaume Aliye Tayari Kwa Ndoa Ni Pale Unapotembea Naye Barabarani, Anawafurahia Watoto Mnaokutana Nao Njiani Na Mara Kwa Mara Ataonekana Kukueleza Jinsi Atakavyowafanyia Watoto Wake Mara Baada Ya Kuwapata Hapo Baadaye.

Mwanaume Huyo Pia Huwa Na Tabia Ya Kufurahia Maisha Ya Ndoa Ya Watu Wengine Yaani Anapomuona Mke Na Mume Wakiwa Na Mtoto Wao Basi Hutamani Sana Mngekuwa Nyinyi. Mnapotoka Hukuita Mke Wake!

4. NI RAFIKI LAKINI NI MUME KAMILI

Mwanaume Anayetaka Kuoa Anakuwa Ni Rafiki Yako Tu Kwa Sababu Hamjafunga Ndoa, Lakini Matendo Anayokufanyia Hayana Tofauti Na Yale Ya Mtu Kwa Mkewe. Kwa Mfano Kupanga Mipango Ya Baadaye Ya Maisha Yenu, Kukutambulisha Kwa Ndugu Na Rafiki Zake. Huwa Na Hamu Ya Kutaka Kujua Matatizo Yako Na Kukusaidia Na Wakati Mwingine Kukushirikisha Katika Matatizo Yanayomkabili.

Mara Nyingi Huwa Makini Sana Kutambua Mabadiliko Ya Mapenzi Na Hutoa Uhuru Na Kukumilikisha Vitu Vyake Kwa Mfano Kukupa Funguo Za Chumba Au Nyumba Yake. Hupenda Kutoa Misaada Ya Kumwendeleza Mpenzi Wake Kimaisha, Kama Kumsomesha Au Kumtafutia Kazi.

5. HUFURAHIA UKARIBU

Mwanaume Aliyetayari Kuoa Hupenda Kuwa Karibu Na Mpenzi Wake Na Asilimia Kubwa Ya Mazungumzo Yake Atayaelekeza Katika Maisha Si Ngono. Atajitoa Kusaidia Ndugu Wa Mke Kila Linapokuja Tatizo. Na Atalalamika Anapotengwa Na Familia Ya Mchumba Wake.


SIFA ZA MWANAUME ANAYEKUCHEZEA
1. ANAKWEPA MAZUNGUMZO YA NDOA

Haonyeshi Kufurahi Unapoanzisha Mazungumzo Kuhusu Suala La Kufunga Ndoa Na Wala Hapendi Kuzungumzia Hilo. Wakati Mwingine Hata Kukutambulisha Kwa Ndugu Zake Au Rafiki Inakuwa Shida.

2. ANAGHARAMIA ANASA KULIKO MAMBO MUHIMU

Anakuwa Ni Mtu Wa Kukununulia Mapambo Ya Gharama Na Vitu Vyote Vya Anasa, Lakini Hana Mawazo Ya Kuzungumzia Maisha Yenu Ya Baadaye Wala Kukununulia Vitu Ambavyo Vitakuwa Na Manufaa Katika Maisha Ya Mbeleni. Haangalii Masuala Ya Elimu Wala Kukutafutia Mtaji Au Kazi.

3. HAJALI MACHOZI YAKO

Unaweza Kugundua Ni Jinsi Gani Hana Mpango Mzuri Na Maisha Yako, Kwani Hata Anapokuudhi Anakuwa Hajali Wala Haumizwi Na Machozi Yako, Ni Busara Kuwa Makini Kwa Sababu Huyo Atakuwa Ni Mtu Wa Kukupa Maumivu Wakati Wote.

4. HAJITOKEZI HADHARANI

Mwanaume Ambaye Malengo Yake Ni Kukuchezea Huwa Hataki Mapenzi Yenu Yajulikane Hadharani Atakuwa Mtu Wa Kutaka Mambo Yaende Kwa Siri. Hajitambulishi Kwa Rafiki Wala Kwa Ndugu Zako. Hatoi Nafasi Ya Wewe Kumtembelea Nyumbani Kwake Wala Kuwajua Wale Wa Karibu yake na familia yake.
 
Ukiona hivyo wanasema akili za kuambiwa, changanya na za kwako........
 


MAPENZI YANAPOENDA KOMBO......Willy Anampenda Sana Lilly Lakini Anajua Fika Kwamba Mwenzi Wake Hajatulia. Hata Hivyo Anashindwa Kujipanga Kuchukua Hatua Muafaka.

Willy Anakuwa Mtu Wa Kulipuka, Akiudhiwa Na Mwenzi Wake Anatangaza Kuachana Naye Bila Kutafakari Mara Mbili...
. Haishii Hapo, Anaamka Na Chuki Mtindo Mmoja, Hata Akimkuta Barabarani Hamsalimii.

Je, Hiyo Ni Dawa? La Hasha, Kwa Kawaida Chuki Yako Itakupeleka Katika Mawazo Mengi. Utamkumbuka Kwa Mabaya Yake Lakini Hutaishia Hapo, Utaanza Kuyaona Mazuri Aliyokufanyia.
Ni Kipindi Hicho Ambacho Utaanza Kuumia Zaidi. Utatamani Yale Mazuri Yake. Inawezekana Ukakosa Aibu Na Kujikuta Wewe Mwenyewe Ndiyo Unaomba Msamaha Mrudiane.

Ukiwa Na Chuki Na Mwenzi Wako, Maana Yake Hisia Zako Bado Zipo Kwake. Akija Kuzungumza Na Wewe Ni Rahisi Kumsamehe Bila Kuzingatia Uzito Wa Kitu Alichokufanyia.
Nakusisitiza Kujua Kwamba Kinyume Cha Mapenzi Siyo Chuki. Ni Kutojali (Kupotezea). Yaani Unapokosana Na Mwenzi Wako, Usianze Bifu, Badala Yake Anza Kumpotezea Na Usimjali Kwa Chochote.

Unahitaji Kuwa Huru Na Hisia Zako. Unapoamua Kuacha Basi Simamia Uamuzi Wako. Ukizingatia Mambo Yafuatayo, Yatakupa Msaada Mkubwa Wa Kuvuka Kipindi Kigumu Cha Kuachana Na Mwenzako.

1. Mara Unapoachana Na Mwenzi Wako, Jitahidi Kadiri Uwezavyo Kuhakikisha Unasitisha Mawasiliano Naye. Iwe Kwa Simu, Ana Kwa Ana Na Mengineyo.

2. Acha Kukaribisha Hisia Kwamba Ipo Siku Wewe Na Yeye Mtarudiana. Amini Kuwa Hiyo Imetoka Jumla, Kwa Hiyo Fanya Mambo Yako, Huku Ukiamini Kwamba Mwenzi Wa Maisha Yako Anakuja.

3. Fanya Mambo Chanya Kama Vile Kujifunza Vitu Vipya, Kuongeza Ujuzi, Kufanya Kazi Kwa Bidii, Kujitolea Kwa Ajili Ya Watu Wengine, Kutoa Misaada Na Kufanya Mazoezi Ya Viungo.

Ukiyafanya Haya Yatakuwezesha Kuondoa Mawazo Hasi Kwa Mwenzi Wako Mliyeachana Na Kuzingatia Vitu Vya Msingi Ambavyo Vinahusu Ujenzi Wa Maisha Yako Ya Sasa Na Ya Baadaye.

MUHIMU:
Achana Na Hulka Za Chuki Kwa Mwenzi Wako Wa Zamani. Tangu Ulipokuwa Mdogo Mpaka Sasa Umekutana Na Marafiki Wangapi Ambao Wengine Leo Hawamo Kwenye Kumbukumbu Zako?

Mtazamo By TheDon...


UTAJUAJE KWAMBA HANA NIA NA WEWE........

ISHARA ZA MWANAUME AMBAYE HANA NIA AU HATAKI KUWA NA WEWE KATIKA MAHUSIANO YA KUDUMU (NDOA) NA WAKATI KIPINDI HICHO HICHO ANAKUTAMKIA NENO “NAKUPENDA”... Follow Me... Dr. Love...


1.HAPIGI SIMU, BALI HUTUMIA SMS

Je, Kijana Huyu Aliyekwambia Anakupenda Huwa Anawasiliana Nawe Kwa Njia Ya Ujumbe Mfupi Kuliko Anavyokupigia? Kama Utaona Hivyo, Basi Una Kila Sababu Ya Kuanza Kuitilia Shaka Nia Ya Kijana Huyu Wa Kiume, Kwani Kwa Hakika Hana Nia Yoyote Ya Dhati Ya Kuendelea Kuwa Nawe.

Kijana Wa Kiume Anapompenda Msichana, Hutamani Muda Wote Kuisikia Sauti Yake. Anapokuwa Anasisitiza Kutumika Kwa Ujumbe Mfupi Maana Yake Hana Haja Sana Ya Kusikia Sauti Yako. Naam, Ujumbe Mfupi Wa Maneno Si Njia Rahisi Sana Ya Kuwasiliana, Lakini Zaidi Ni Njia Rahisi Zaidi Ya Kuepuka Mawasiliano Na Kutoa Majibu Mafupi Kwa Mtu Ambaye Usingependa Kuwasiliana Naye.

2.HANA SABABU ZA KUCHELEWA

Unaweza Kubaini Katika Mikutano Yako Miwili-Mitatu Na Kijana Aliyekwambia Anakupenda, Kwamba Si Mtu Wa Kujali Wala Kutunza Muda. Naam, Yawezekana Katika Mara Mnazokutana, Mara Nyingi Zaidi Anachelewa Kuliko Anavyowahi. Unaweza Kudhani Kuwa Kijana Huyu Ana Mambo Mengi, Au Si Mzuri Katika Upangiliaji Wake Wa Muda, Lakini Kwa Hakika Hupaswi Kumtafutia Visingizio Hata Kama Unampenda, Kwani Kuna Uwezekano Mkubwa Kuwa Kijana Huyu Hana Mpango Na Wewe.

Kijana Wa Kiume Akikupenda Na Kupenda Kuendelea Kuwa Nawe, Lazima Tu Atakuwa Na Msukumo Wa Kutaka Kukutana Na Wewe Na Hatapenda Kukuudhi Kwa Kuchelewa. Mtu Huyu Hata Kama Atakuwa Amebanwa Vipi Kazini Ni Rahisi Sana Kutafuta Muda Wa Kukutana Na Wewe. Kinyume Chake Atakuwa Ni Mtu Wa Visingizio Vya Kuchelewa Na Wakati Mwingine Kutofika Kabisa Katika Eneo La Miadi – Hususan Kama Ameshakupata.

3.ANAWASILIANA NA MPENZI WA ZAMANI

Mwanamume Asiye Na Mpango Wa Kuendelea Kuwa Nawe Anapokuwa Amekutongoza Na Pengine Mmekutana Mara Moja Au Mbili, Atakutaarifu Kwa Kuendelea Kuwasiliana Na Mpenzi Wake Wa Zamani.

Kwa Hakika, Hakuna Jambo Ambalo Humsahaulisha Mwanamume Mpenzi Wa Zamani Kama Kumpata Mpenzi Mpya Anayempenda Kwa Dhati. Iwapo Ataendelea Kuwasiliana Na Kuzungumza Na Mpenzi Wake Wa Zamani, Hiyo Ni Ishara Kuwa Hajamalizana Na Mpenzi Wake Huyo Wa Zamani Na Pengine Bado Anatarajia Kurudiana Naye. Lakini La Muhimu Zaidi Ni Kwamba, Mwanamuke Huyu Hakupendi Kama Unavyodhani Na Wala Hajawa Tayari Kuwa Nawe Kama Mpenzi Au Mchumba.

4.HAKUTAMBULISHI KWA MARAFIKI

Mwanamume Akikupenda, Hususan Vijana Katika Zama Hizi, Lazima Tu Atakutambulisha Kwa Marafiki Zake, Maana Atakuwa Anajisikia Fahari Kwa Kufanya Hivyo, Hususan Kama Anahisi Wewe Ni Mwanamke Maridadi.

Kwa Hulka, Lazima Tu Kijana Wa Kiume Atataka Kujionesha Kwa Watu Anapokuwa Na Kimwana Maridadi Na Anayempenda Kwa Dhati. Usipoona Dalili Zozote Za Jambo Hili, Basi Chukulia Tu Kuwa Kijana Huyu Wa Kiume Hajakupenda Kama Unavyodhani.

5.HUEPUKA WATU KUWAONA PAMOJA

Mwanamume Asiye Na Mpango Wa Kuendelea Kuwa Nawe Katika Uhusiano, Hujitahidi Kuepuka Watu Kuwaona Pamoja. Ni Kweli Kuwa Si Vijana Wote Wa Kiume Wanaopenda Mapenzi Ya Maonesho Ya Kushikana Mikono Wanapotembea, Lakini Kama Ameridhika Nawe Lazima Tu Kwa Kiasi Fulani Atataka Umma Ujue.

Kwa Hakika, Kijana Wa Kiume Anapokuwa Amempenda Msichana Kwa Dhati, Hujikuta Akifanya Hata Mambo Ambayo Zamani Alikuwa Hadhani Kuwa Anaweza Kuyafanya, Ikiwa Ni Pamoja Na Kuonesha Mapenzi Hadharani, Japo Kwa Idhara Ndogo Ndogo. Kwa Tamaduni Za Magharibi Ni Kawaida Kumbusu Mpenzi Hadharani Au Kumzungushia Mkono Kiuononi, Au Kumshika Mkono, Au Kumbusu. Lakini Afrika Hata Kutoka Naye Nje Mkizungumza Huwafanya Watu Washuku Jambo. Kama Hukuliona Hilo Kwa Mpenzi Wako, Basi Chukulia Tu Kuwa Unapoteza Muda.

6.HAZUNGUMZII MIPANGO YA BAADAYE

Unapokuwa Unazungumza Na Mwanamume Ambaye Ana Mpango Wa Kuwa Nawe Katika Kipindi Chake Cha Maisha Yaliyobaki, Lazima Tu Utambaini Akiingiza Mambo Yanayohusiana Na Maisha Ya Baadaye Mkiwa Pamoja. Kwa Hakika, Utambaini Mwanamume Huyu Akitumia Nafsi Ya Kwanza Wingi Tena Katika Muda Wa Baadaye, Yaani Akizungumza Mambo Ambayo Atafanya Na Wewe Miaka Ijayo.

Iwapo Atazungumzia Klabu Fulani Aliyoiona Karibuni Lakini Akawa Hagusii Kuwa Mtakwenda Huko Siku Moja – Tena Mbaya Zaidi Akawa Anasema Kuwa Huwa Anakwenda Pale Mara Kwa Mara, Basi Tambua Kuwa Hauko Katika Mipango Yake Ya Baadaye.

