Social Icons

Wednesday, 14 August 2013

HONGERA MBEYA YETU BLOG....Hati ya ushindi ya Mbeya Yetu blog kutoka Tanzania Agricultural Society


Baadhi ya kikosi kazi cha Mbeya Yetu Blog, Kutoka kushoto ni Venance Matinya, Joseph Mwaisango, Ezekiel Kamanga na Fredy Anthony

Chama Cha Wakulima Tanzania (TASO) kanda ya Nyanda za juu Kusini, kimeutunuku cheti mtandao wa kijamii wa www.mbeyayetu.blogspot.com ambao upo chini ya Tone Multimedia Company Limited kutokana na kuibuka mshindi wa kwanza wa kurusha matangazo kwa njia ya Kidigitali katika maonesho ya Wakulima nanenane yaliyofanyika katika viwanja vya John Mwakagale Uyole Jijini Mbeya.

Tuzo hiyo imekuja kutokana na kikosi cha Mtandao huu kuweka kambi katika maonesho hayo na kufanya shughuli za kurusha matangazo moja kwa moja kutoka uwanjani hapo na kuwapagawisha wakulima ambao walipata fursa ya kutembelea banda letu na kujionea habari zilizotokea muda huo huo na kuonekana hewani.

Hongera sana Mbeya Yetu Blog na Tone Media....

0 comments:

Post a Comment