Social Icons

Tuesday 9 October 2012

SECRETS TO A BEAUTIFUL SKIN.....


 
 
 
You too can have a beautiful complexion that is free from acne/chunusi, madoa doa na matatizo mbalimbali yaikumbayo ngozi isiyotunzwa vyema.
 
Jifunze njia zifuatazo na yapi ya kuepuka ili uwe na ngozi inayong'ara na ya kuvutia.......
 
  • Je, unalala vya kutosha...
 
 
Ukosefu wa kulala kwa muda ulioshauriwa na wataalamu wa afya wa masaa yasiyopungua 8 husababisha ngozi kuchoka, kuzeeka na kupunguza mng'aro wake. Muda unaolala mwili huwa unajirutubisha kwa kubadili seli za mwili zilizokufa ukipunguza muda wa kupumzika/kulala unakatisha process hiyo. Pia kukosa usingizi kunasababisha matatizo mbali mbali ya ngozi kama chunusi, eczema na psoriasis.
 
  • Kutumia bidhaa ambazo haziendani na aina ya ngozi yako
  •  
     
    Je unajua ngozi yako ni ya aina ipi? oily, dry or combination skin?
     
    Kama hujui aina ya ngozi yako kuna hatari ya kutumia bidhaa/products za aina nyingine ya ngozi na kuleta madhara kwenye ngozi yako.
     
    Kwenye topic nyingine nitaongelea jinsi ya kujua aina ya ngozi yako na nini cha kutumia ili uwe na ngozi inayong'ara....
     
  • Kusahau shingo na kifua kwenye skincare regime yako
 
 
Wengi huwa tunaangalia sana ngozi ya usoni na kuijali kwa kila kitu je wajua kuwa ngozi yako ya kifuani na shingo vinahitaji uangalifu wa juu pia? Haipendezi kuwa na uso mng'aavu na smooth wenye kupendeza juu ya shingo na mabega yenye mabaka na madoa doa
TIP: Face cream uitumiayo waweza kuipaka shingoni na kifuani kwa kung'arisha maeneo hayo pia
 
  •         Make up brushes.....unazisafisha?
 
 
 
Baada ya shughuli za kila siku kusafisha make up brushes na vingine utumiavyo kupaka cosmetics zako ni kitu cha mwisho kufikiria. Ila ukweli ni kwamba unavyotumia make up brushes chafu unafanya madhara zaidi kwa ngozi yako na usishangae chunusi zitakapoanza kukuandama na matokeo yake utatumia make up nyingi zaidi kuziba matatizo hayo hapo ule usemi wa 'make up imedunda' unapokuja kutumika.
 Wataalamu wanashauri uoshe brush zako za make up atleast mara moja kwa mwezi kwa kutumia mild shampoo/detergent uziache zikauke zenyewe kabla ya kuzitumia tena unless una mpango wa kununua make up brushes na utensils every now and then.....
 
  • Kuongea na simu muda mrefu kunaidhuru ngozi yako
 
Hata kama simu ni safi au sio jambo ambalo si mara nyingi (tuwe wakweli simu zetu ni moja ya kitu kichafu tunachoshinda nacho kutwa nzima) ule msuguano na joto linalosababishwa na kuiegemeza sikioni mwako unaweza kusababisha chunusi (jaribu kuangalia chunusi huwa zinakutokea zaidi upande upi wa uso wako, utashangaa kujua mara nyingi ni ule upande tunapoegemeza simu sikioni mwetu......chunguza!)
 
TIP: Kama una maongezi ya muda mrefu bora utumie headset (i think thats why call center agents use headsets :) )
 
 
 
 


0 comments:

Post a Comment