Social Icons

Thursday 11 October 2012

ROTARY DAR MARATHON JUMAPILI YA TAREHE 14 OCTOBER, 2012

 
ROTARY CLUB KUCHANGISHA MILIONI 560 KWA AJILI YA KUJENGA HOSPITALI YA SARATANI KWA WATOTO
 
 
 
Shilingi milioni 560 zinatarajiwa kuchangishwa kwa ajili ya kusaidia ununuzi wa vifaa vya hospitali katika wodi ya wagonjwa wa saratani kwa watoto ambayo itajengwa katika hospitali ya taifa ya muhimbili iliyopo jijini dar es salaam.

Tayari ujenzi wa hospital hiyo umeanza kufanyika ambapo upo katika ngazi ya uchoraji wa ramani ambao ujenzi mzima utagharimu shilingi million 750 na itakuwa na ubora mkubwa kuliko nchi nyingine yeyote kusini mwa jangwa la sahara.

Taasisi ya kusaidia jamii ya Rotary Club kwa kushirikiana na wafadhili mbalimbali wameandaa mbio za hisani zitakazo shirikisha zaidi ya wakimbiaji 5000 (mimi pia nikiwa mmoja wao na wafanyakazi wenzangu wa First National Bank) kwa lengo la kuchangisha fedha hizo na baadaye kuzitumia kwa ununuzi wa vifaa hivyo vya hospitali.


Naye mwenyekiti wa mbio hizo ambazo zitafanyika siku ya Kumbukumbu ya siku ya kifo cha baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwezi Octoba tarehe 14 Zainul Dossa amesema kuwa lengo ni kuhakikisha taasisi yake inawafikia wananchi wenye mahitaji mbalimbali ambao kwa kiasi kikubwa hawana uwezo wa kifedha.

Karibuni sana kudhamini mbio na matembezi haya ya hisani tuokoe watoto wanaosumbuliwa na saratani za aina mbalimbali ambapo matibabu yake bado yanaleta changamoto kubwa kwa jamii ya kitanzania.

Tukutane Police officers mess saa kumi na mbili asubuhi jumapili ya tarehe 14 October 2012 kuanza mbio/matembezi haya ya hisani.

 
Kinga ni bora kuliko tiba......watoto wengi wanateseka kwa saratani ambazo kama zingegundulika na kutibiwa mapema kwa vifaa husika madhara makubwa yangeweza kuepukika. Tanzania ni mimi na wewe katika kuijenga Tanzania yetu......



0 comments:

Post a Comment