7.HAKUNA MATENDO YA MAHABA

Mwanamume Asiye Na Mpango Wowote Na Wewe Si Aghalabu Kukufanyia Jambo Ambalo Utaliona La Kimapenzi Au La Kimahaba, Hususan Anapokuwa Amefanikiwa Kufanya Mapenzi Na Wewe. Ukiona Hivi, Shtuka Mapema Na Anza Kuangalia Ustaarabu Mwingine.

Haina Maana Kuwa Asipokununulia Maua Basi Hana Mpango Nawe, Lakini Angalau Mara Moja Moja Akufanyie Jambo Au Angalau Atoe Kauli Ambayo Itakusisimua Na Kukufanya Ujione Wa Thamani Na Wa Pekee Machoni Pake.

8.MIPANGO UNAPANGA WEWE

Iwapo Utabaini Kuwa Asilimia 80 Ya Mambo Mnayofanya Pamoja Unayaanzisha Wewe, Basi Una Kila Sababu Ya Kuutilia Shaka Mustakabali Wa Uhusiano Wenu.

Kama Ilivyobainishwa Awali, Mwanamume Akikupenda Atataka Muwe Pamoja Muda Mwingi, Lakini Kama Utabaini Kuwa Mipango Mingi Unaanzisha Wewe Na Unazungumza Naye Kwenye Simu Ijumaa Na Mnamaliza Bila Mwanamume Huyu Kuonesha Dalili Za Kutaka Kuwa Nawe Wikiendi, Japo Kwa Kinywaji, Basi Chukulia Kuwa Mwanamume Huyu Hana Nia Yoyote Ya Kuwa Nawe Kwa Muda Mrefu Zaidi.

9.HANA MPANGO NA WATU WAKO

Mwanamume Anayekupenda Atajishughulisha Na Mambo Yanayohusiana Na Watu Wako Wa Karibu, Hususan Ndugu, Jamaa Na Marafiki Zako. Iwpao Utabaini Kuwa Mwanamume Huyu Haulizi Swali Lolote Kuhusiana Na Familia Yako Au Marafiki Zako, Basi Tambua Kuwa Hana Mpango Wowote Wa Maana Na Wewe. Kumbuka Mwanamume Akikupenda Hujaribu Kuwafahamu Na Kuwapenda Watu Wako, Maana Amependa Boga Na Sheria Ni Kwamba Lazima Upende Na Ua Lake.

10.HAKUMBUKI LOLOTE LA MAANA

Ni Wazi Kuwa Hujakaa Sana Na Mwanamume Huyu, Lakini Angalau Kuna Mambo Muhimu Umefanya Naye Ambayo Anapaswa Kuyakumbuka. Kama Hawezi Kukumbuka Tarehe Muhimu Za Uhusiano Wenu, Mathalani Tarehe Mliyokutana Mara Ya Kwanza, Au Siku Mliyofanya Mapenzi, Basi Yamkini Mwanamume Huyu Hana Mpango Wowote Wa Dhati Wa Kuendelea Kuwa Nawe.

USIPOTEZE MUDA

Hakuna Mtu Mwenye Lengo La Kukuvunja Moyo, Lakini Ujumbe Ulio Dhahiri Ni Kwamba, Kama Unafikiria Uhusiano Wa Kudumu Na Mtu Kisha Akawa Anaonesha Ishara Zilizobainishwa Hapa, Basi Tambua Tu Kuwa Huyo Si Wako Na Atakupotezea Muda Wako Bure. Wala Usijaribu Kumlazimisha, Maana Mambo Ya Kulazimisha Huwa Hayadumu.

Ni Muhimu Sana Kuhakikisha Kuwa Mtu Unayetaka Kujenga Naye Uhusiano Wa Kudumu Anakupenda Kwa Dhati. Wala Haipendezi Kumng’ang’ania Mtu Ambaye Mapenzi Yake Kwako Ni Nusu Nusu. Hakikisha Kuwa Mtu Unayempenda Na Unayetaka Kuwa Naye Ni Yule Ambaye Amekuzimikia Na Atamani Sana Kuwa Nawe. Mtu Huyu Utampata, Hususan Kama Wewe Mwenyewe Utaweka Jitihada Za Makusudi Na Kujiweka Katika Hali Ya Kupendwa Na Kupendeka.....
Hizi ni dalili tu si lazima sana ziwe na ukweli kwa asilimia zote itategemea na mtu alivyo, alivyolelewa na mazingira aliyopo......

MAMBO MUHIMU YA KUYAFAHAMU ILI KUEPUKA KUSALITIWA.1.Amini Hawezi Kukusaliti
Jambo La Kwanza Kabisa Ni Kujenga Imani Kwamba Mpenzi Wako Anakupenda, Anakuheshimu Na Kukuthamini Hivyo Hawezi Kushawishika Kwa Namna Yoyote Ile Kukusaliti.

Hii... Itakufanya Kuwa Na Furaha Na Yeye, Pia Utamfanyia Mambo Ya Kumfurahisha. Ukiwa Huna Imani Na Mpenzi Wako, Unaweza Kujikuta Unapunguza Mapenzi Kwake Na Matokeo Yake Ukachochea Yeye Kuanza Kukusaliti. Punguza kumpekua pekua utagundua mengi yatakayokukosesha raha bureee....kama anataka ujue utayajua tu usijipe jakamoyo bure.....

2.Mtosheleze
Mpenzi Wako Mchukulie Kama Mtoto. Unapomlisha Unahakikisha Ameshiba Ndiyo Unamuacha. Akitaka Pipi Unamnunulia. Vivyo Hivyo Kwa Mpenzi Wako. Mtoshelezea Katika Kila Nyanja.

3.Muoneshe Upendo Wa Hali Ya Juu, Mpe Heshima Anayostahili Na Pale Mnapokuwa Kwenye Mambo Yetu Yalee, Mpe Hadi Aseme Nimeshiba Mpenzi Wangu. Ukifanya Hivyo Aende Nje Kutafuta Nini? Akienda, Huyo Ana Tamaa Zake Za Kijinga Na Ukibaini Muache Haraka kama hajutii makosa yake.

4.Zungumza Naye
Ndiyo, Vunja Ukimya, Zungumza Naye! Si Vibaya Ukawa Unazungumza Na Mpenzi Wako Juu Ya Mambo Yahusuyo Uhusiano Wenu. Muulize Ni Mambo Gani Ukimfanyia Anasikia Furaha, Akikuambia Na Mambo Hayo Yakawa Ndani Ya Uwezo Wako, Jitahidi Kumtimizia.

5.Muulize, Anachukizwa Na Mambo Gani, Akikuambia Basi Jiepushe Nayo. Hata Asipokuambia, Ukimchunguza Utayabaini Tu.
Hayo Ni Baadhi Tu Ya Mambo Ambayo Ukiyazingatia Yanaweza Kukusaidia Katika Kumfunga ‘Spidi Gavana’ Kimtindo Mpenzi Wako Ili Asikusaliti. Kama Itatokea Akakusaliti Licha Ya Kumfanyia Yote Hayo, Huyo Siyo Mtu Wa Kuendelea Kuwa Naye.
.......tutaendelea....UCHOVU ISIWE SABABU YA KUNYIMANA ‘CHAKULA CHA USIKU’


Ndani Ya Maisha Ya Ndoa, Muda Wowote Mwenzako Anapohitaji Penzi Hutakiwi Kumkatalia Kwa Kuwa Wewe Ndiye Daktari Wake Na Kumkubalia Kwako Ni Sawa Na Kumtibu Ugonjwa Ambao Ungeweza Kuyaathiri Maisha Yake.

Hata Hivyo, Asilimia Kubwa Ya Wanandoa Wanatajwa Kufanya Tendo La Ndoa Wakati Wa Usiku. Usiku Wa Saa Ngapi? Hiyo Itategemea Na Wanandoa Husika.

Lakini Sasa Inaelezwa Kuwa Wanandoa Wanaofanya Kazi Ni Vigumu Sana Kulifurahia Tendo La Ndoa Kwa Kulifanya Usiku. Hii Ni Kwa Sababu, Muda Huo Kila Mmoja Anakuwa Amechoka Kutokana Na Mihangaiko Ya Siku Nzima.

Usiku Ni Tatizo?

Wanaume Wengi Wakati Wa Usiku Ndiyo Wanautumia Kutafakari Juu Ya Maisha, Pia Ni Wakati Ambao Wanakuwa Wamechoka Hivyo Wanaweza Kukosa Mshawasha Wa Kukutana Na Wake Zao.

Ukijaribu Kufuatilia Utabaini Ndoa Nyingi Ziko Kwenye Migogoro Chanzo Kikiwa Na Wanawake Kutopatiwa Haki Zao Za Ndoa. Wanaikosa Haki Hiyo Kwa Kuwa Muda Ambao Waume Zao Wanatakiwa Kuwapa ‘Mambo’, Wanakuwa Hoi.

Mbaya Zaidi Baadhi Ya Wanawake Hufikia Hatua Ya Kuhisi Wanasalitiwa Kumbe Siyo Kweli Bali Inatokana Na Kutopatiwa Raha Hiyo Kwa Wakati Walioutarajia.

Wataalam Wa Mapenzi Wanaeleza Kuwa, Usiku Ndiyo Muda Muafaka Kwa Wanandoa Kukutana Na Kwa Mwanaume Hata Kama Atakuwa Anajisikia Hali Ya Kuchoka, Ajue Ana Wajibu Wa Kufanya Hivyo.

Kufanya Mapenzi Ni Moja Ya Mazoezi Hivyo Mwanaume Anaporudi Nyumbani Asikimbilie Kuoga, Kula Na Kulala Bali Akumbuke Kumpatia Haki Mke Wake, Haki Ambayo Pia Inamsaidia Kimazoezi.

Inaelezwa Kuwa, Mwanaume Kujihisi Uchovu Kila Siku Na Kushindwa Kufanya Tendo La Ndoa Ni Dalili Kwamba Ana Tatizo La Kiafya Analotakiwa Kulitafutia Ufumbuzi Haraka Kabla Ya Kuiathiri Ndoa Yake.

Mapenzi Ni Starehe

Ifahamike Kwamba, Kufanya Mapenzi Licha Ya Kwamba Unatumia Nguvu Na Akili Lakini Ni Sehemu Ya Kustarehe. Ndiyo Maana Wengine Baada Ya Kumaliza Shughuli Zao Za Siku Nzima Badala Ya Kwenda Baa, Moja Kwa Moja Wanakwenda Nyumbani Na Wakifika Huko Wakioga Wanaweza Kutumia Muda Mwingi Kitandani Na Wenza Wao.

Kwa Maana Hiyo Kukutana Faragha Isichukuliwe Kama Kitu Kitakachokufanya Uzidi Kuchoka Bali Kwa Kutumia Kanuni Sahihi, Uchovu Hauwezi Kuwa Sababu Ya Kutomtimizia Mwenzake Haki Yake Ya Ndoa.

Mwanaume Afanyeje?

Zipo Njia Mbalimbali Za Kukabiliana Na Hali Ya Uchovu Na Leo Nitazungumzia Mbili Ambazo Naamini Ukizifanyia Kazi Zinaweza Kukusaidia.

Kunywa Kahawa

Wapo Wanaoitumia Kama Njia Ya Kuwafanya Wasilale Usiku Lakini Pia Kitaalam Inaelezwa Mtu Anapokunywa Kahawa Kabla Ya Kupanda Kitandani Inamsaidia Kuondoa Uchovu.

Aidha, Kahawa Ina Uwezo Wa Kumfanya Mtu Apate Mshawasha Wa Kufanya Tendo La Ndoa Hata Kama Ametoka Kwenye Kazi Zilizomfanya Achoke Sana.

Mazingira Ya Kutokuwa Mchovu Yatamfanya Aweze Kumtimizia Mke Wake Haki Yake Ya Ndoa Bila Wasiwasi. Cha Kuzingatia Katika Hili Ni Kunywa Kahawa Kiasi Ili Isikuletee Madhara Badala Ya Faida.

Tumia Zabibu Za Baridi

Wataalam Wanaeleza Kuwa, Zabibu Hasa Za Baridi Zinaweza Kukuweka Katika Mazingira Mazuri Ya Kukutana Faragha Na Mwenzako Na Kushibishana Chakula Cha Usiku.

Ukiwasili Nyumbani Kutoka Kazini Na Kuhisi Hali Ya Kuchoka. Baada Ya Kuoga Ukiwa Umepumzika Kula Tunda Hilo Taratibu, Faida Yake Utaiona Utakapokuwa Kitandani Na Mwenza Wako.

Zingatio

Kukutana Faragha Ni Mhimili Muhimu Katika Kuidumisha Ndoa. Visingizio Visivyo Na Msingi Visitumike Kunyimana Utamu Huu. Kama Umechoka Basi Ujue Ukifanya Mapenzi Na Mwenzako Uchovu Utaondoka, Kama Hujisikii Kufanya Hivyo Mwenzako Atakupa Stimu Lakini Usipuuzie Hisia Zake.............tutaendelea......HERI UPWEKE KULIKO MPENZI ASIYEJUA MAANA: (SEHEMU YA TATU)

 
 

 

Katika Somo Lililopita Kama Nilivyogusia Ushauri Wa Brandon King Na Makala Yake Ya “Be Aware With Ones Heart” Nilieleza Kuwa Ni Kosa Kubwa Kumuona Mwenzi Wako Ana Thamani Ndogo Na Wakati Huo Huo Ukawa Unatoa Kipaumbele Kwa Watu Wa Pembeni.

Tafsiri Inayotawala Katika Uhusiano Ni Kuwa Kundi Linalosumbua Mno Na Kuonekana Ni Sugu Kwa Tabia Ya Namna Hii Ni Lile Ambalo Linawahusisha Memba Wanaoingia Kwenye Uhusiano Wa Kimapenzi Pasipo Imani Kamili.
Wanajaribu Na Hawana Ufahamu Kwamba Moyo Haufanyiwi Majaribio.
Hii Ndiyo Sababu Ya Kusisitiza Kuwa Ikiwa Hujaamua Kupenda Basi Kaa Mbali.

Kuna Mengi Unayoweza Kumsababishia Mwenzako, Ukampotezea Muda Huku Ukimjengea Imani Upo Naye Lakini Mwisho Anakuja Kujikuta Anauguza Dondo La Moyo.
Sikitiko La Mahaba Linashinda Msiba!
Hujaumia Subiri Usimuliwe!

Moyo Unapouma Kwa Sababu Ya Mapenzi Hakuna Kitu Cha Kupoza. Unaweza Kunywa Pombe Na Usilewe, Ukabugia Dawa Za Usingizi Na Usilale.
Kifua Kinajaa Na Kwa Sababu Inaathiri Mfumo Wa Upumuaji Na Mapafu Nayo Huingia Katika Maumivu.
Sikitiko La Mahaba Ni Hatari, Likikufika Utapungua Uzito Kwa Kasi Bila Maelezo Ya Ziada.

