Social Icons

Showing posts with label Siasa. Show all posts
Showing posts with label Siasa. Show all posts

Thursday, 26 November 2015

MAGUFULI AND THE 'HOPE' FOR NEW TANZANIA




The son of a peasant farmer, John Pombe Magufuli won the election to become Tanzania's next president on his 56th birthday
He was never part of the inner-circle of the governing Chama Cha Mapinduzi (CCM) party, so it came as a surprise to his critics that he secured its candidature for the presidency.
His nomination angered ex-Prime Minister Edward Lowassa, who crossed to the opposition to challenge Mr Magufuli for the presidency.
With the backing of CCM machinery, Mr Magufuli won the 29 October poll with 58% of the votes to Mr Lowassa's 40% in a fiercely contested election.
As works minister in the outgoing government, he was reputed to be a no-nonsense, results-driven politician.
His famous motto is ''HAPA KAZI TU'' has really come to action since he was sworn in less than three weeks ago
God bless Our President, God bless Magufuli, God bless Tanzania

Sunday, 3 May 2015

ROYAL PRINCESS CHARLOTTE



 
 
A close-up of the princess in the arms of her mother. 


 
Her Royal Highness Princess Charlotte of Cambridge.
 
 
 
 
The Duke and Duchess make a quick appearance to show Princess Cambridge to an ecstatic crowd
 
Prince William and his son, Prince George, wave as they visit the hospital after the announcement of the princess's birth.
 
Prince William and his son, Prince George wave to the public
 
 


Sunday, 26 April 2015

UNION DAY 2015




 
 





 
Ramani ya Tanzania ambayo ni muungano wa Tanganyika na Zanzibar
 
 
 
 
Waasisi wa Muungano, Julius K. Nyerere na  Abeid Amani Karume siku ya muungano tarehe 26 Aprili 1964

Saturday, 22 March 2014

HOTUBA YA RAIS WA JAMHURIYA MUUNGANO WA TANZANIA,JAKAYA MRISHO KIKWETE, WAKATI WA KULIHUTUBIA BUNGE MAALUM LA KATIBA - 21 MACHI 2014












HOTUBA YA RAIS WA JAMHURIYA MUUNGANO WA TANZANIA,JAKAYA MRISHO KIKWETE, WAKATI WA KULIHUTUBIA BUNGE MAALUM LA KATIBA, TAREHE 21 MACHI, 2014, DODOMA

 Mheshimiwa Samuel Sitta, Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba; Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi; Mheshimiwa... Mizengo Peter Pinda, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;Mheshimiwa Maalim Seif Sharif Hamad, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar; Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi, Makamu wa Pili wa Rais wa ZanzibarMheshimiwa Anne Semamba Makinda; Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano;Mheshimiwa Pandu Ameir Kificho, Spika wa Baraza la Wawakilishi na Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Maalum la Katiba ;Mheshimiwa Rashid Othman Chande, Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Mheshimiwa Othman Makungu, Jaji Mkuu wa Zanzibar; Viongozi Wakuu Wastaafu; Waheshimiwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba; Waheshimiwa Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba; Wageni waalikwa; Mabibi na Mabwana; Pongezi Nakushukuru sana Mheshimiwa Mwenyekiti kwa kunipa fursa ya kuja kuzungumza na Waheshimiwa Wajumbe wa Bunge letu Maalum la Katiba katika siku hii muhimu na ya kihistoria kwa nchi yetu.


Nimekuja kuwatakia heri na naungana na Watanzania wenzetu wote kuwaombea baraka za Mwenyezi Mungu, ili muweze kuifanya kazi yenu kwa utulivu, hekima, umakini mkubwa na kuimaliza kwa salama na kwa mafanikio yanayoyatarajiwa na Watanzania. Natoa pongezi nyingi kwako na kwa Makamu wako kwa kuchaguliwa kwenu kuongoza Bunge hili maalumu na la kihistoria. Ushindi mkubwa mliopata ni kielelezo tosha cha imani kubwa na matumaini waliyonayo Wajumbe wenzenu kwenu. Matumaini yao ndiyo matumaini ya Watanzania wote, kwamba mtaliongoza vizuri Bunge hili, ili liweze kutimiza kwa ufanisi mkubwa jukumu lake muhimu sana katika historia ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mheshimiwa Mwenyekiti; Niruhusu pia niwapongeze kwa dhati Wajumbe wote wa Bunge Maalum la Katiba kwa bahati ya aina yake waliyopata ya kutunga Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Fursa hii hutokea mara chache sana katika historia ya nchi yo yote na watu wake. Mkifanikiwa kuipatia nchi yetu Katiba nzuri majina yenu yataandikwa kwa wino wa dhahabu, katika kumbukumbu za historia ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ni matarajio ya Watanzania kuwa mtatunga Katiba itakayokubalika na wengi. Katiba inayotekelezeka. Katiba itakayoimarisha Muungano wetu kwa kuondoa changamoto zilizopo sasa. Katiba itakayoipa nchi yetu mfumo bora wa kuongoza na kuendesha mambo yetu.

