Social Icons

Friday 19 October 2012

MAANDAMANO DAR UPDATES.....


 
POSTA PEUPE.....
 

Picture


Picture

VIPEPERUSHI VYA UCHOCHEZI VIMESAMBAZWA.....
 
Picture
 
 
JESHI LA POLISI LATOA TAMKO......
 
 
Katika taarifa ya waliyoitoa mapema leo asubuhi wakuu na viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwemo wa dini wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadick, aliwatoa hofu wananchi wa Jiji la Dar es Salaam kuendelea na shughuli zao kama kawaida kwani wamejipanga kulinda hali ya amani.

Akitoa tamko hilo, Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa kumekuwapo na taarifa za waumini wa Kiislamu kuandamana na kufanya fujo mara baada ya swala ya Ijumaa na baadala yake amewataka kuacha kufanya hivyo na warejee majumbani kwa amani na suala hilo linashughulikiwa kisheria.

Hata hivyo kwa upande wao viongozi wa dini waliokutana na Mkuu wa mkoa juu ya kutolea tamko hilo waliwaasa waumini wote kutoingia mitaani na kuandamana kwani wakifanya hivyo ni kukiuka misingi mbalimbali ya kisheria iliyopo kihalali na watakapofanya hivyo ni kukiuka sheria za nchi.

Kamanda KovaSheikh wa mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Musa bin Salum amewataka wakuu wa misikiti mkoa wa Dar es Salaam kuwakataza waumini hao kufanya maandamano kwani kufanya hivyo ni kukiuka misingi iliyopo. Aidha, aliwaomba waumini warejee majumbani kwa amani.

Askofu Makunda aliwataka watanzania kuendelea kufuata misingi ya kiimani bila chuki wala kufanya fujo.

Kamanda wa Polisi Kanda maalum mkoa wa Dar es Salaam, Suleiman Kova alitoa onyo kali kwa waislamu kuacha kufanya hivyo hii leo kwani kwa atakaekiuka atachukuliwa hatua kali. Kova aliwataka waumini kurejea majumbani mwao kwa amani bila kufanya maandamano na pia aliwataka wakazi wa jiji la Dar es Salaam kuendelea na shughuli zao kama kawaida na kupuuza tishio hilo la fujo kutoka kwa waislamu.

“Jeshi limejipanga kuakikisha hali ya amani na usalama inakuwepo hivyo taadhari kwa waislamu kuacha kufanya maandamano mara moja” alisema Kova kwenye kikao hicho ambacho kinaendelea hivi sasa.

Wakuu hao wamekutana kwa dharura baada ya kuwepo kwa taarifa za juu ya waumini hao kutishia kuandamana na kufanya fujo.
 
 
Askari mamia kwa mamia wakielekea mitaa ya katikati ya mji kuhakikisha amani ipo

 
 
EE MUNGU TUNUSURU WAJA WAKO........



0 comments:

Post a Comment