Chakula Hakiwezi Kupita Na Macho Yanaweza Kujaa Machozi Ilhali Unatamani Kujizuia. Binadamu Tumetofautiana, Wapo Wanaotamani Kupendwa Lakini Wengine Wanawacheza Shere Wanaowapenda.
Dawa Kuu Ni Kujihadhari Na Watu Wasio Na Mapenzi Ya Dhati.

Kuwaepuka Kadiri Inavyowezekana.

Ni Mzuri Na Anakuvutia Lakini Heri Umuone Kwa Mbali Kwa Sababu Ukimjaza Moyoni Atakusumbua.
Atakutoa Machozi Katika Eneo Ambalo Ulihitaji Kufurahi.
Maumivu Yako Hata Yajali Kwa Sababu Hana Hisia Na Wewe.

Atakusaliti Bila Woga Kwa Maana Hana Hofu Yoyote Juu Yako.
Itakuwa Ngumu Kumuacha, Vilevile Utaona Uamuzi Wowote Wa Kutengana Naye Ni Mateso Makubwa Kwamba Heri Uumie Ukiwa Naye Kuliko Kuachana.

Usijidanganye Ndugu Yangu, Wewe Ni Binadamu Uliyekamilika, Kwa Hiyo Usitarajie Mtu Wa Pili Au Wa Tatu Anaweza Kusikia Kile Kinachokuuma Moyoni.

Mateso Yaliyopo Ndani Yako Unayajua Mwenyewe, Kwa Hiyo Unatakiwa Kuwa Wa Kwanza Kujihurumia Na Kuchukua Uamuzi Wa Kujiokoa Na Mateso.

Kuna Kitu Kimoja Ambacho Unatakiwa Kukifahamu; Binadamu Ni Wa Ajabu Sana, Watayajua Yako Ya Siri Na Kile Ambacho Mwenzi Wako Anakifanya Pembeni, Lakini Hawakwambii Badala Yake Wataketi Pembeni Kuzungumza. “Aah Yule Wa Ajabu, Anadhani Kapata Mpenzi Kumbe Kapatikana!”

Wengine Utakaa Nao Meza Moja Kushauriana Mambo Mbalimbali, Lakini Anayekwambia Umvumilie Mwenzi Wako Licha Ya Vitimbi Anavyokufanyia, Ndiyo Huyo Huyo Akikaa Pembeni Na Watu Anawaambia Kwa Mtindo Wa Kukucheka Kwamba Unamng’ang’ania Mpenzi Bomu.

Lingine Ni Kuwa Unapokuwa Na Mpenzi Ambaye Hakuheshimu, Thamani Yako Katika Jamii Inashuka.
Kukuheshimu Si Mpaka Akutukane, Bali Vitendo Vyake. Kutoka Na Wapenzi Wengine, Kujenga Mazoea Na Watu Wa Jinsia Nyingine Kiasi Kwamba Mpaka Anahusishwa Kwamba Ni Wapenzi Wake.

Mathalan, Mpenzi Wako Anakuwa Na Urafiki Na Watu Mpaka Anafikiriwa Anatembea Nao.
Hii Ni Tabia Mbaya Na Haikubaliki, Ingawa Wapo Wazuri Wa Kutetea. Watasema, Sisi Ni Washkaji Ila Fahamu Mapenzi Yenu Yanazikutanisha Familia Mbili. Una Ndugu, Marafiki, Wazazi.

Inakuaje Mpenzi Wako Anahisiwa Anatoka Na Mwanamke Mwingine Na Taarifa Zinafika Mpaka Kwa Wazazi Wako? Watajua Mkwe Wao Ni Kicheche Na Hilo Litakugharimu Kwa Kiasi Kikubwa.

Unatakiwa Kulinda Thamani, Heshima Na Utu Wako, Kwa Hiyo Achana Na Mtu Asiyejua Maana!
Unaweza Kuona Leo Inakuuma Kwa Sababu Unaepukana Na Mtu Ambaye Unampenda Lakini Hiyo Ni Nafuu Kwako Kesho.
Amini Kwamba Mwisho Wa Mateso Hayo Ya Moyo Ni Furaha Kubwa, Mwisho Utajiuliza:

Ni Kipi Kilichokuwa Kinakufanya Uumie Kwa Muda Wote? Upo Huru Sasa!
Mapenzi Maana Yake Utulivu Wa Moyo, Yaani Wewe Na Mtu Wako Spesho Muogelee Katika Dimbwi Maalum, Ninyi Wote Mkiwa Na Amani.

Mkishirikiana Katika Hali Zote. Inakuwa Hakuna Anayewaza La Kwake Peke Yake Isipokuwa Kwa Ajili Yenu.
Ukilia Anakuwa Wa Kwanza Kukubembeleza, Anapogundua Amekuudhi Ni Mwepesi Kukuomba Msamaha.
Anasoma Mabadiliko Yako Na Kukuuliza Kile Kinachokusumbua.
Anaficha Siri Zako, Anazungumza Lugha Tamu Na Hisia Zake Zote Zipo Kwako. Kwa Wengine Haoni Hatamani.

USITHUBUTU KULAZIMISHA PENZI

Yamewafika Wengi Na Wameumia, Kwa Hiyo Ni Vizuri Kuwa Makini.
Utauguza Donda La Moyo Lisiloweza Kutibika, Utakonda Wenzako Watakucheka, Atakugeuza Punda Afanye Anachokitaka.
Ni Kazi Bure Kumpenda Mtu Asiyekupenda.
Pamoja Na Maumivu Unayoweza Kuyapata Lakini Kuna Vitu Hivi Lazima Vikukute Kwa Huyo Mwenzi Wako Wa Kulazimisha.

ATAKUTESA KWA UBINAFSI WAKE

Hana Mapenzi Ya Kweli Na Wewe, Kwa Hiyo Si Kila Wakati Atakufikiria.
Kama Hamjawa Kwenye Ndoa Itakusumbua Kwa Sababu Ni Ngumu Kufikiria Kwa Ajili Yenu, Isipokuwa Atawaza Kwa Matilaba Yake. Kama Kuoana, Utalazimisha Wewe Lakini Yeye Hatokuwa Na Habari.

Mkiwa Kwenye Ndoa, Hatojisikia Fahari Kutoka Na Wewe Atalazimisha Maisha Ya Kila Mmoja Kuwa Huru Kufanya Mambo Yake.
Nguo Atanunua Za Kwake Na Hata Siku Moja Hutoona Amekununulia. Wewe Utafanya Mengi Kwa Ajili Yake Lakini Yeye Atabaki Na Ubinafsi Wake.
Atakutesa, Pasha Moto Ubongo!

AKIONA WENGINE ATAHISI NI WAZURI ZAIDI YAKO!

Mtu Huishi Kwa Fikra Zake, Kwa Hiyo Kwa Sababu Hakupendi Kwa Moyo Wake Wote Inakuwa Ngumu Kukukubali, Hivyo Anapokutana Na Watu Wengine Barabarani Atadhani Ni Wazuri Kuliko Wewe. Atababaika Hata Mbele Yako.

Unahitaji Heshima Ya Kiwango Bora Na Kwa Kawaida Mpenzi Wako Anapaswa Kukuona Wewe Ni Mtu Namba Moja.
Kama Hakupi Nafasi Hiyo Maana Yake Anapenda Nusunusu Au Hapendi Kabisa.
Usikaribishe Mateso, Fikiria Kesho, Chukua Uamuzi Leo.

HASIFU MUONEKANO WAKO, ANA LAKE KICHWANI!
Hujiulizi, Kila Siku Anakuona Na Hakusifii! Ni Wazi Kuwa Hata Kama Wewe Ni Mzuri Kiasi Gani, Unavaa Na Kupendeza Kwa Namna Bora Kabisa Lakini Mwenzi Wako Hawezi Kukupa Pongezi Kwa Sababu Ana Lake Kichwani.

Ukiona Hilo Ujue Kwamba Yupo Mtu Ambaye Anamsifu Kwa Sababu Ndiye Anayemkubali, Na Wewe Utasifiwa Na Wengine.
Inauma Mwenzi Wako Kukuacha Nyumbani Na Kwenda Kumwaga Sifa Pembeni, Wakati Na Wewe Unazihitaji.
Una Thamani Kubwa, Pigania Utulivu Wa Moyo Wako!.......HERI UPWEKE KULIKO MPENZI ASIYEJUA MAANA: (SEHEMU YA PILI)

KILA Mtu Angeyaheshimu Mapenzi, Angejua Jinsi Ya Kulinda Hisia Za Mwenzi Wake. Angeelewa Maana Ya Kupenda, Asigekuwa Na Shaka Pale Anapopendwa. Angeishi Ndani Ya Mwenzake, Hivyo Kuumizana Kusingekuwepo, Migogoro Mikubwa Na Kuachana Isingetokea.

Migogoro Mingi Inatokea Kwa Sababu Wengi Wameyageuza Mapenzi Kama Mchezo (Game), Hawajui Kuwa Saikolojia Inaonya Vitendo Vya Kuucheza Shere Moyo Wa Mtu. Kumfanyia Hivyo Mtu Mwenye Hisia Za Ndani Na Za Kweli Katika Kupenda Unaweza Kuua Bila Kukusudia.

Katika Sehemu Ya Kwanza Ya Makala Haya Nilieleza Kuwa Kama Hujawa Tayari Kupenda, Kunyenyekea Na Kuheshimu Ni Vizuri Ukakaa Pembeni Kwa Sababu Unaruhusiwa Kucheza Game Na Mtu Lakini Ni Kosa Kubwa Kucheza Game Na Moyo Wa Mtu.

Hata Hivyo, Nilitaka Kila Mtu Awe Makini Anapokuwa Anaingia Kwenye Uhusiano Wa Kimapenzi Na Mtu. Anapaswa Kujihakikishia Upendo Kutoka Moyoni Badala Ya Kujaribu. Wengi Walioingia Kwa Mtindo Wa Kupima Kina Cha Maji, Walilia Kwa Kusaga Meno.

Lipo Tabaka Ambalo Linakuwa Limejitosheleza Kuwa Mapenzi Hamna Lakini Wanang’ang’ania, Matokeo Yake Wanauguza Jeraha La Moyo Kwa Muda Mrefu. Wengine Wakajipa Ugonjwa Wa Moyo. Ni Vizuri Kuwa Makini Mno Ikiwa Unahitaji Kupata Thamani Halisi Ya Penzi.

Pigania Kuhifadhi Moyo Wako. Uweke Katika Himaya Salama. Usijidanganye Kwa Penzi Lisilo Na Uelekeo. Lenye Sura Ya Upande Mmoja. Wewe Unapenda, Yeye Anakuchora, Presha Inakupanda Na Kushuka Mwenzako Hana Habari Hata Kidogo, Tena Ikiwezekana Atakucheka Kama Katuni.

Kuna Watu Hawaoni Hili Umuhimu, Mpenzi Maana Yake Ni Msiri Wa Maisha Yako. Unapokuwa Umelala Fofofo Hujitambui, Ubavuni Kwako Yupo Yeye. Anaweza Kukufanya Lolote Wakati Wewe Unaogelea Ndotoni. Mpende Akupendaye, Vinginevyo Utakumbana Na Maumivu Yafuatayo;

HATAKUSIKILIZA IPASAVYO

Mapenzi Ni Hisia. Ni Rahisi Kwako Kujua Kwamba Uliyenaye Anakupenda Kwa Dhati Mnapokuwa Mnazungumza. Je, Anakusikiliza Kiasi Gani?

Mtu Ambaye Hana Mapenzi Na Wewe, Hata Umwambie Kwa Lugha Gani Hawezi Kukuelewa. Tena Inawezekana Ulizungumza Naye Jana Kwa Herufi Kubwa, Lakini Leo Jua Limechomoza Anarudia Yale Yale.

Inawezekana Ulimuonya Kuhusu Tabia Ambazo Zinakufanya Heshima Yake Ipotee. Hakatazwi Kuwa Na Marafiki Wa Jinsia Nyingine, Lakini Mazoea Yake Siyo Mazuri Kiasi Kwamba Wanaweza Kutembea Barabarani Wameshikana Viuno. Ikiwa Unamueleza Habadiliki, Huyo Hakupendi.
Hakusikilizi Kwa Sababu Hana Hisia Na Wewe.

ATAPENDA KUKUFANANISHA

Haamini Kama Wewe Ni Mwanamke Au Mwanaume Mwenye Mvuto Kamili. Akiona Wengine Barabarani Ni Rahisi Kushawishika. Atajiuliza Hivi Huyu Na Wangu Vipi? Huyu Anaonekana Ni Mzuri Zaidi. Anajiuliza Maswali Hayo Kwa Sababu Hajakukubali. Shtuka Mapema.

Mwanasaikolojia Brandon King Katika Makala Yake: “Be Aware With Ones Heart!” Anasema Kuwa Ni Rahisi Mtu Kujidanganya Kwamba Aliyenaye Siyo Chaguo Sahihi Kwa Sababu Yupo Naye Lakini Hiyo Hutokea Kwa Mtu Ambaye Mapenzi Yake Si Asimilia 100.

Anasema: “Vitu Vya Thamani Yeye Huvichukulia Ni Rahisi. Hajui Kama Mpenzi Wake Ni Wa Gharama Kubwa. Mtu Wa Barabarani Labda Kwa Sababu Tu Amevaa Kapendeza, Yeye Ataanza Kumfananisha Na Mwenzi Wake Nyumbani Na Ikiwezekana Kumuona Bora.

“Wengine Hawana Uvumilivu, Kwa Hiyo Wanaweza Kujikuta Wakimwaga Sifa Kwa Watu Wa Pembeni. Wakiendelea Huharibu Kabisa Kwa Sababu Hujikuta Wakiwaeleza Hata Wapenzi Wao, Kitu Ambacho Taaluma Ya Saikolojia Katika Eneo La Mapenzi Inakataza.”

Brandon Anaonya: “Ni Kosa Kubwa Kumsifia Mtu Wa Jinsia Inayofanana Na Mwenzi Wako Mbele Yake. Mfano Unamwambia Mwenzi Wako Wa Kiume Kwamba ‘Yule Kaka Mzuri Jamani’! Hata Kama Huna Hisia Za Ndani Ya Moyo Wako Lakini Haiwezi Kumpa Picha Nzuri, Atajiona Hayupo Salama Kwamba Unavutiwa Na Mwingine.

