- Je mambo gani umwambie mpenzi wako mpya hasa yanayohusu maisha yako ya zamani (kabla hujakutana naye?)
- Je unatakiwa kusema yooote namaanisha ukweli mtupu kukuhusu wewe, leaving no stone unturned?
- Je ana haki ya kujua kila kitu ulichofanya? matukio yote uliyopitia? mahusiano yote uliyokuwa nayo na details zote kukuhusu wewe?
- Au ni bora ufiche mengineyo hasa kama ushayasahau na ushajifunza kutokana na makosa hayo na maisha yakasonga mbele?
- Mambo kama abortions, magonjwa hatarishi ambayo ushaumwa, ubakaji, mila na desturi za kwenu za hatari ulizofanya, kama ulishawahi kufungwa jela na kwa kosa gani, uliwahi kufilisika na madeni yako yote, historia za kufedhehesha za familia yako?
- Je kipi umezee na kipi useme - swali atakuamini tena pale atakaposikia kwingine yaliyokusibu na hukuwahi kumwambia?
- Vipi kama anataka kujua na akakuuliza - ukakataa katakata hujawahi fanya au kukumbana nayo na baadaye ukweli ukajulikana? Utauweka wapi uso wako?
Tujadiliane.....
0 comments:
Post a Comment