Katiba itakayoimarisha umoja, upendo, ushirikiano na mshikamano miongoni mwa wananchi wa Tanzania, licha ya tofauti zao za asili za upande wa Muungano na maeneo watokako, au tofauti za jinsia, rangi, kabila, dini na ufuasi wa vyama vya siasa. Katiba itakayodumisha amani, usalama na utulivu nchini. Katiba itakayostawisha zaidi demokrasia, haki za binadamu, utawala wa sheria, utawala bora na kudhibiti maovu. Na, mwisho ingawaje siyo mwisho kwa umuhimu, Katiba itakayoweka mazingira mazuri kwa uchumi wa nchi kukua, na wananchi wengi kunufaika sawia na maendeleo yatayopatikana. Historia ya Katiba NchiniMheshimiwa Mwenyekiti na Waheshimiwa Wajumbe; Hii itakuwa mara ya tatu tangu kuzaliwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Aprili 26, 1964, kwa nchi yetu kuwa na mchakato wa kutunga Katiba mpya. Mara ya kwanza ilikuwa mwaka 1965 ilipotungwa Katiba ya Muda na mara ya pili ni mwaka 1977 ilipotungwa Katiba ya Kudumu tuliyonao sasa. Tofauti na mara mbili zilizopita, safari hii mchakato unahusisha watu wengi zaidi. Wananchi wameshiriki moja kwa moja kutoa maoni yao kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, na ndio watakaofanya uamuzi wa mwisho kuhusu Katiba mpya kwa kura ya maoni. Wananchi pia walipata nafasi ya kuchagua Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya yaliyojadili Rasimu ya Kwanza ya Katiba. Pia walipata nafasi ya kutoa maoni yao kupitia Mabaraza ya Katiba ya taasisi. Katika Bunge hili wapo wananchi 201 kutoka makundi mbalimbali. Katika mchakato wa kutunga Katiba za mwaka 1965 na 1977 kulikuwapo Tume za Kuandaa Rasimu na Bunge Maalum la Katiba kama ilivyo katika mchakato huu. Hata hivyo, kwa Katiba zilizopita Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano pekee ndio waliounda Bunge Maalum. Safari hii Bunge Maalum linajumuisha Wabunge, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na wananchi 201 wanaotoka kwenye jamii, wakiwakilisha asasi na makundi mbalimbali ya Watanzania kutoka Zanzibar na Tanzania Bara. Mchakato wa sasa utaishia kwenye kura ya maoni itakayoshirikisha wananchi wote wa Tanzania wanaoruhusiwa kupiga kura. Michakato iliyopita iliishia Bunge Maalum pekee. Mheshimiwa Mwenyekiti;