“Fikiria Na Wewe Upande Wako. Mwenzi Wako Anamuona Mwanamke Na Yeye Anamwagia Sifa, ‘Dah Yule Manzi Mrembo, Wewe Ungekuwa Mrembo Kama Yeye Ningejidai Sana’! Bila Shaka Utaumia Sana, Kwa Hiyo Na Yeye Ndivyo Anavyoweza Kupata Maumivu.”

Anashauri: “Kila Mmoja Aridhike Kwa Jinsi Mwenzi Wake Alivyo. Haikusaidii Kitu Kumuona Bora Wa Jirani Kwani Kuna Wenzako Wanajiuliza Huyo Wako Watampataje? Mheshimu Na Mtukuze Mbele Za Watu. Ukijenga Imani Kwamba Mpenzi Wako Ni Bora Kuliko Wote Duniani, Itakuwa Na Moyo Wako Utakubali… Itaendelea.......HERI UPWEKE KULIKO MPENZI ASIYEJUA MAANA: (SEHEMU YA KWANZA)


MAPENZI Yana Siri Kubwa. Kila Mmoja Ana Ugonjwa Wake Wa Kupenda. Wengine Wanawapenda Wapenzi Warefu, Lakini Kuna Kundi Ambalo Huchanganyikiwa Zaidi Kwa Wafupi. Pamoja Na Mchanganuo Huo, Kuachwa Inauma Hata Kama Anayekutosa Hukuwa Na Mapenzi Naye.

Ile Dhana Tu Ya Kuachwa Ndiyo Hutesa Watu. Kuna Dhana Kwamba Anayeacha Mara Nyingi Hujiona Mshindi Dhidi Ya Aliyemuacha. Na Hiyo Ndiyo Sababu Ya Wengi Kuumia Wanapofungiwa Milango Ya Kukatisha Uhusiano Ambao Pengine Hata Hawakuwa Na Masilahi Nao.

Mathalan, Mwanamke Anaweza Kuwa Havutiwi Na Mtu Aliyenaye Kwa Maana Moja Au Nyingine. Ilitokea Kuwa Naye Kama Ajali Tu! Kutokana Na Kutokuwa Na Hisia Naye, Hakuona Tatizo Kumsaliti Kwa Mwanaume Mwingine, Lakini Huwezi Kuamini Siku Akiambiwa Basi, Atalia Machozi Na Kuomba Msamaha.

Si Kwamba Atalia Kwa Sababu Ya Mapenzi Ya Dhati Aliyonayo Kwa Mwenzi Wake, Kwamba Inamuuma Kuachana Naye, Ila Kinachomtesa Ni Zile Hisia Za Kuachwa. Na Ingetokea Kuwa Yeye Ndiye Anayeamua Kuacha, Tafsiri Ingekuwa Kinyume Chake.

Macho Yangekuwa Makavu Na Ikiwezekana Angekwenda Kusimulia Kwa Marafiki: “Aah, John Nimempiga Chini Kanililia Huyo!” Anafurahi Dada Yetu Na Wenzake Watampongeza Kwa Kugongesheana Viganja!

Tatizo Kubwa Ambalo Linawagharimu Wengi Ni Kuwa Mapenzi Yanabebwa Kama Aina Ya Mchezo Wa Kuigiza. Watu Wanaingia Kwenye Uhusiano Kwa Kujaribu. Kuna Waliofunga Ndoa Si Kwa Kuchaguana, Isipokuwa Walidanganyana Kwa Hisia Za “Mapozeo” Mwisho Wa Siku Wakazoeana, Ikawa Ngumu Kuachana.

Wapo Wanaoingia Kwenye Ndoa Si Kwa Kuvutwa Na Nyoyo Zao, Ila Wanakabiliwa Na Fikra Za “Waoaji Wenyewe Hawapo, Acha Nimkubali Huyu Huyu!” Mapenzi Ni Nguzo Maalum Mno Kwa Maisha Ya Binadamu, Kwa Hiyo Ni Vema Yabebe Heshima Inayostahili.

Ogopa Sana Mtu Anayekuwa Na Wewe Kwa Sababu Haoni Chaguo Lake. Adhabu Yako Ni Kubwa Mbele Ya Safari Ingawa Unaweza Kujiona Upo Kwenye Bwawa La Asali Mwanzoni. Kiama Chako Ni Pale Atakapomuona Anayedhani Ndiye Sahihi Kwake. Utasilitiwa Upende Usipende!
Nimekuwa Nikisisitiza Hili Kuwa Ni Bora Kuacha Kumsogelea Kabisa Kuliko Kumdanganya Unampenda Wakati Unamcheza Shere. Ukatili Wako Ni Mkubwa Kwa Maana Yeye Anaweza Kudhani Amefika Na Akatuliza ‘Mizuka’ Yote, Hivyo Akapandikiza Matarajio Juu Yako.

Siku Atakapojua Haupo Naye Atajisikiaje? Unaweza Kuua Bila Kukusudia Kwa Sababu Binadamu Tumeumbwa Na Roho Tofauti. Utamuona Aliyekunywa Sumu Kwa Mapenzi Ni Mjinga Kwa Sababu Hayajakufika. Kuna Waliosema Wao Ni Ngangari Lakini Ukurasa Ulipofunguka Kwao, Waliona Dunia Chungu.

USIJARIBU MAPENZI
Dhana Ya Mapenzi Duniani Kote Inaelekeza Kwamba Asili Yake Ni Moyoni. Hii Ina Mantiki Kuwa Ndani Ya Kila Mtu Kuna Vitu Ambavyo Anahisi Kuhitaji Mwenzi Wake Awe Navyo. Sura, Umbo Na Tabia.

Hata Hivyo, Kuna Nakshi Nyingi Ambazo Si Za Lazima Lakini Hutokea Kuwavutia Watu Na Kufunika Hata Yale Ya Msingi.

USHAURI: Zingatia Sifa Muhimu Na Kuachana Na Vionjo Vya Ziada (Accessories).
Kuna Mwanamke Yeye Huvutiwa Na Mwanaume Mwenye Kucha Ndefu.

Ukimuuliza, Anakwamba Basi Tu Napenda. Mwingine Anaweza Kusema: “Nikiwa Naye Napenda Kuichezea, Naskia Raha!” Yupo Atakayekueleza: “Ile Kucha Yake Akinipitishia Mgongoni Au Shingoni Kwangu Taabani!”

Ni Vionjo Tu Vya Ziada! Kuna Wasiotaka Mambo Mengi Ila Wakikutana Na Watu Ambao Wananukia Ni Balaa! Wapo Watakaosema Wanataka Wachangamfu, Ingawa Mapepe Yakizidi Nayo Ni Tatizo Kubwa, Ila Mwingine Atadai Anahitaji Mpenzi Anayejua Kiingereza.

Ipo Sifa Nyeti Kwenye Dimbwi La Mahaba. Kama Karata Zako Unazicheza Vizuri Kwa Mwandani Wako Na Kuhakikisha Kila Mnapoachiana Anakuwa Ameridhika Kwa 100% Ni Turufu Ya Kulinda Penzi Lako.

JAMBO MUHIMU KWAKO

Penda Kujiona Mtu Nambari Moja Kwa Ubora Kwa Sababu Mungu Aliona Una Umuhimu Ndiyo Maana Akakuumba. Linda Thamani Na Heshima Yako, Usikubali Mapenzi Yakuondolee Nguvu Ambayo Mfalme Wa Mbingu Na Ardhi Amekupa.

Ni Rahisi Kudharauliwa Ikiwa Utakuwa Na Mtu Ambaye Hana Mapenzi Ya Dhati Na Wewe. Atakusaliti, Watu Watazungumza Pembeni. Atakusema Vibaya, Ukipita Mitaani Utaonekana Kituko. Mpenzi Mwenye Uelewa Na Anayekupenda Kwa Dhati, Atakulinda Mahali Popote.

Hatakusaliti, Ataishi Ndani Yako. Linalokuuma, Litamtesa. Wasiokupenda Atawachukia. Marafiki Zako Atawageuza Ndugu. Kinyume Chake Ni Kwamba Mwenzi Asiyekupenda Kwa Dhati, Si Ajabu Akashiriki Kukumaliza.

Kuna Watu Hawaoni Hili Umuhimu, Mpenzi Maana Yake Ni Msiri Wa Maisha Yako. Unapokuwa Umelala Fofofo Hujitambui, Ubavuni Kwako Yupo Yeye. Anaweza Kukufanya Lolote Wakati Wewe Unaogelea Ndotoni. Mpende Akupendaye, Vinginevyo Utakumbana Na Maumivu Yafuatayo;

HATOKUSIKILIZA IPASAVYO

Mapenzi Ni Hisia. Ni Rahisi Kwako Kujua Kwamba Uliyenaye Anakupenda Kwa Dhati Mnapokuwa Mnazungumza. Je, Anakusikiliza Kiasi Gani?

Mtu Ambaye Hana Mapenzi Na Wewe, Hata Umwambie Kwa Lugha Gani Hawezi Kukuelewa. Tena Inawezekana Ulizungumza Naye Jana Kwa Herufi Kubwa, Lakini Leo Jua Limechomoza Anarudia Yale Yale.

Inawezekana Ulimuonya Kuhusu Tabia Ambazo Zinakufanya Heshima Yake Ipotee. Hakatazwi Kuwa Na Marafiki Wa Jinsia Nyingine, Lakini Mazoea Yake Siyo Mazuri Kiasi Kwamba Wanaweza Kutembea Barabarani Wameshikana Viuno. Ikiwa Unamueleza Habadiliki, Huyo Hakupendi.

Hakusikilizi Kwa Sababu Hana Hisia Na Wewe…. Itaendelea…


Ukimsaliti Mpenzi Wako, Utafaidi Nini?

 Hebu Nifuatilie Kwa Makini Sana Na Nina Imani Kuna Kitu Utajifunza...

Kama Kuna Kitu Kinachukiwa Na Wengi Katika Mapenzi, Basi Ni Usaliti. Ni Kilio Cha Wengi. Vijana Kwa Wazee, Wote Hawa Hawataki Kusalitiwa. Usaliti Una Maumivu Makali. Kiukweli Kila Mmoja Huwa Anajisikia Vibaya Sana Anaposalitiwa.
Wengi (Hasa Wanawaume) Baada Ya Kuwasaliti Wapenzi Wao Huwa ...Na Maamuzi Mazito Sana. Wakati Mwingine Hufikia Uamuzi Wa Kukatisha Uhusiano Kwa Sababu Hiyo. Unadhani Ni Kwa Nini Wanachukua Uamuzi Huo Mgumu? Hakuna Kingine Zaidi Ya Maumivu.

Unajua Kuna Watu Ambao Huumia Na Kuchukia Sana Wanaposalitiwa, Lakini Wao Ni Wasaliti Namba Moja. Kwa Nini Wanafanya Hivyo?

Je, Kwa Kufanya Hivyo Wanafaidika Nini? Hebu Nizungumze Na Wewe Rafiki Yangu Ambaye Una Tabia Hiyo Mbaya Ya Kusaliti, Unajisikiaje Unaposaliti? Amani? Kuna Faida Unayoipata Kwa Kusaliti Kwako?

Binadamu Wote Sawa
Kuna Mambo Mengi Ambayo Mpenzi Akifanyiwa Na Mwenzake Lazima Ataumia Sana. Ingawa Kuna Mengine Yanafichwa Au Kupasishwa Kama Sahihi, Lakini Ukweli Unabaki Pale Pale Kwamba Yanaumiza.

Kikubwa Ambacho Unatakiwa Kufahamu Ni Kwamba Maumivu Hayo Yapo Sawa Kwa Kila Mmoja. Haijalishi Jinsi, Umri, Kabila Wala Dini, Maumivu Ya Mapenzi Yote Yanafanana. Kufanana Huko Kunasababishwa Na Mioyo Yote Kuwa Na Nyama!
Kwa Sababu Mioyo Yote Ina Nyama Basi Unatakiwa Kufahamu Kwamba, Jinsi Unavyoumia Wewe Moyoni Mwako, Ndivyo Mpenzi Wako Anavyoumia Ikiwa Utamkwaza Kwa Namna Yoyote.

Vipi Ukisalitiwa?

Unajua Kabisa Una Mpenzi, Tena Inawezekana Wakati Mwingine Mmeshawahi Kuzungumza Juu Ya Kuishi Pamoja, Lakini Bila Haya Wala Aibu, Unamsaliti! Kwa Nini Unafanya Hivyo? Kama Umeona Hana Thamani Tena Kwako, Kwa Nini Unazidi Kumpotezea Muda?
Unafikiri Anafurahia Sana Wewe Kuwa Na Kimada Mwingine Huko Uchochoroni Au Unadhani Atafurahi Siku Akijua Kuwa Una Mtoto Umezaa Nje Ya Ndoa Yako? Nafsi Yako Yenyewe Inakusuta, Inajua Ni Kiasi Gani Unamkosea Mpenzi Wako Lakini Unajifanya Kichwa Ngumu Na Kuendelea Na Uchafu Wako. Kwa Nini Hutaki Kubadilika?

Hebu Jitoe Katika Nafasi Yako, Kisha Mfanye Mpenzi Wako Ndiyo Wewe, Halafu Fikiria Kama Yeye Ndiyo Angekuwa Anakusaliti, Ungejikiaje? Lazima Utaumia! Sasa Kama Utaumia Kwa Nini Unaendelea Kumfanya Mwenzako Akose Raha?

Lazima Uwe Na Moyo Wa Huruma, Akili Yako Ifanye Kazi Ipasavyo Na Kugundua Makosa Unayoyafanya Kisha Kufanya Mabadiliko Ya Haraka. Amini Jinsi Utakavyoumia Kwa Kufanyiwa Mabaya Na Mwenzako Ndivyo Mpenzio Anavyoumia Kwa Mabaya Unayoyafanya.
Wengi Wamekuwa Wakiwasaliti Wapenzi Wao Wakiwa Hawafikirii Siku Ya Wao Kufanyiwa Hivyo Itakavyokuwa. Hebu Vuta Picha, Unakwenda Nyumbani Kwa Mpenzi Wako, Unagonga Mlango Haufunguliwi!

Lakini Baadaye Unahisi Kama Ndani Kuna Watu, Hilo Linaingia Akilini Mwako Baada Ya Kuona Viatu Vya Mpenzi Wako Pamoja Na Viatu Vingine Vya Jinsi Tofauti Ya Mpenzi Wako. Unaamua Kusukuma Mlango Na Kuingia Ndani, Hamadi! Unakuta Mpenzio Akiwa Anafanya Mapenzi Na Patna Mwingine...Utajisikiaje?
Mapenzi Ya Kweli Hayaambatani Na Usaliti. Penzi La Kweli Lina Uaminifu Wa Dhati, Kuchukuliana, Kupendana, Kusaidiana, Ukarimu, Huruma Na Mengine Mengi Ambayo Huyafanya Mapenzi Yazidi Kuwa Imara Kila Siku.

