Social Icons

Showing posts with label Humour. Show all posts
Showing posts with label Humour. Show all posts

Saturday, 4 May 2013

WHAT TO WEAR.....


 
 
 
 
 
 
An average woman spend nearly a year in their lifetime deciding on what to wear.....no wonder we always have nothing to wear even though our wardrobes are full of clothes.


Thursday, 18 April 2013

WAZIRI LUKUVI ATOA UFAFANUZI WA SH 1Bn ZA MAZISHI YA VIONGOZI.....

 
Dodoma. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi ametoa ufafanuzi kuhusu Sh1 bilioni zilizotengwa kwa ajili ya mazishi ya viongozi wa nchi mwaka huu, akisema ni za kununua eneo ambalo baadhi ya viongozi wa nchi watakuwa wakizikwa.
 
Lukuvi alisema fedha hizo zimetengwa kwa ajili ya kukunua eneo la hekta 129 zilizopo eneo la Iyumba mkoani Dodoma, ili liwe linatumika kwa mazishi ya viongozi hao kwa mujibu wa Sheria ya Maziko ya mwaka 2006.
 
“Fedha hizi zitalipwa kama fidia kwa wale watu wa eneo lile, kwani tayari tulikuwa tumeshapanga kufanya hivyo,” alisema Lukuvi na kuongeza:
“Siyo kila kiongozi atazikwa Dodoma, lakini kuna baadhi watakuwa wakizikwa eneo hilo.”
Lukuvi alisema hiyo inaonyesha kuwa nia ya Serikali kuhamia Dodoma iko palepale, ndiyo maana mwenyewe ni Mwenyekiti wa Bodi ya CDA ili kuharakisha mambo yafanyike haraka.
Lukuvi alilazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya wabunge kulalamikia Ofisi ya Waziri Mkuu kutenga Sh1 bilioni kwa mazishi ya viongozi wa Serikali, wakati wananchi wanaishi hali duni ya umaskini.

 
Lukuvi alikuwa anajibu michango ya wabunge, akiwamo Lucy Owenya (Viti Maalumu - Chadema), aliyelalamikia kitendo hicho akieleza kuwa haiwezekani fedha hizo zikatengwa wakati haijulikani viongozi wangapi watakufa kwa mwaka huu.
 
Miongoni mwa wabunge ambao wamepinga kutengwa kwa fedha hizo ni Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola ambaye alidai fedha hizo ni ulaji kwa baadhi ya watu na kutoa wito kwa wenzake kutopitisha fedha hizo.
 
Hata hivyo, tangu kupitishwa Sheria ya Maziko ya Viongozi mwaka 2006, hakuna kiongozi ambaye amezikwa Dodoma ambako kunaelezwa kuwa watakuwa wakizikwa. Viongozi wengi huzikwa mikoa wanayotoka.

Source: http://www.mwananchi.co.tz/habari/habari-ya-ndani/-/1724700/1751644/-/vcarha/-/index.html

Sunday, 14 April 2013

SERIKALI YAOMBA BILIONI MOJA KUZIKA VIONGOZI WATAKAOKUFA 2013 - 2014.....



 
 

Katika hali inayotafsiriwa kuwa ni ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha za umma, Ofisi ya Waziri Mkuu, imeomba Shilingi bilioni moja kwa ajili ya kuwazika viongozi wa kitaifa watakaokufa katika mwaka wa fedha unaoanza Juni, mwaka huu.

Iliwasilisha ombi hilo kwenye bajeti yake iliyosomwa bungeni Jumatano wiki hii.


Kufuatia ombi hilo, wabunge Lucy Owenya Viti maalumu (Chadema) na Kange Lugora (CCM) Mwibara, wameishambulia ofisi hiyo na kuhoji ni viongozi gani wa kitaifa watakaokufa mwaka ujao.

Owenya ndiye aliyeibua hoja hiyo wakati akichangia hotuba ya makadirio na matumizi ya ofisi hiyo iliyowasilishwa bungeni Jumatano wiki hii na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Owenya alisema inashangaza kutumia mabilioni kwa watu watakaokufa badala ya kuwekeza fedha hizo kwa maendeleo ya walio hai.

Aliitaka Ofisi ya Waziri Mkuu kupunguza fedha hizo na kujenga chumba cha upasuaji cha hospitali ya Mawenzi na kuisaidia hospitali teule ya St Joseph kununua vitanda vya wodi ya wazazi.

Lugora kwa upande wake akiponda bajeti hiyo alisema licha ya kuwa mbunge wa CCM haungi mkono bajeti ya Waziri Mkuu, akiituhumu kuomba kutengea Sh bilioni kwa ajili ya mazishi ya viongozi watakaokufa ni ubadhirifu.

“Siungi mkono hoja mpaka nione bajeti inaeleza mikakati na dhamira ya dhati ya kumaliza rushwa na dawa za kulevya nchini,” alisema.
“Mazishi gani ya viongozi bilioni moja huu ni wizi, wizi mtupu ndani ya serikali kama wasipokufa tutapata ripoti ya matumizi mengine ya fedha hizo.”

S
oma zaidi habari hii http://thedonsimon.blogspot.com/2013/04/serikali-yaomba-shbilmoja-kuzika.html?spref=fb

BEAUTIFUL......


 
Do you love this??
 
 
Who wouldn't want to spend a night here....