Tangu kutungwa kwake, tarehe 25 Aprili, 1977, mpaka sasa Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 imefanyiwa mabadiliko takriban mara 14. Mabadiliko hayo yalitokana na kufanyika au kutokea kwa mabadiliko muhimu ya kiuchumi, kisiasa na kijamii katika nyakati mbalimbali hapa nchini na katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kwa ruksa yako naomba nitaje baadhi ya mabadiliko yaliyofanywa:-
1. Mabadiliko ya 1979 yaliunda Mahakama ya Rufani ya Tanzania kufuatia kufa kwa Mahakama ya Rufani ya Afrika Mashariki baada ya kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 1977.
2. Mabadiliko ya mwaka 1980 yalifanyika baada ya kutungwa kwa Katiba ya Zanzibar, hivyo kulazimu Katiba hiyo kutambulika kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano.
3. Mabadiliko ya mwaka 1984 yaliweka utaratibu wa ukomo wa vipindi vya Urais ambao haukuwepo kabla ya hapo. Aidha, masuala ya Haki za Binadamu (Bill of Rights) yaliingizwa kwa mara ya kwanza katika Katiba. Vilevile, Mahakama ya Rufani ya Tanzania na mambo mengine ya iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliongezwa katika Orodha ya Mambo ya Muungano.
4. Mwaka 1992, yalifanyika mabadiliko yaliyoanzisha Mfumo wa Vyama Vingi vya Siasa badala ya ule wa Chama kimoja uliokuwepo tangu 1965. Pia utaratibu wa uchaguzi wa Rais na Wabunge ulirekebishwa ili uendane na mfumo wa vyama vingi vya siasa. Vilevile utaratibu wa kuwa na viti maalum vya wanawake katika Bunge ulianzishwa. Wakati ule ilikuwa asilimia 15 ya Wabunge wote. Aidha, kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu Bunge lilipewa mamlaka ya kumwajibisha Rais na Waziri Mkuu kupitia kura ya kutokuwa na imani.
5. Mabadiliko ya mwaka 1994 yaliweka mfumo mpya wa kumpata Makamu wa Rais kupitia Mgombea Mwenza.
6. Mwaka 2000 na 2005, pamoja na mambo mengine yalifanyika mabadiliko yaliyopanua wigo wa Haki za Binadamu na kuongeza uwakilishi wa wanawake.Umuhimu wa Mabadiliko ya Katiba

Mheshimiwa Mwenyekiti; Kufanyika kwa mabadiliko hayo kunathibitisha utayari wa Serikali kufanya mabadiliko kila ilipoonekana inafaa kufanya hivyo. Pamoja na kufanya yote hayo na Serikali kuwa na msimamo huo, kumekuwepo na madai yaliyokuwa yanajirudia ya kutaka Katiba ya Tanzania iandikwe upya. Wako watu walioimithilisha Katiba yetu na nguo yenye viraka vingi mno kiasi kwamba ingefaa kununua mpya badala ya kuendelea kuivaa. Madai ya kutaka Katiba mpya yalipazwa sauti baada ya kuanza kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa. Wapo waliokuwa wanadai Katiba mpya kwa imani, eti kwamba, itawawezesha kuishinda CCM. Lakini, si hayo tu, hata katika mchakato wa Serikali zetu mbili kushughulikia kero za Muungano, imedhihirika kuwa baadhi ya changamoto zilikuwa zinahitaji mabadiliko ya Katiba ili kuzipatia ufumbuzi wa uhakika na wa kudumu. 





Monday, 9 December 2013

HAPPY INDEPENDENCE TANZANIA....




TANZANIA NATIONAL ANTHEM

1. Mungu Ibariki Afrika


Wabariki Viongozi Wake,

Hekima, Umoja na Amani

Hizi ni Ngao ZetuAfrika na Watu Wake.


Ibariki, Afrika,


Ibariki, Afrika,

Tubariki, Watoto wa Afrika,




2. Mungu Ibariki Tanzania,


Dumisha Uhuru na Umoja,

Wake kwa Waume na Watoto,

Mungu, Ibariki,

Tanzania na Watu Wake

Ibariki, Tanzania,

Ibariki, Tanzania,

Tubariki, Watoto wa Tanzania

 


Wednesday, 28 August 2013

I HAVE A DREAM....







Today August 28th 2013 - its 50th anniversary to Martin Luther King Jr. famous speech "I have a dream" 

If you have a dream, follow it. This is what one man did. You may fell like you are just an normal person who cannot impact others life. No. We are all different. You can succeed your dream, it just needs the effort and time put into it. And faith. Lots of Faith and the matter of not giving up.


If you have a dream, you have a goal. Martin Luther King Jr had a dream and because of it, he moved crowds and changed the lives of many people for the better. His dream gave them hope and strength to fight and take action for their civil rights. Actions are important, of course they are, but the fundamental part is the dream, the project. You can't build a bridge without visualising the project and writing it down on paper, just as you can't do a lab research without asking yourself why and how you'll do it


What is your dream today?

Monday, 1 July 2013

BARACK OBAMA IN TANZANIA.....