Hakuna Mwenye Haki Ya Kusaliti
Acha Kujiwazia Mwenyewe, Kujiona Wewe Pekee Ndiye Mwenye Haki Ya Kuwa Salama Katika Penzi Lako. Chunga Nafsi Yako Lakini Wakati Huo Huo Ukiangalia Kwa Jicho La Tatu, Nafsi Ya Mwenzako.

Kila Mmoja Anaumia Anapohisi Anasalitiwa, Hivi Unafikiri Ni Nani, Anayependa Kushea Mapenzi? Nani Mwenye Haki Ya Kumsaliti Mwenzake? Kimsingi Hakuna. Utakuta Mwingine Simu Ya Mpenzi Wake Ikiita Yeye Anakuwa Wa Kwanza Kuichukua Na Kutaka Kupokea Au Kusoma Sms, Lakini Subiri Sasa Simu Yake Iite; Anakuwa Mkali Huyo! Acha Kujifikiria Peke Yako.

Zingatio La Mwisho
Siamini Kama Kuna Ambacho Sijaandika Katika Vipengele Vyote Vinne Vilivyopita, Lakini Hapa Nakusisitiza Ufanye Mabadiliko Ya Haraka Ili Mwisho Wa Siku Uweze Kuishi Maisha Mapya, Mazuri, Yenye Mapenzi Ya Kweli Huku Moyo Wako Ukiwa Huru.

Hutakuwa Na Hukumu Moyoni Mwako, Maana Utakuwa Unamtendea Haki Mpenzi Wako. Lakini Kama Ukiendelea Kumsaliti, Ujue Wazi Kwamba Utakuwa Unajizidishia Maumivu Katika Moyo Wako.


HATUA SABA ZA KUTATUA MIGOGORO INAYOTUKABILI

Two brothers playfully fighting on the couch.   Stock Photo - 9418918

Watu Wamekuwa Wakifanyiana Ukatili, Nchi Zinapigana Vita Kwa Sababu Ambazo Kama Mwanzo Zingepata Wajuzi Wa Kuitatua Isingeleta Madhara Makubwa (L. Ron Hubbard, Mtafiti Wa Sayansi Ya Jamii Kutoka Marekani Anathibitisha Hili Pia).

Zifuatazo Ni Mbinu Za Kufikia Makubaliano Na Mtu Uliyekosana Naye Kwa Sababu Za Kimaisha.

1 : Mgogoro Unapotokea Baina Ya Mtu Na Mtu Au Taifa Na Taifa, Kitu Cha Kwanza Kabisa Kufanyika Ni Kwa Wahusika Kutambua Kuwa Wameingia Katika Mgogoro Na Hivyo Kutazama Kwa Kina Madhara Ya Mgogoro Na Kuamua Kutuliza Jazba Zao Kwa Lengo La Kuangalia Namna Ya Kumaliza Tatizo Kwa Amani.

Hapa Anayesuluhisha Hatakiwi Kutafuta Nani Mwenye Makosa Katika Mgogoro Huo Bali Ni Wakati Wa Kutatua Tatizo, Huku Hilo La Nani Kakosa Likishughulikiwa Baadaye.

2 : Kwenye Mgogoro Kila Mtu Hupenda Kusikilizwa Akiamini Kuwa Ana Sababu Za Msingi Zilizomfanya Akasirike Au Akorofishane Na Mwenzake. Hivyo Ni Wajibu Kwa Watu Wenye Elimu Ya Kutatua Migogoro Kuwapa Nafasi Wahusika Wa Pande Zote Mbili Waseme Yaliyo Mioyoni Mwao, Hata Kama Yatakuwa Yamesheheni Matusi Na Uongo.

Usimkatize Mwenzako Anapotoa Maelezo Yake, Nyamaza Umsikilize Mpaka Mwisho Akimaliza Na Wewe Eleza Yako Kwa Upole, Kama Una Haki Jamii Itakupa.

3 : Usikimbilie Kujihukumu Hasa Pale Wasuluhishi Wanapojaribu Kuchambua Mambo Kwa Kuonesha Dalili Za Kukuzonga Na Pengine Kukuhukumu. “Ok, Kama Mimi Nina Makosa Basi Niacheni Kaeni Ninyi Wasafi,” Usiseme Hivyo Vumilia Lawama Na Pointi Yako Ya Msingi Iwe Ni Kwenye Busara Ya Kulimaza Tatizo Ukiwa Unafahamu Fika Kuwa Kuishi Na Familia, Mke/Mume Kwa Mgogoro Si Jambo Zuri.

4: Unapokuwa Katika Safari Ya Kutaka Suluhu Pendelea Sana Kuunga Mkono Yale Yanayozungumzwa Kwenye Kikao Au Anayozungumza Mwenzako. “Ni Kweli, Ni Kweli Kabisa, Hapo Umesema Sawa, Nakubaliana Na Wewe”. Kauli Za Kukubali Kama Hizi Zina Nguvu Kubwa Ya Kuwafanya Wajumbe Au Mgomvi Mwenzako Anyonywe Hasira Na Kukuona Ni Mtu Mwelewa Unayestahili Kusamehewa Na Kupewa Nafasi Ya Kujisahihisha.

5: Kama Utaona Mgomvi Wako Bado Amejaa Hasira Kiasi Cha Kutotaka Kukusikiliza, Sitisha Mapatano Na Umruhusu Aondoke Au Wewe Uachane Naye Kwa Muda. “Naona Bado Una Hasira Nyingi, Tulia Hasira Zikipungua Tutazungumza”.

Unapompa Mwenzako Muda Wa Zaidi Wa Kutafakari, Kiwango Cha Hasira Hushuka Na Pengine Kufikiria Zaidi Madhara Ya Kugombana. Usilazimishe Kuwasuluhisha Watu Wakati Unaona Wako Kwenye Muwako Wa Hasira, Ukifanya Hivyo Utakuza Tatizo.

6: Mtakapofikia Katika Hatua Ya Maelewano Na Ukabaini Kuwa Wewe Ulikuwa Na Makosa Katika Mgogoro Huo, Uungwana Unakutaka Uwe Mwepesi Kukiri Kosa Na Kutaka Kumaliza Tatizo. “Niliteleza Naomba Unisamehe.” Lakini Hata Kama Umeona Mwenzako Ana Makosa Ila Hataki Kukubaliana Na Wewe, Kuwa Tayari Kubeba Lawama Kwa Lengo La Kumaliza Tatizo, Kwani Gharama Ya Kubeba Kosa Ni Ndogo Ukilinganisha Na Ile Ya Kuendeleza Mgogoro.

7: Jambo Kubwa La Mwisho Linaloweza Kusaidia Kutatua Migogoro Ni Kutumia Nguvu Ya Ufahamu Wako Wa Mambo.

Kama Unaishi Na Mkeo Nyumba Moja Kwa Miaka Mingi, Unatakiwa Kumfahamu Tabia Zake Na Kuzichukulia Hadhari, Vivyo Hivyo Bosi Wako, Wafanyakazi Wenzako, Wanafunzi Wenzio Na Waalimu Wako, Lazima Uwafahamu Tabia Zao. Hii Itakusaidia Kutoingia Katika Migogoro Nao Kwa Vile Utakuwa Unafahamu Mambo Wasiyoyapenda

KANUNI ZA KUISHI NA WANAOKUCHUKIA Maisha Ya Mwanadamu Wakati Mwingine Yamejaa Matukio Ambayo Mwenyewe Hawezi Kuyaepuka. Moja Kati Ya Hayo Ni Mtu Kuchukiwa Na Wenzake Na Kujikuta Katika Wakati Mgumu Iwe Kwenye Familia Na Hata Kazini.
Mara Nyingi Uamuzi Mwepesi Ambao Wanaochukiwa Huwa Wanauchukua Ni Kujibu Mashambulizi Huku Wengine Wakiamua Kujiepusha Eti Kwa Kuhama Maeneo Wanayoishi Au Kujitenga Na Wenye Chuki.

Njia Hizo Zinaweza Kuwa Sahihi Lakini Si Zenye Kuleta Mafanikio Ya Kudumu. Ni Vema Ikafahamika Kwamba Kujibu Mapigo Ya Chuki Hukuza Migogoro Na Jambo Baya Zaidi Ni Kwamba Maadui Huongezeka.

Pengine Msomaji Wangu Ungependa Kujua Kwa Nini Maadui Huongezeka?

Jibu Ni Kwamba Wanaompenda Huyo Unayemlipiza Kisasi Wataingilia Ugomvi Na Kufanya Kila Liwezekanalo Wakumalize.

Nimewahi Kushuhudia Watu Wawili Kazini Wanahitilafiana Kwa Jambo Fulani Lakini Mwisho Kundi La Wafanyakazi Liliingia Kwenye Mgogoro, Chanzo Kikiwa Ni Kile Kile Cha Watu Wawili Wa Mwanzo.

Kwa Nini Hali Hiyo Hutokea? Kwa Sababu Ya Utashi Wa Kibinadamu Na Msukumo Asili Wa Kupenda Kwani Sote Tunajua Hata Wezi Hupendana Na Kuteteana.

Aidha, Tunapotazama Uamuzi Mwingine Wa Kukimbia Maadui Zetu Tunajikuta Tukipata Utata Wa Kimaamuzi Kwa Sababu Hatuwezi Kuwakimbia Wote Kwenye Maisha Yetu, Tukifanya Hivyo Tutakuwa Watu Wa Kuhamahama Kila Siku, Maana Wenye Chuki Ni Wengi Na Wanaanzia Kwenye Familia Zetu Mpaka Kazini.

Jambo La Msingi La Kufanya Pale Tunapobaini Kuwa Kuna Watu Wanaotuchukia Mahali Popote Pale, Ni Kutumia Njia Zifuatazo;

KWANZA: Ni Kufunua Ukweli Kuhusu Kuchukiwa, Yaani Tuwaambie Wanaotuchukia Kuwa Hatufurahishwi Na Chuki, Tuwaombe Msamaha Ikibidi.

PILI: Tujilinde Wenyewe Kwa Kupunguza Uhusiano Na Mwingiliano Wa Kimatendo Na Kauli Hasa Zenye Kupingana.

 TATU: Tutumie Muda Mwingi Sana Kuambatana Na Wanaotupenda Na Kupata Faraja Kwao, Lengo Ni Kuharibu Hisia Mbaya Zitakazokuwepo Kwenye Akili Zetu Juu Ya Wanaotuchukia.

NNE: Tusiachie Nafasi Za Kimaisha Wazitawale Adui Zetu; “Mimi Sitafanya Kazi Na Fulani Acha Afanye Yeye Aone Raha.”
“Nitaacha Kazi Ili Tusigombane Naye Zaidi.” Kamwe Tusitoe Nafasi Za Utawala Badala Yake Tuonyeshe Wengine Kwamba Tunatekeleza Majukumu Yetu Ya Kimaisha Vizuri Ingawa Tunachukiwa Kwenye Familia Au Kazini.

TANO: Tuwashirikishe Ndugu/Rafiki Wenye Busara Katika Kila Kwazo Ili Wasaidie Namna Ya Kufanya. Tusichukue Uamuzi Wenyewe Bila Ushauri Hasa Tunapokuwa Na Hasira. Tujipe Muda Wa Kutafakari Zaidi Kila Jambo La Chuki Tunalofanyiwa Kabla Ya Kuamua Kufanya Chochote.

MUHIMU: Tuepuke Kukuza Mgogoro Kwa Kuwajumuisha Wengine Kwenye Ugomvi. Tusikumbatie Tatizo Na Kulikuza Kwenye Mawazo Yetu. Tuwe Watu Wa Kupuuza Na Kupunguza Msongo Wa Mawazo.
Tusimwambie Kila Mtu Tatizo Letu. Tusimame Kwenye Nguzo Ya Uvumilivu Kwa Muda Mrefu Kabla Ya Kukata Tamaa.

KUKABILIANA NA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME  

Wanaume Wengi Hapa Duniani Huamini Kuwa, Mwanaume Hasa Ni Yule Anayeweza Kufanya Tendo Hilo Kwa Muda Mrefu Na Mara Nyingi Ndio Maana Vijana Wengi Utawasikia Wakijisifu Kuwa, Mpenzi Wake Hakulala Usiku Mzima Kutokana Na Dozi Ya Maana Aliyompa Na Ukimuuliza Mtu Wa Namna Hii Atakwambia Kuwa Alikwenda Mizunguko Sita Usiku Mzima.

Hata Hivyo, Ukweli Ni Kuwa, Watu Wengi Hufikia Hatua Ya Kusema Uongo Ili Waonekana Kuwa Ni Wanaume Hasa Mbele Ya Wenzao Huku Wengine Wakigubikwa Na Nadharia Kuwa Ukubwa Wa Uume Unaashiria Jinsi Gani Walivyo Wanaume Kitu Ambacho Si Kweli.

Ni Mtazamo Huu Ndio Unaowafanya Wanaume Wakitaniwa Au Kuambiwa Kuwa Wako Kama Wanawake Wanaweza Waue Mtu. Tunaamini Kuwa Uanamke Ni Udhaifu Na Uanaume Ni Ushujaa Fulani Hivi.
Wakati Hali Ikiwa Hivyo, Hivi Sasa Wanaume Wengi Wamekuwa Wakihangaika Na Jambo Moja Kubwa, Kutafuta Dawa Za Kuongeza Nguvu Za Kiume Ili Kujiongezea Heshima Faragha!
Ukitaka Kuthibitisha Hili Jaribu Kuangalia Karibu Katika Kila Gazeti Utakalo Soma, Ni Nadra Sana Kukosa Tangazo Dogo La Biashara Lililotolewa Na Mganga Wa Kienyeji Anayejigamba Kuwa Anazo Dawa Za Kuongeza Nguvu Za Kiume, Na Matangazo Hayo Hayaishii Magazetini Tu, Bali Hata Redioni Pia Yapo.

Mbaya Zaidi Dawa Zinazoongelewa Hupewa Majina Mengi Ya `Kusisimua` Kama Kombora, Simba Na Nyati Siushasikia Mziki Wa Nyati Akikasirika Sasa Jenga Picha Nuvu Ya Hiyo Dawa, Hata Hivyo, Dawa Nyingi Ni Uzushi Tu Na Hupewa Majina Hayo Ili Kuwavuta Wateja Na Kuwashawishi Kuzijaribu, Enewei Ndivyo Biashara Zilivyo.

