Social Icons

Wednesday, 1 February 2012

What earings suit you....Hereni gani zinakufaa....

Hereni gani zinakufaa kulingana na shape ya uso wako na urefu wa shingo yako. Rangi, muonekano na style ya hereni inaweza ikakufanya ukapendeza zaidi au ikakupunguzia mvuto wako.
Kuna aina mbalimbali za shape ya sura kama zifuatavyo:

UNA OVAL FACE SHAPE KAMA:


Oval Face ShapeSura yako ni ndefu kidogo kuliko kuwa pana
  • Paji la uso ni pana kidogo kuliko taya
    Sura yako ni pana kiasi kwenye mashavu ya uso
Taya/Jawline ni la mduara kiasi

      Hereni gani zinafaa:

    • Aina zote za hereni ziwe ndefu\chandelier au ndogo\studs zinapendeza

    UNA USO WA DIAMOND KAMA:



                                                       Taya\Jawline ni refu kiasi
    Diamond Face Shape
    Uso wako ni mrefu zaidi kuliko upana wake.

    Paji la uso ni jembamba kiasi

    Uso wako ni mpana hasa sehemu za mashavu

                                            

    Hereni gani zinafaa:
    • Muhimu ni kuchagua hereni nyembamba ili kuongeza upana kiasi wa taya\jawline
    • Hereni ambazo ni nyembamba juu na nene chini zinafaa zaidi
    • Hereni fupi na nene, studs, zenye maumbo ya duara\oval
    • Epuka hereni ndefu nyembemba  zitaongeza urefu wa kidevu chako
    earrings diamond face
                     Hereni zinazofaa kwa watu wenye Diamond Face

    UNA USO OBLONG KAMA:
    NB: Samahani sikupata maana ya oblong kwa kiswahili

    Oblong Face ShapeUso wako ni mrefu zaidi kuliko upana
    • Paji la uso, mashavu na taya yana urefu karibia sawa
    Mwanzo wa nywele zako kwenye paji la uso ni duara

    Taya\Jawline ina umbo la duara

    Hereni gani zinafaa:
    • Muhimu ni kuchagua hereni ambazo ni pana kiasi kuliko ndefu ili kubalance shape ya uso
    • Hereni za duara\round,square na zenye umbo la kutanda kama feni hivi
    • Hereni ndogo na fupi\studs au zile ndefu\chandelier
    • Hereni kubwa
    • Hereni ambazo ni ndefu zinazoanguka lakini zisipite urefu wa kidevu
    • Epuka hereni flat au nyembamba zinazoanguka
    earrings oblong face
                           Hereni zinazofaa kwa watu wenye Oblong Face


    UNA USO WA SHAPE YA MOYO\HEART FACE KAMA:



    Heart Face ShapeUso wako ni mrefu kiasi kuliko upana wake

    Paji lako la uso ndio sehemu pana zaidi katika uso wako au upana wake unalingana na wa mashavu yako

    Taya\Jawline ni refu na lenye ncha kiasi toka sehemu za mashavu yako


    Hereni gani zinafaa:

    • Muhimu ni kuchagua hereni zenye shape ya kuongeza urefu wa uso na upana katika mashavu\jawline
    • Hereni zinazoning'inia\chandeliers ambazo ni nyembamba juu na pana chini
    • Hereni zenye umbo la mstatili\rectangle na zenye mduara\oval
    • Epuka hereni ambazo zina shape ya uso wako ambazo ni nene juu na nyembamba chini

    earrings heart face
                            Hereni zinazofaa watu wenye uso wa Heart Face


    UNA USO WA MSTATIRI\TRIANGLE FACE KAMA :



    Triangle Face ShapeUso wako ni mrefu zaidi ya upana wake

    Paji lako la uso ni sehemu nyembamba zaidi

    Taya\Jawline ni sehemu pana zaidi katika uso wako

    Hereni zipi zinafaa:

    • Muhimu ni kuvaa hereni ambazo ni ndefu zaidi kuliko pana lengo ni kubalance urefu na upana wa mashavu
    • Hereni ndefu za mduara\oval
    • Hereni zenye mikunjo\curves kwa chini
    • Epuka hereni zenye umbo la mstatiri
    earrings triangle face
                     Hereni zinazofaa wenye uso wa mstatiri\Triangle Face



      UNA USO WA PEMBE NNE\SQUARE FACE KAMA:


    Square Face ShapeUso wako ni mrefu kiasi kuliko upana wake

    Paji la uso ni sehemu nyembamba zaidi

    Taya\Jawline ni sehemu pana zaidi
    • Your face is slightly longer than wide

    • Hereni gani zinafaa:
    • Muhimu ni hereni ambazo ni ndefu zaidi kuliko pana
    • Hereni ndefu zinazoning'inia\chandelier
    • Hereni zenye ngazingazi\multi-tiered
    • Hereni fupi\studs
    • Epuka hereni zenye shape ya mstatiri\square
    earrings square face
                      Hereni zinazofaa watu wenye uso wa mstatiri\Square Face

    UNA USO DUARA\ROUND FACE KAMA:

    Round Face ShapeUso wako unalingana kwa urefu na upana wake

    Uso ni mpana zaidi kwenye mashavu\cheekbones

    Taya lina umbo la mduara\round

    Mwanzo wa nywele zako una umbo la mduara

    Hereni gani zinafaa:
    • Muhimu ni kuvaa hereni ambazo ni ndefu zaidi kuliko pana ili kubalance
    • Hereni ndefu zinazoning'inia\chandelier\drops
    • Hereni za square\oblong\mduara na zinazoning'inia za mstatiri\square drops
    • Epuka studs\hereni fupi au zile kubwa nene chini zitazidisha upana wa sura yako
    earrings round face
                      Hereni zinazofaa watu wenye uso wa mduara\Round Face
       
       
     

    0 comments:

    Post a Comment