 
 
President Obama dancing in Dar es salaam earlier today accompanied by his host H.E President @[33236101224:274:Jakaya Kikwete]
 
U.S. President Barack Obama, basking in an exuberant welcome from Tanzania's streets teeming with well-wishers, today declared a new era in U.S. relations with Africa based on partnership as opposed to charitable aid.
 
 
 
 
"I feel a special connection to this country," Obama said, adding that some of his father's family spent time in Tanzania. "I want to ensure you that love is reciprocated and given back in return."
 
U.S. President Barack Obama, left, and Tanzanian President Jakaya Kikwete applaud a group of performers during an arrival ceremony at Julius Nyerere International Airport in Dar Es Salaam on Monday. Obama was in Tanzania on the final leg of his three-country tour in Africa.
 
'We can't force a solution onto the region,' Obama says in Tanzania on last stop of African tour
 
 
Obama and Kikwete met privately at the Tanzanian State House, an ocean-front government complex that includes the presidential offices. They then held a news conference on the lush grounds outside, with bunting in the colours of the American and Tanzanian flags lining balconies above.
 
 
 


Monday, 6 May 2013

WIMBO WA TAIFA.....


Je unakumbuka verse zote za wimbo wa taifa......Jikumbushe......
 
 

 
Mungu ibariki Africa
Wabariki Viongozi wake
Hekima Umoja na Amani
Hizi ni ngao zetu
Afrika na watu wake.
 
Chorus:
Ibariki Afrika
Ibariki Afrika
Tubariki watoto wa Afrika.
Mungu ibariki Tanzania
Dumisha uhuru na Umoja
Wake kwa Waume na Watoto
Mungu Ibariki,
Tanzania
na watu wake.
 
Chorus:
Ibariki Tanzania
Ibariki Tanzania
Tubariki watoto wa Tanzania.
 
 
 


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI: SALAMU ZA RAIS KIKWETE KWA WATANZANIA....


 
Picture
 
Picture

Wednesday, 1 May 2013

HAPPY LABOUR DAY.....


 
Growing up, i used to think and take advantage of this day catching up with my sleep and relaxing at home. But since i started working this day means more to me and the next 1 year - i am forced to make a follow up with the celebrations and listening to government officials on what they have in store for us workers - if there is anything instore this year!
 
 
Are your hours in a day as summarized like that or less rest and more work?  Enjoy the fruit of your labour
 
 
 
 
 

 


Friday, 26 April 2013

HERI YA SIKU YA MUUNGANO.....


 
 
 
 
 
Mungu ibariki Tanzania
 
Wabariki Watanzania....
 
Tunapoadhimisha miaka 49 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar kuunda Tanzania

Wednesday, 24 April 2013

POZI LA PICHA.....


 
Photo: "Most people who meet my wife quickly conclude that she is remarkable. They are right about this. She is smart, funny and thoroughly charming. Often, after hearing her speak at some function or working with her on a project, people will approach me and say something to the effect of, you know, I think the world of you but your wife, WOW!"

~ President Obama

LORD, help me be the Wife my Husband will be proud of...AMEN!
 
 
Most people who meet my wife quickly conclude that she is remarkable. They are right about this. She is smart, funny and thoroughly charming. Often, after hearing her speak at some function or working with her on a project, people will approach me and say something to the effect of, you know, I think the world of you but your wife, WOW!"

~ President Obama

 
 
 


Thursday, 18 April 2013

WAZIRI LUKUVI ATOA UFAFANUZI WA SH 1Bn ZA MAZISHI YA VIONGOZI.....

 
Dodoma. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi ametoa ufafanuzi kuhusu Sh1 bilioni zilizotengwa kwa ajili ya mazishi ya viongozi wa nchi mwaka huu, akisema ni za kununua eneo ambalo baadhi ya viongozi wa nchi watakuwa wakizikwa.
 
Lukuvi alisema fedha hizo zimetengwa kwa ajili ya kukunua eneo la hekta 129 zilizopo eneo la Iyumba mkoani Dodoma, ili liwe linatumika kwa mazishi ya viongozi hao kwa mujibu wa Sheria ya Maziko ya mwaka 2006.
 