Wingi Huu Wa Matangazo Umeanza Kuonekana Katika Miaka Ya Hivi Karibuni, Na Kadiri Siku Zinavyozidi Ndivyo Idadi Ya Waganga Wanaojigamba Kuwa Na Dawa Hizo Inavyozidi Kushamiri, Kuna Waganga Wenye Dawa Za Kiswahili, Kiarabu Na Za Kichina Ndio Usiseme!
Binafsi Utitili Wa Matangazo Haya Umenifanya Niamini Kuwa, Kuna Tatizo Kubwa La Wanaume Kupungukiwa Nguvu Hizo, Na Ingawa Hakuna Utafiti Wa Kitaalamu Uliofanywa Rasmi, Lakini Inaonyesha Kuwa Tatizo Hilo Kwa Sasa Ni Kubwa Sana Na Si Tanzania Tu, Bali Ni Dunia Nzima.

Kutokana Na Hali Hiyo Ndipo Waganga Wa Kienyeji Pamoja Na Makampuni Mengi Makubwa Duniani Hujaribu Kuelekeza Nguvu Zao Katika Kufanya Utafiti Wa Kutengeneza Dawa Za Kusaidia Watu Wenye Tatizo Hilo, Na Bahati Nzuri Kwa Makampuni Na Waganga Hao Ni Kwamba Inaonekana Kama Biashara Inawaendea Vizuri.
Kwa Mujibu Wa Utafiti Wa Taasisi Moja Ya Biashara Ya Dawa Za Aina Hiyo Nchini Uingereza, Imebainika Kuwa Asilimia 46 Ya Wanaume Nchini Humo Hutumia Dawa Hizo, Hata Hivyo Wengi Wao Huzitumia Bila Ya Kupata Ushauri Wa Daktari Na Maduka Mengi Ya Dawa Yametozwa Faini Kwa Kuwauzia Dawa Hizo Bila Ya Kuwa Na Vyeti Vya Daktari.
Kupungua Kwa Nguvu Miongoni Mwa Wanaume Wengi Kumesababisha Wengi Wao Waishi Katika Maisha Na Hali Ya Usononekaji Na Wengine Wamekumbwa Na Umauti Kutokana Na Hali Hiyo Ya Kuishi Na Sononi Kwa Muda Mrefu.

Kuna Mambo Mengi Yanayosababisha Wanaume Wengi Wajikute Wakipungukiwa Nguvu Za Kiume, Wataalamu Wa Masuala Ya Saikolojia Wanaamini Kuwa Mara Nyingi Suala Hilo, Hasa Kwa Watu Wenye Umri Wa Chini Ya Miaka 45, Husababishwa Na Msongo Wa Akili Kuliko Ufanyaji Kazi Wa Misuli Ya Mwili.

``Watu Wengi Wanaofikiri Kuwa Wamepungukiwa Na Nguvu Hizo Huwa Hawako Hivyo,`` Inasema Sehemu Moja Ya Utafiti Uliofanywa Na Wataalamu Wa Chuo Kikuu Cha Havard, Nchini Marekani Na Kufafanua Kuwa:

``Tatizo La Watu Hao Huwa Ni Kushiriki Tendo Hilo Kwa Wakati Usio Muafaka Kwao, Wanashiriki Wakati Bado Hawajajitayarisha Kiakili Au Wanapokuwa Wamejitayarisha, Basi `Njiani` Hukutana Na Wenzi Ambao Hawaafiki Mwelekeo Wa `Safari` Yao``.

Wataalamu Wa Masuala Ya Vyakula Nao Wanaeleza Kuwa Tatizo Hilo Huwapata Wanaume Wengi Kwa Sababu Ya Utumiaji Wa Vyakula Vyenye Kuongeza Kiwango Kikubwa Cha Mafuta Mwilini Ambao Hawashiriki Katika Mazoezi Ya Viungo Ambayo Huifanya Misuli Ya Damu Mwilini Kutokufanya Kazi Vizuri Na Hivyo Kusababisha Matatizo Mengi Ya Mwili Kushindwa Kufanya Kazi Zake Vizuri.

Kumbukumbu Yangu Inaonesha Kuwa, Mheshimiwa Mbunge Wa Viti Maalumu Kuputua Tiketi Ya Chama Cha Mapinduzi, Janet Bina Kahama, 10 Aprili 2007 Katika Kikao Cha Saba Cha Bunge Aliulizwa Swali Ambalo Lilikuwa Namba 8 Lenye Kipengele A, B, Na C Ambapo Kwenye Kipengele B Aliuliza: Je, Serikali Inafahamu Ni Sababu Gani Zinasababisha Kupungua Kwa Nguvu Za Kiume Kunakotangazwa Sana Na Waganga Wa Jadi?

Waziri Wa Afya Na Ustawi Wa Jamii, Prof. David Homeli Mwakyusa Alijibu Kuwa, Upungufu Wa Nguvu Za Kiume Unasababishwa Na Mambo Mengi, Baadhi Yao Ni Lishe Duni Hasa Mboga Za Majani, Kutokula Aina Mbalimbali Za Jamii Ya Karanga (Nuts), Matumizi Yasiyofaa Ya Ulevi Kama Pombe, Sigara Na Dawa Za Kulevya, Dawa Zinazotibu Baadhi Ya Magonjwa Kama Kisukari, Shinikizo La Damu, Magonjwa Ya Akili Na Vilevile Kutopumzika Kunakosababishwa Na Shughuli Nyingi Za Kijamii Hivyo Kusababisha Uchovu.

Lakini Ni Kweli Dawa Hizi Za Asili Zinauwezo Wa Kutatua Tatizo La Upungufu Wa Nguvu Za Kiume? Pro. Mwakyusa Anathibitisha Kwa Kusema Kuwa, Dawa Nyingi Za Tiba Asili Ni Virutubisho Ambavyo Muhitaji Angeweza Kuvipata Endapo Angekula Vyakula Vyenye Virutubisho Hivyo.

Pamoja Na Kuwa Dawa Hizo Hazijafanyiwa Utafiti Wa Sayansi Ya Leo Na Kutokana Na Unyeti Wa Usiri Wa Watumiaji Wa Dawa Hizo Zingekuwa Na Madhara Zisingetumiwa Na Wananchi Hata Huko Zinakotoka Yaani Maeneo Yake Ya Asili.

Na Kusisitiza Kuwa, Wizara Ya Afya Na Ustawi Wa Jamii Haijapokea Taarifa Ya Tukio Kutoka Kwa Walalamikaji Wanaotumia Dawa Hizo Za Kuongeza Nguvu Za Kiume.

Hata Hivyo, Hali Ni Tofauti Kidogo Katika Nchi Zilizoendelea Kama Marekani Na Baadhi Ya Nchi Za Ulaya, Matumizi Ya Dawa Hizi Hutolewa Kwa Watu Baada Ya Kuandikiwa Cheti Na Daktari, Na Watu Wenye Matatizo Ya Msukumo Wa Ndamu (Bp), Mara Nyingi Wamekuwa Wakishauriwa Kutotumia Dawa Hizo Kwa Sababu Ni Hatari Kwa Maisha Yao.

Hii Ni Kwa Sababu Dawa Nyingi, Kama Viagra, Ciallis, Levitra, Yohimbine Na Nyingine Mbali Ya Kuwa Na Nafasi Ya Kusababisha Magonjwa Ya Moyo, Kwa Watu Wasiokuwa Nayo, Pia Yana Madhara Mengine Kama Vile Kusababisha Upofu Na Kuleta Hali Ya Mwili Kuwa Na Kitetemeshi.

Madhara Mengine Ya Dawa Hizo Ni Pamoja Na Kumsababishia Mtumiaji Hali Ya Kuumwa Na Kichwa Mara Kwa Mara, Macho Kuwa Mekundu, Kuziba Kwa Hewa Puani Na Maumivu Ya Tumbo Pamoja Na Kuharisha.

Haya Ni Aina Ya Madhara Yanayotokana Na Dawa Za Kizungu, Ambazo Kabla Ya Kuingia Madukani Kufanyiwa Utafiti Wa Kina Kuangalia Madhara Yake Kwa Watumiaji, Na Ingawa Hayo Yote Yanafanyika Lakini Bado Athari Zake Kwa Watumiaji Zinaonekana.

Mwandishi Na Muandaaji Mkongwe Wa Filamu Nchini Ambaye Kwa Sasa Anaishi Marekani, Chemi Che-Mponda Alishawahi Kuandika Makala Isemayo ‘Kukosa Nguvu Za Kiume Si Mwisho Wa Dunia!’ Na Katika Makala Hiyo Kulikuwa Na Hadithi Hii Isome Ili Ujue Kinachoweza Kukutokea Kwa Kujifanya Mjuaji Na Kuagiza Dawa Za Kuoneza Nguvu Kwenye Mtandao.

Chemi Alianza Hivi: “Jamani, Jamani, Jamani, Kuna Jirani Yangu Kafa Hivi Majuzi. Alikuwa Ni Baba Wa Makamu, Mmarekani Mweusi. Alikuwa Mcheshi Na Ilikuwa Kila Tukionana Lazima Tusalimiane.
“Mara Ananinunulia Kahawa Halafu Tunakaa Namsimulia Kuhusu Afrika. Yule Baba, Alionekana Mzima Na Mwenye Afya Fiti Kabisa. Nilibakia Kushangaa Kusikia Kafa Na Si Kwa Ajali. Mke Wake Alifariki Mwaka Juzi, Lakini Miezi Ya Karibuni Alikuwa Anaonekana Mwenye Furaha Kwa Vile Alipata Mpenzi, Dada Mwenye Miaka 25 Hivi.

”Story Niliyosikia Ni Hivi: Kumbe Jamaa Alikuwa Na Matatizo Ya Moyo. Alifia Kitandani Akiwa Kwenye Shughuli Ya Kufanya Tendo La Ndoa Na Mpenzi Wake. Tena Wanasema Alifariki Mara Alipofikia Kilele Cha Tendo.“Navyosikia Ilikuwa Ni ‘Massive Heart Attack’. Kama Ni Massive Bila Shaka Na Utamu Wa Shughuli Hakujua Kuwa Yuko Hatarini. Mpenzi Wake Alipiga Sana Kelele, Majirani Walipigiga Simu 911 (Polisi) Kwa Vile Walidhania Wameingiliwa Na Majambazi.

“Kumbe Jamaa Alikuwa Mtumizi Wa Viagra, Yaani Vile Vidonge Vya Kuongeza Uume, Na Kumpa Mwanaume Uweza Wa Kufanya Tendo La Ndoa. Ndugu Zake Wanalamika Kweli, Maana Hakuzipata Kwa Prescription (Maelezo) Ya Daktari, Alizaiagiza Kwenye Mtandao (Internet).
Hiyo Ni Baadhi Ya Mifano Hai Inayoonesha Wazi Madhara Unayoweza Kupata Kwa Kuamua Kutumia Tu Dawa Bila Maelekezo Kutoka Kwa Daktari!

Binafsi Nina Hofu Juu Ya Dawa ‘Za Kienyeji’ Zinazotengenezwa Na Waganga Na Kuuzwa Kama Karanga Kila Kona Ya Miji Mbalimbali Ya Tanzania Bila Ya Kufanyiwa Utafiti Wa Kina, Ni Wazi Kama Kanuni Za Kiafya Zinavyosema, Kuwa Kila Dawa Ina Madhara Yake, Lakini Je, Ni Nani Anapima Madhara Mabaya Yatokanayo Na Dawa Hizi Za Kienyeji Zinazouzwa Kama Njugu?

Ukiacha Madhara Yatokanayo Na Dawa Hizo, Pia Wanaume Wengi Hukumbwa Na Tatizo Hili La Kupungukiwa Nguvu Kwa Sababu Ya Uvutaji Wa Sigara Kwa Wingi, Utafiti Mbalimbali Wa Kitabibu Duniani Unaonyesha Kuwa Matumizi Ya Bidhaa Zitokanazo Na Tumbaku Huwasababishia Wanaume Upungufu Wa Nguvu Hizo.

Ni Kweli Ulio Wazi Kwamba Tatizo La Wanaume Wengi Kupungukiwa Nguvu Za Kiume Nchini Kwetu Na Duniani Kote Linazidi Kushika Kasi Na Tiba Mbadara Zinahitajika Ili Kurudisha Heshima Na Furaha Miongoni Mwa Wanaume Wengi Duniani, Lakini Utumiaji Wa Dawa Za Kuongeza Nguvu Haupaswi Kufanyika Kiholela Kwa Kuzingatia Kuwa Matatizo Yake Kiafya Ni Makubwa Kuliko Faraja Ya Muda Mfupi Anayopata Mtumiaji!

Siku Moja Nilikuwa Nimekaa Kwenye Kijiwe Cha Kahawa Kariakoo Jijini Dar Es Salaam Nikachokonoa Wazee Kwa Kuchomekea Mada Hii, Mambo Mengi Walinieleza Lakini Kubwa Zaidi Ni Kuwa, Vijana Wa Siku Hizi Wanakubwa Zaidi Na Tatizo Hili Kutokana Na Kufakamia Vyakula Visivyo Vya Asili Na Kusahau Kuwa, Miogo, Asali, Karanga Na Pweza Huweza Kukusaidia Ukawa Na Nguvu Kama Nyati. Vyakula Vingi Vinavyoingizwa Nchini Vikiwa Vimesindikwa Ambavyo Vijana Wengi Hukimbilia Na Kujiona Kuwa, Babu Kubwa Wakivila Hivyo Na Kumcheka Mzalendo Anayepata Muogo Wa Kuchoma Na Chachandu Huku Akishushia Na Juisi Ya Mua Pale Kariakoo Bila Kujua Kuwa Sehemu Kubwa Ya Aina Nyingi Ya Vyakula Wanavyokula Ni Sumu Yenye Ladha Nzuri Inayonenepesha! Madhara Yake Ni Mengi Na Miongoni Mwake Ni Kuwasababishia Watumiaji Kukosa Nguvu Za Kurudia Tendo.

SABABU ZA KUPUNGUA NGUVU ZA KIUME:

 1. Hata Hivyo, Kuna Wakati Pia Upendo Unapopungua Na Mvuto Unapungua Baina Ya Wanandoa, Mwanaume Anaweza Kujikuta Kila Akiwa Faragha Anashindwa Kuendesha Gari Kwa Muda Mrefu Na Anaweza Kudhani Kuwa Ana Matatizo Kumbe Hali Hiyo Inamkumbwa Kutokana Na Kutokuvutiwa Na Mwenzi Wake.

Tatizo Kama Hili Linaweza Kutatuliwa Kwa Kumueleza Wazi Mkeo Ama Mpenzi Wako Jinsi Gani Anaweza Kujipanga Na Kuonekana Na Mvuto Wa Hatari Utakaokufanya Uchanganyikiwe Kila Umuonapo Na Hata Mkiingia Kwenye Mambo Fulani Basi Kwa Hakika Utahamasika Na Kutoa Dozi Ya Maana.

