Social Icons

Friday, 23 May 2008

Urembo wa macho/Eye make up(Smoky Eyes)



Kuna urembo mbalimbali wa macho kulingana na taste ya mtu na mapendeleo yake . Leo nitazungumzia "smoky eyes" au macho yaliyapambwa kwa eye liner, mascara na eye shadows zenye rangi nyeusi, grey au za mng'aro.

Jinsi ya kuremba jicho:
-hakikisha uso na ngozi inayozunguka jicho ni safi kabla ya kuanza urembo wowote usishawishike kupaka vipodozi juu ya ngozi chafu haitakaa vizuri make up yako. Safisha kwa kutumia face towel iliyochovywa kwenye maji ya moto(huwa naona ni rahisi kwangu hasa kama kitambaa nitumiacho ni cheupe ni rahisi kujua kuwa u msafi au la kwa kuangalia kitambaa) kamwe usioshe uso wako kwa sabuni au maji ya moto. Ngozi ya uso iko rahisi kudhulika ikipata msukosuko kidogo. Sabuni huwa na kemikali nyingi na maji ya moto yanapausha uso. kama utalazimika kutumia sabuni osha uso kwa maji ya baridi kwa muda kiasi ili kuondoa kemikali zitakazokuwa zimeachwa.

- tayarisha kope/eye lids zako kwa kupaka wanja mweusi kwa uangalifu au eyeliner ya dark colour kama ni mtu anayejiamini unaweza tumia rangi yoyote ile sababu si wote wanaweza paka rangi ya njano au kijani na wakawa confident na muonekano wao.

-Kwa matokeo mazuri uwe na eye shadow za aina mbili moja ya rangi iliyokolea na nyingine iliyo light. Anza na rangi iliyo light paka kwa uangalifu kuelekea kona ya nyusi kama picha hapo chini
endelea kama unapenda ming'ao machoni(hususani kwa sherehe) unaweza kupaka juu ya kope zako ila hakikisha hufiki mbali sana karibu na nyusi . Kisha malizia na darker colour kama picha ya kulia inavyoonyesha anzia kona ya kushoto ya jicho kwenda kulia kwa kiasi upendacho.

-Linganisha macho yako yote kama yana muonekano sawa kisha unaweza kuongezea mascara kwa juu ya nyusi ikiwa ni mpenzi.

till next time.....

Wednesday, 21 May 2008

Fashion

Huwa navaa tofauti ninapofeel sexy, happy, sad na mood ya what i wear changes with what i feel and who i am meeting.
Body shapes: can be classified into different categories kuna wanene, wembamba, stick thin/size zero, super models, namba nane, kumi na moja, tisa na kadhalika na kadhalika ila ktk hayo yote mwili wa mwanamke una sifa moja kama atajua jinsi ya kuvaa kulingana na mwili wake na shepu yake hakuna mbaya duniani ila ni jinsi ya kupanga mavazi mwilini.
Kama wewe ni mnene na tipwa tipwa kisha ukatinga mavazi mahsusi ya wale vimbaumbau hakika utaonekana kichekesho bidada. Vaa mavazi yatakayo compliment mwili wako bwana highlight kile muumba alichokupendelea above all jamii yetu inapenda a bit of meat ati.

Kutoka niliyosema wale wembamba kama mie msione hee vipi tena nasi tumependelewa na muumba akha tuna uhuru wa kutinga lolote na tukapendeza bila mikunjo wala mituno inayochora ramani za dunia mwilini mwetu.

Muhimu ladies tuvae kwa stara zetu na kulingana na miili yetu
baadaaye nitakuja na aina mbalimbali za mavazi kwa shepu mbalimbali.....usikose

Fashion

Lets talk about fashion ladies.....
Kila mtu anavaa na ana personal choice kwa anachoamua kuvaa mwilini. Matters za fashion zinatofautiana kutokana na umri,how you feel, uko wapi, na kona ipi ya dunia. Tukubaliane katika hili warembo kuna fashion nyingine ambazo huwezi kuvaa ukiwa nchi kama Tanzania manake watu watakushangaa na mapigo yako.
Just a word of advice kwa wale walio nchi za ughaibuni jaribu kuinvest kwa aina tofauti za mavazi na accessories ambazo zitakuacha ukiwa confident na umevunjia at the same time ukibahatika kwenda likizo Tanzania. Si kila fashion inafaa katika macho ya jamii ya kitanzania it may seem right uliko lakini bado ikaonekana haifai kwa watz. anyway ni mtazamo tu u still have a choice of ur own.