“Fedha hizi zitalipwa kama fidia kwa wale watu wa eneo lile, kwani tayari tulikuwa tumeshapanga kufanya hivyo,” alisema Lukuvi na kuongeza:
“Siyo kila kiongozi atazikwa Dodoma, lakini kuna baadhi watakuwa wakizikwa eneo hilo.”
Lukuvi alisema hiyo inaonyesha kuwa nia ya Serikali kuhamia Dodoma iko palepale, ndiyo maana mwenyewe ni Mwenyekiti wa Bodi ya CDA ili kuharakisha mambo yafanyike haraka.
Lukuvi alilazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya wabunge kulalamikia Ofisi ya Waziri Mkuu kutenga Sh1 bilioni kwa mazishi ya viongozi wa Serikali, wakati wananchi wanaishi hali duni ya umaskini.

 
Lukuvi alikuwa anajibu michango ya wabunge, akiwamo Lucy Owenya (Viti Maalumu - Chadema), aliyelalamikia kitendo hicho akieleza kuwa haiwezekani fedha hizo zikatengwa wakati haijulikani viongozi wangapi watakufa kwa mwaka huu.
 
Miongoni mwa wabunge ambao wamepinga kutengwa kwa fedha hizo ni Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola ambaye alidai fedha hizo ni ulaji kwa baadhi ya watu na kutoa wito kwa wenzake kutopitisha fedha hizo.
 
Hata hivyo, tangu kupitishwa Sheria ya Maziko ya Viongozi mwaka 2006, hakuna kiongozi ambaye amezikwa Dodoma ambako kunaelezwa kuwa watakuwa wakizikwa. Viongozi wengi huzikwa mikoa wanayotoka.

Source: http://www.mwananchi.co.tz/habari/habari-ya-ndani/-/1724700/1751644/-/vcarha/-/index.html

Sunday, 14 April 2013

SERIKALI YAOMBA BILIONI MOJA KUZIKA VIONGOZI WATAKAOKUFA 2013 - 2014.....



 
 

Katika hali inayotafsiriwa kuwa ni ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha za umma, Ofisi ya Waziri Mkuu, imeomba Shilingi bilioni moja kwa ajili ya kuwazika viongozi wa kitaifa watakaokufa katika mwaka wa fedha unaoanza Juni, mwaka huu.

Iliwasilisha ombi hilo kwenye bajeti yake iliyosomwa bungeni Jumatano wiki hii.


Kufuatia ombi hilo, wabunge Lucy Owenya Viti maalumu (Chadema) na Kange Lugora (CCM) Mwibara, wameishambulia ofisi hiyo na kuhoji ni viongozi gani wa kitaifa watakaokufa mwaka ujao.

Owenya ndiye aliyeibua hoja hiyo wakati akichangia hotuba ya makadirio na matumizi ya ofisi hiyo iliyowasilishwa bungeni Jumatano wiki hii na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Owenya alisema inashangaza kutumia mabilioni kwa watu watakaokufa badala ya kuwekeza fedha hizo kwa maendeleo ya walio hai.

Aliitaka Ofisi ya Waziri Mkuu kupunguza fedha hizo na kujenga chumba cha upasuaji cha hospitali ya Mawenzi na kuisaidia hospitali teule ya St Joseph kununua vitanda vya wodi ya wazazi.

Lugora kwa upande wake akiponda bajeti hiyo alisema licha ya kuwa mbunge wa CCM haungi mkono bajeti ya Waziri Mkuu, akiituhumu kuomba kutengea Sh bilioni kwa ajili ya mazishi ya viongozi watakaokufa ni ubadhirifu.

“Siungi mkono hoja mpaka nione bajeti inaeleza mikakati na dhamira ya dhati ya kumaliza rushwa na dawa za kulevya nchini,” alisema.
“Mazishi gani ya viongozi bilioni moja huu ni wizi, wizi mtupu ndani ya serikali kama wasipokufa tutapata ripoti ya matumizi mengine ya fedha hizo.”

S
oma zaidi habari hii http://thedonsimon.blogspot.com/2013/04/serikali-yaomba-shbilmoja-kuzika.html?spref=fb

Friday, 12 April 2013

ROLE MODEL: CONDOLEEZZA RICE....


 
 
 
Condoleezza Rice is the first black woman to serve as the United States' national security adviser, as well as the first black woman to serve as U.S. Secretary of State (2005-09).