2.Uchovu Wa Kazi Za Ajira Mkufunzi Wangu Wa Saikolojia Katika Chuo Kikuu Cha Tumaini Iringa Ambaye Ameshatangulia Mbele Za Haki, Pro. Samuel Mshana (Mungu Amlaze Mahali Pema Peponi) Aliwahi Niambia Kuwa Wanawake Wanataka Security Kutoka Kwa Mwanaume Nami Nikamtania Pro. Sasa Mbona Mimi Na Mwili Mdogo Nitampa Ulinzi Gani Mwanamke Akacheka Kisha Akaniambia Ulinzi Naouzungumzia Ni Wa Jumla Ikiwa Ni Pamoja Na Kuhakikisha Mambo Yanakwenda Sana Ndani Ya Nyumba Yani Watoto Wanakwenda Shule Na Mambo Ya Mlo Wa Uhakika.

Hivyo Ni Wazi Kuwa Wanaume Huhangaika Kwa Kiasi Kikubwa Kuhakikisha Wanamudu Majukumu Yao Ya Kila Siku Na Huko Makazini Kuna Mauzauza Mengi Na Usiombe Ufanye Kazi Kwenye Kampuni Binafsi Kila Kukicha Wewe Upo Roho Juu Sasa Katika Hali Kama Hiyo Ukikutana Na Mwenzi Wako Kunako Majambozi Utahisi Una Upungufu Wa Nguvu Za Kiume Kwani Mara Tu Baada Ya Kumaliza Mshindo Wa Kwanza Hutoweza Kurudia Tena! Hali Ni Hivyo Hivyo Kwa Watu Wanaofanya Kazi Nzito Zinazosababisha Wajikute Wanarudi Majumbani Wakiwa Wamechoka.

Hivyo Basi, Endapo Nawe Ni Miongoni Mwa Watu Wanaokumbana Na Tatizo La Kushindwa Kurudia Majambozi Kwa Sababu Ya Uchovu Na Msongo Wa Mawazo Kutoka Kazini Hakikisha Unapanga Muda Muafaka Na Mwenzi Wako Kupeana Raha.

Mfano Kama Jumamosi Unafanya Kazi Nusu Siku Ukitoka Usiende Kulewa Kama Ni Mtu Wa Kinywaji Bali Nenda Kapumzike Kisha Kesho Yake Waweza Kumtoa Out Mama Na Kwenda Mazingira Tofauti Kupeana Kitu Roho Inapenda Hakika Utajishangaa Jinsi Utakavyomudu Majambozi.

3. Kuchacha Nakumbuka Vema Miaka Ya 1990 Enzi Hizo Redio Tanzania Pekee Ndio Ilikuwa Ikitupa Burudani Na Moja Kati Ya Nyimbo Ambazo Ilikuwa Ikinikuna Ni ‘Kuchacha Usiombee’ Iliyoimbwa Na Juwata Jazz Na Hichi Ni Kibwagizo Chake ‘Maradhi Yote Ugua Lakini Kuchacha Usiombe…’ Ebwana Usije Ukawa Katika Hali Mbaya Kifedha Na Kila Jambo Unalolipanga Linakwenda Ndivyo Sivyo Hali Inayokusababishia Uchache Kisha Mwenzi Wako Akakuomba Unyumba Hapa Kuna Mawili Ama Kuchelewa Sana Kufika Safari Yenu Ama Kumaliza Halaka Kisha Jamaa Analala Chapchap Na Hataki Tena Kuonesha Ushirikioano Hata Mamaa Akimbembeleza Vipi!

Hivyo Basi, Si Vema Kukutana Kimwili Na Mwenza Wako Kipindi Ukiwa Umechacha Kwani Wanaume Wengi Pindi Wanapokuwa Na Msongo Wa Mawazo Hukimbilia Kuomba Unyumba Kwa Wenzi Wao Wakiamini Kuwa, Wao Ndio Watawasaidia Kuwapunguzia Mawazo Badala Ya Kutafuta Njia Mbadara Ya Kumaliza Tatizo.

4. Kuishiwa Hamu Ya Nyama Na Mapishi Yale Yale Kila Siku Uzoefu Wangu Unanionesha Kuwa Wanaume Wengi Hujikuta Wakikosa Hamu Ya Kurudia Tendo La Ndoa Mara Bada Ya Kumnaliza Mzunguko Wa Kwanza Kutokana Na Wake Zao Kutowaonesha Ubunifu Yaani Kila Siku Ni Kifo Cha Mende Tu Hakuna Jipya Linaloongezwa Hata Nakshi Za Miguno Ni Ile Ile Hali Inayosababisha Wanaume Wakose Hamy Ya Kuendelea Mara Baada Ya Kumaliza Mzunguko Wa Kwanza.

Wanaume Wengi Hujikuta Wanalazimika Kutafuta Kimada Ili Kupata Radha Mpya Na Huko Mambo Huwa Mulua Kwani Hufanikiwa Kwenda Raundi Hadi Tatu Na Bado Akawa Na Hamu Kwa Vile Tu Amekutana Na Vitu Adimu Hivyo Basi, Mwanaume Anapaswa Kumueleza Wazi Mkewe Kuwa Anahitaji Wakutane Faragha Ambapo Anataka Vutu Hadimu Vya Kabatini Na Si Kumsaliti Mwenza Wako Kwani Uwezo Wa Kumfanya Awe Bora Kunako Majambozi Unao Wewe Mnwenyewe Mwanamme.

Mfano Siku Akikwambia Anakwenda Kwenye Kitchen Party Mruhusu Kisha Akiwa Huko Mtumie Meseji Kuwa, “Mpenzi Najiandaa Kumalizia Sehemu Ya Pili Ya Soma Ulilojifunza Yaani La Vitendo, Hakika Leo Nitafaidi” Asikdanganye Mtu Hapo Hata Kama Bi. Harusi Mtarajiwa Hakufundishwa Mambo Fulani Ya Kumpagawisha Mumewe Atahakikisha Hakuangushi Atakuja Na Mambo Mapya Na Hapo Ndipo Mwanaume Hujikuta Akiganda Kifuani.

Nimalize Kwa Kusema Kuwa, Hakuna Haja Ya Kukurupuka Na Kukimbilia Kununua Dawa Za Kuongeza Nguvu Ya Kiume Bila Kutafakari Kwa Kina Chanzo Cha Tatizo Lako Kwani Yawezekana Tatizo Ulilonalo Linaweza Kutatulika Kwa Njia Nyingine Ambazo Hazitakufanya Uwe Hatarini.

UMEMFUMANIA, SASA UNASEMAJE NA UNAFANYAJE?
HEBU FIKIRIA KUWA UMEDHIBITISHA KWAMBA MWENZAKO SIO MWAMINIFU, YAANI AMETOKA AU ANATOKA NJE YA NDOA, UTAFANYAJE? JE, UTAONDOKA, UTALIPA KISASI NA WEWE, AU UTACHUKUA HATUA GANI?...

 Kuna Mambo Ambayo Ukiona Kwamba Yamejitokeza, Baada Ya Fumanizi, Unapaswa Kujua Nafasi Yako Kwenye Uhusiano Wako. Kutokea Hapo Ndipo Unapoweza Kuamua Kama Uondoke Au Hapana.

Kwanza, Hebu Jikague, Je, Umevunjika Moyo Kupita Kiasi? Unadhani Itakuwa Bora Kuvumilia? Unadhani Kumvaa Na Kumwambia Umechoka Na Unataka Kuondoka Itakuwa Ni Kujiongezea Mfadhaiko Zaidi?

Pili, Unadhani Utaendelea Kubaki Katika Ndoa Kwa Sababu Za Kidini? Unataka Kufanya Kitu Kilicho Sahihi Daima? Uko Tayari Kuendelea Kudhalilika Na Kuwa Hatarini Kwa Sababu Ya Imani Yako Ya Kukukataza Kuvunja Ndoa? Je Ni Kwa Imani Yako Au Wasiwasi Wako Umelazimika Kubaki? Nijuavyo Mimi, Kosa La Kutoka Nje Halitetewi Na Dini Yoyote Linapokuja Swala La Kuvunja Ndoa.

Tatu, Unadhani Unalazimika Kubaki Kwa Usalama Wa Watoto? Unadhani Ni Wewe Pekee Unawajali Watoto Na Mwenzio Hawajali? Inawezekana Na Mzazi Mwenzio Pia Ni Mpenda Watoto? Unadhani Kuachana Kutawaletea Watoto Matatizo Zaidi? Una Wasiwasi Na Maisha Ya Watoto Kama Utaamua Kuondoka? Kumbuka Kuishi Kwenye Vurugu Za Ndoa Huwavuruga Watoto Kuliko Watoto Kuishi Na Baba Au Mama Wa Kambo Mwenye Upendo.

Nne, Unadhani Hakuna Uwezekano Kabisa Katika Ndoa Hii? Umekwama? Umenata Kama Ulimbona Huwezi Kuondoka? Unaweza Kufikia Muafaka Kwamba Umejitahidi Kwa Uwezo Wako Wote Kumrekebisha Mwenzio Lakini Wapi. Hivyo Umeamua Kuishi Hivyo Hivyo?

Tano, Unadhani Huwezi Kuondoka? Kuna Kitu Unachodhani Kinakuletea Ugumu Wa Kuanza Safari? Kuanza Maisha Mapya? Huna Uwezo Wa Kujiamulia? Kumbuka Kwamba, Huenda Ni Mazoea Tu Yanayokuzuia Au Utegemezi Wa Kipato. Lakini, Kila Binadamu Ameletwa Duniani Ili Asimame Kama Yeye, Na Siyo Kama Kipande Cha Mwenzake.

Sita, Unataka Kumlinda? Kuna Kitu Kibaya Unachodhani Kinaweza Kutokea Kama Utaamua Kuondoka? Ataweza Kuishi Peke Yake? Kama Utaondoka Unadhani Itakuwa Ni Njia Ya Kumpeleka Shimoni Zaidi? Umeamua Kubaki Ukijua Kwamba Baada Ya Muda Tatizo Lenu Linaweza Kutatuliwa? Inawezekana Likatatuliwa, Lakini Inawezekana Wewe Ni Mtu Wa Kuumia Kwa Sababu Ya Wengine Bila Sababu.

Saba, Unaendelea Kuishi Naye Kwa Sababu Kuna Hatari Kumwambia Unataka Kuondoka? Unadhani Atalipuka Kwa Hasira Utakapomwambia Unataka Kuondoka? Una Wasiwasi Kwamba Una Haki Ya Kuamua Kuhusu Maisha Yako Na Kuna Sheria Zinazokulinda.

Je, Hujafikiria Namna Ya Kuanza Maisha Mapya? Hii Ni Tofauti Na Hofu Ya Kuanza Maisha Mapya. Labda Maisha Yako, Yake Na Ya Watoto Yameambatanishwa Kupita Kiasi, Hivyo Inakuwia Vigumu Kujinasua? Pia Kuambatanishwa Huku Labda Ndiko Kunakokufanya Hata Usiwe Na Chembe Ya Wazo La Kutaka Kuondoka? Umewahi Kufikiria Kuhusu Utashi Wako, Ujuzi Wako, Ndoto Zako, Matumaini Yako Na Mustakabali Wa Maisha Yako Bila Yeye, Au Bila Watoto?

Chukua Muda Wa Kutosha Kufikiri Kwa Makini Na Uyajibu Maswali Hayo Yote Ukishayajibu Utakuta Unatoa Uamuzi Sahihi Utakaokupeleka Kwenye Maisha Uyatakayo. Kumbuka, Kila Binadamu Hukosea Na Kusamehe Kwa Aliyekosewa. Lakini Kusamehe Hakuna Maana Ya Kuendelea Kuumia Au Kuumizwa Na uliyemsamehe........unaweza ukasamehe huku ukiendelea na maisha yako na kutimiza ndoto zako na malengo yako maishani.


Tatizo La Mwanaume Kuwahi Kufika Kileleni Mapema!  1. Malalamiko Yanayotolewa Na Baadhi Yao Yanaonesha Kwamba, Muda Wa Kumaliza Tendo Huwa Kati Ya Nusu Dakika Na Dakika Tatu Kwa Tendo La Kwanza, Huku Wengine Wakimaliza Hamu Katika Hatua Za Awali Tu Za Hamasa Ya Kimahaba.

2. Hata Hivyo, Kumetolewa Maelezo Na Nafuu Ya Ongezeko La Muda Katika Tendo La Pili Na Kuendelea, Ingawa Bado Suala La Kutangulia Kufika Kileleni Kabla Ya Wanawake Limekuwa Likiwahuzunisha Wanaume Wengi.

3. Ni Ukweli Usiopingika Kuwa, Mwanaume Anapowahi Kufika Kileleni Kabla Ya Mwenzake Humsababishia Kero Mwanamke Anayeshiriki Naye Tendo, Kwani Humwacha Njia Panda Pasipokuwa Na Hitimisho La Raha Ya Kujamiiana.

4. Hali Hii Inatokana Na Maumbile Ya Uume Wa Mwanaume Ambao Husinyaa Mara Baada Ya Kuhitimisha Mbio Zake, Lakini Kwa Mwanamke Kuwahi Si Tatizo, Kwani Hakumfanyi Ashindwe Kumsindikiza Mwenzake Hadi Kileleni.

5. Utofauti Huu Ndiyo Unaowafanya Wanaume Wahuzunike Zaidi Wanapokabiliwa Na Janga Hilo Kiasi Cha Kufikia Hatua Ya Kwenda Kwa Waganga/Matabibu Ili Iwasaidie Kuepuka Balaa Ya Kutoka Uwanjani Na Aibu.

6. Ingawa Kumekuwa Na Mafanikio Katika Tiba Za Kisayansi, Lakini Bado Wanaume Wameshindwa Kupata Ukombozi Wa Kudumu Wa Tatizo Hili. Wengi Wamejikuta Wakijiongezea Mzigo Wa Fikra Kwa Kuzitumaini Zaidi Dawa Au Kuzitumia Na Kupata Matokeo Mabaya Zaidi Ya Kuishiwa Nguvu Kabisa.

7. Kwa Kufahamu Mikinzamo Iliyopo Kati Ya Akili Na Tiba Ya Nguvu Za Kiume Na Madhara Yachipukiayo Imebainika Kuwa, Mtu Anaweza Kujitibu Tatizo Hilo Kwa Kutumia Kanuni Za Kisaikolojia Na Mafanikio Yasiyo Na Madhara Yakapatikana.
Wataalamu Wa Kisaikolojia Wanatambua Kuwa Kanuni Ya Ufanyaji Mapenzi Iko Zaidi Kwenye Ubongo Kuliko Mwilini.

8. Kinachotokea Hadi Mtu Akapata Msisimko Wa Kufanya Mapenzi Si Mwitikio Wa Mwili, Bali Ni Utambuzi Wa Akili Juu Ya Kiwango Cha Mapenzi Kilichopokelewa Kwenye Ubongo Unaojihusisha Na Hisia.


FAHAMU VYAKULA VINAVYOONGEZA NGUVU.....


Kuna Aina 2 Ya Vyakula Ambavyo Vimefanyiwa Utafiti Na Kubaini Kuwa Ni Moja Ya Vyakula Vinavyosaidia Kuongeza Nguvu Za Kiume Na Havina Madhara Katika Engezeko La Nguvu Za Kiume, Katika Vyakula Hivyo Vyenye Uwezo Wa Kuongeza Nguvu Za Kiume Kiasili Ni:

1. TANGAWIZITangawizi Ni Moja Ya Chakula Kinachoweza Kurejesha Nguvu Za Kiume, Unaweza Kuichemsha Tangawizi Na Ukatumia Kwa Kuinywa Kama Chai Asubuhi, Mchana Na Jioni Pia Tangawizi Unaweza Ukaitumia Katika Mchanganyiko Wa Kiasili Kwa Kutumia Asali,Kitunguu Saumu Na Tangawizi Yenyewe.
 


JINSI YA KUTUMIA MCHANGANYIKO HUU:
Chukua Tangawizi Na Kitunguu Saumu Vitwange Kisha Vichanganye Na Asali Pamoja Na Unga Wa Habat Soda Na Uwe Unakunywa Mchanganyiko Huu Kwa Kutumia Kijiko Cha Chai Kimoja Kutwa Mara 3 Kwa Muda Wa Wiki Moja Na Utaona Mabadiliko.

2. TIKITI MAJI:
-Chakula Kingine Kinachosaidia Katika Upande Wa Kuongeza Nguvu Za Kiume Ni Tunda La Tikiti Maji, Unaweza Ukachukua Tikiti Lako Ukalikata Na Kutengeneza Juice Ya Tikiti Kisha Unakunywa Ila Sio Lazima Utengeneze Juice Hata Lenyewe Tu Unaweza Ukalila. Ila Jitahidi Kutumia Tunda Hili Hata Kila Siku Kwani Linasaidia Sana Kwa Wenye Matatizo Ya Nguvu Za Kiume.


Si lazima utumie chemicals tumezungukwa na suluhisho ya matatizo mbalimbali kwa kutumia matunda na mbogamboga ............Jaribu ujionee.....

UKIFUATA MAMBO HAYA KUMI UTAKUA UMERAMBA SUMU YA PENZI NA HAUTOUMIZA/HUTOUMIZWA KAMWE…

Fighting lovers

1. Wivu Wa Kupindukia
Ni Jambo Jema Kwa Mwanamume Kumtakia Heri Mpenzi Wake Na Kufanya Kila Awezalo Kuhakikisha Kuwa Hapati Madhara, Lakini Iwapo Utakuwa Mtu Wa Wasiwasi Na Mashaka Pale Unapomwona Mpenzi Wako Akizungumza Na Mwanamume Mwingine, Au Anapotoka Na Marafiki Zake Wa Kike, Au Anapovaa Nguo Inayomfanya Atamanishe, Basi Fahamu Kuwa Tayari Umekunywa Sumu Ya Mapenzi.

Katika Uhusiano Wa Kimapenzi, Kuaminiana Ni Jambo Muhimu Sana. Kama Kweli Unataka Mpenzi Wako Akupende Kwa Dhati, Mwoneshe Kuwa Unamwamini Na Unaheshimu Maamuzi Yake, Ikiwa Ni Pamoja Na Maamuzi Ya Kutoka Na Marafiki Zake Wa Kike Na Kuwa Na Marafiki Wa Kawaida Wa Kiume. Ondoa Hofu Na Acha Kabisa Kumpeleleza, Maana Wapo Wanaume Ambao Hutumia Muda Wao Mwingi Kuwapeleleza Wapenzi Wao Ikiwa Ni Pamoja Na Kuwategeshea Kamera Na Rekoda Za Simu.

2. Kutomwachia Nafasi Mpenzi
Kama Huishi Na Mpenzi Wako Ni Jambo La Kawaida Kuwa Na Hamu Ya Kumwona Mara Kwa Mara, Lakini Kumbuka Kuwa Mpenzi Wako Naye Ana Maisha Yake Na Anahitaji Nafasi Ya Kuwa Peke Yake Kwa Ajili Ya Mambo Yake Binafsi.

Hisia Za Kutaka Kuwa Na Mpenzi Wako Muda Wote Zinaweza Kudhaniwa Kuwa Ni Za Mapenzi Ya Dhati, Lakini Kwa Hakika Hiyo Si Ishara Njema Ya Mapenzi Ya Kudumu. Hebu Jiulize Kama Unaweza Kuendeleza Hali Hiyo Maisha Yako Yote. Ni Wazi Kuwa Utachoka. Kwa Hiyo, Mpe Mpenzi Wako Fursa Ya Kupumua. Namna Hii Mpenzi Wako Atajenga Hamu Ya Kutaka Kukutana Nawe Lakini Ukiwa Naye Muda Wote Hamu Hiyo Itaisha.

3. Kumwamulia Mpenzi Mambo Yake
Unaweza Kujikuta Ukisukumwa Kumwambia Mpenzi Wako Awe Anavaa Nini Wakati Gani, Akutane Na Nani Na Kwa Wakati Gani Au Ale Nini. Ukiona Hivyo, Fahamu Kuwa Hayo Si Mapenzi, Bali Umepitiliza Na Pengine Mwisho Wa Uhusiano Wenu Unanukia.

Hata Ukiachilia Mbali Suala Zima La Usawa Wa Jinsia, Hakuna Mwanamke Ambaye Angependa Apangiwe Kila Kitu Kuhusiana Na Maisha Yake. Kama Ilivyodokezwa Hapo Juu, Kila Mtu Ana Maisha Yake Na Kilichowaunganisha Ni Mapenzi Tu. Kama Utataka Kumpangia Kila Kitu Ni Wazi Kuwa Utaishia Kuishi Peke Yako.

4. Kumuuliza Mpenzi Maswali
Iwapo Utajikuta Ukimuuliza Mpenzi Wako Maswali Mengi Yanayoonesha Wasiwasi Wako Kuhusiana Na Mwenendo Wake, Fahamu Kuwa Kuna Tatizo Na Tatizo Hilo Lisipopatiwa Ufumbuzi Utakuwa Mwanzo Wa Mwisho Wa Uhusiano Wenu.

Mwanamke Angependa Umuulize Maswali Ya Kawaida Kuhusiana Na Jinsi Siku Yake Ilivyokuwa Na Kama Marafiki Zake Hawajambo Au La, Lakini Kila Jambo Lina Mpaka Wake. Mwanamke Hatarajii Kuwa Kila Mnapokutana Atakuwa Kama Ameingia Kwenye Chumba Cha Mtihani Au Usaili Wa Kazi.

5. Kutoamini Anachokweleza Mpenzi
Wakati Mwingine Watu Hushindwa Kuwaamini Wenzao, Lakini Kwa Sababu Ambazo Ni Za Msingi, Lakini Kuna Wakati Ambapo Mtu Hushindwa Kumwamini Mwenzake Bila Sababu Yoyote Ya Msingi, Au Kwa Sababu Zisizo Sahihi, Kisingizio Kikiwa Ni Mapenzi.

Kuna Tatizo La Kisaikolojia La Kujishuku Au Kuwashuku Wenzako. Hili Ni Jambo Ambalo Linaweza Kukuharibia Mustakabali Wako Katika Mapenzi, Maana Husababisha Kujengeka Kwa Mazingira Ya Kutokuaminiana. Ili Uweze Kwenda Sanjari Na Mpenzi Wako, Amini Kila Anachokweleza Hadi Pale Utakapokuwa Na Sababu Za Msingi Za Kutokumwamini. Na Hata Unapokuwa Umelithibitisha Jambo, Endelea Kuwa Katika Uhalisia Wako.
6. Kuacha Hobi, Marafiki
Mahusiano Ya Kimapenzi Mara Nyingi Huhusisha Kila Mmoja Kuacha Baadhi Ya Mambo Yake Kwa Ajili Ya Mwenzake. Hata Hivyo, Lengo Ni Kuweka Tu Uwiano Wa Mahitaji, Si Kuacha Kila Kitu Ulichokuwa Nacho Kwa Ajili Ya Mwenzako, Ama Kwa Shinikizo, Au Kwa Kulewa Penzi.

Iwapo Utabaini Kuwa Marafiki Zako Sasa Wamekuwa Ni Marafiki Zako Wa Zamani Na Hobi Zako Zimebaki Tu Katika Kumbukumbu Japo Kwa Hakika Bado Unahisi Mapenzi Katika Hobi Hizo, Basi Tambua Kuwa Huyo Mrembo Wako Amekunywesha Sumu Ya Penzi Na Sasa Huwezi Hata Kuitumia Vema Mantiki Yako.

Mbaya Zaidi, Iwapo Utabaini Kuwa Marafiki Zako Wapya Ni Marafiki Wa Siku Zote Wa Mpenzi Wako Na Hobi Zako Ni Zile Za Mpenzi Wako, Basi Tambua Kuwa Huna Tena Nafsi Yako, Bali Umejisalimisha Mzima Mzima Kwa Mpenzi Wako. Lakini Msemo Mmoja Wa Hekima Unatwambia Usiweke Mayai Yako Yote Kwenye Kikapu Kimoja. Yamkini Unaelewa.

7. Kukubali Kupelekeshwa
Pengine Unakumbuka Kuwa Kuna Nyakati Ambapo Ulikuwa Na Uwezo Wa Kujikita Katika Jambo Moja Na Kulifanya Kwa Umakini, Huku Ukiwa Pia Mwerevu, Mjanja Na Unayejisimamia, Lakini Leo Unayeyuka Kirahisi Tu Kama Barafu Iliyowekwa Juani! Hii Ni Hatari Kwa Mustakabali Wa Maisha Yako.

Mbaya Zaidi Ni Pale Utakapoiacha Kazi Yako Inayokulipa Vizuri Na Kufanya Kazi Nyingine Kwa Ajili Ya Kumfurahisha Mpenzi Wako. Ukifika Hali Hii Ujue Wewe Mwenyewe Kuwa Hapo Hakuna Mwanamume.

8. Utayari Wa Kufa Kwa Ajili Yake
Umewahi Kujisikia Kuwa Na Utayari Wa Kufa Kwa Ajili Ya Mpenzi Wako? Kama Jibu Ni “Ndiyo”, Basi Fahamu Kwa Hakika Kuwa Hayo Uliyo Nayo Si Mapenzi Bali Ni Upumbavu. Pengine Huku Ndiko Kunywesha Sumu Ya Mapenzi. Kwa Hakika, Hakuna Mwanamke Ambaye Anastahili Kumfanya Mwanamume Yeyote Kufa Kwa Ajili Yake.

Yamkini Wanaume Wanaolengwa Katika Makala Haya Si Wavulana Wanaosoma Sekondari, Waliobalehe Majuzi, Ambao Wakipenda Au Kupendwa Hujiona Kama Wako Katika Sayari Yao. Mwanamume Aliyepevuka Hujiamini Na Hayaweki Maisha Yake Yote Mikononi Mwa Mwanamke, Hata Kama Mwanamke Huyo Angekuwa Ndiye Mrembo Wa Dunia.

Iwapo, Ama Kwa Ujinga Au Kwa Kufahamu Umewahi Kumwambia Mpenzi Wako: “Ukiniacha Nitajiua,” Na Ukawa Unaamini Hivyo Kabisa, Basi Yamkini Unahitaji Kutafuta Msaada Wa Ushauri Nasaha, Maana Kwa Hakika Umepotoka.

9. Muda Wote Unawasiliana Naye
Vijana Wa Siku Hizi Ni Watumiaji Wazuri Sana Wa Simu, Lakini Iwapo Utabaini Kuwa Asilimia Kubwa Ya Muda Wako Unautumia Ama Kwa Kuongea Au Kuwasiliana Kwa Ujumbe Mfupi Na Mpenzi Wako, Basi Fahamu Kuwa Kuna Tatizo Ambalo Linahitaji Ufumbuzi Wa Haraka.

Kumbuka Kuwa Mapenzi Hayachukui Nafasi Ya Kila Kitu. Yamkini Huyo Mpenzi Wako Amekukuta Unaishi Na Kuna Mambo Ya Muhimu Ya Kufanya. Hebu Achana Na Simu Kwanza Ufanye Mambo Ya Muhimu Kuhusiana Na Maisha Yako. Kama Mpenzi Wako Hakwelewi Katika Hili Basi Hakufai.

10. Ndugu Zake Wanakufuatilia
Iwapo Utabaini Kuwa Marafiki, Ndugu Na Jamaa Za Mpenzi Wako Wanamtonya Mpenzi Wako Kuhusiana Na Kile Wanachokiita Mwenendo Wako Mbaya, Usipuuze Hali Hii. Kuna Uwezekano Mkubwa Kuwa Watu Hawa Wanayo Sababu Ya Kuwa Na Wasiwasi Na Mwenendo Wako, Kwa Hiyo Jichunguze Na Kuangalia Jinsi Unavyoenenda.

Hata Hivyo, Jambo Hili Si Ishara Njema Ya Mustakabali Mwema Wa Uhusiano Wenu. Iwapo Mpenzi Wako Ataweka Watu Wake Wakufuatilie, Maana Yake Halisi Ni Kwamba Hakuamini. Katika Hali Kama Hii, Haitarajiwi Kuwa Mustakabali Wa Uhusiano Wenu Utakuwa Mzuri, Kwani Kutakuwa Na Uingilizi Mwingi Wa Ndugu, Jamaa Na Marafiki Zake. Unaweza Kukubali Kuendelea Kuishi Katika Hali Hii Kwa Kisingizio Cha Mapenzi, Lakini Ukweli Ni Kwamba Hayatakuwa Mapenzi Bali Karaha.

KUWA MAKINI
Kama Unavyoona, Hizi Ni Baadhi Tu Ya Dalili Kuwa Mapenzi Yako Kwa Mwanamke Sasa Yanaelekea Katika Ulevi, Mithili Ya Ule Wa Dawa Za Kulevya. Jambo Moja La Kukumbuka Ni Kwamba Kweli Mapenzi Ni Kitu Kizuri, Lakini Pia Mapenzi Yanahitaji Kuwa Jambo Linaloashiria Mustakabali Mwema Kwa Wahusika Wawili. Yakiwapo Mambo Haya Kumi Hauwezi Kuwapo Mustakabali Mwema Katika Mapenzi.

15 comments:

Post a Comment