Social Icons

Thursday, 9 May 2013

UKWELI MTUPU....


 
Tatizo la msingi tulilo nalo katika nchi yetu kwa sasa utabaini kuwa sio maisha magumu na wala sio ukosefu wa ajira isipokuwa ni mfumo mbaya wa kifikra ambao ni tegemezi kwa serikali. Kila anaesoma anawaza kuajiriwa na kwa sababu ajira (za kuajiriwa) ni chache wanapata wachache na waliobakia wanabaki kuwa mzigo ama hatari kwa taifa. 

Kama wiki zilizo pita nimepokea email zaidi ya 32 kutoka kwa rafiki zangu wakiomba ushauri, wa jinsi ya kuwekeza kwenye kilimo cha miti na mboga mboga, nimejitahidi kujibu kadri ya uwezo wangu, wengi wamebadirika na wamechukua hatua,wengi wao wamesafiri kutoka walipo,wamekuja Iringa,wengine tumewasiliana kwa simu na wameshanunua mashamba. Nimewapa elimu na fursa,,, Nitafurahi zaidi kuwaona watu wengi wakiwa wajasiriamali na hivyo kuondoa malalamiko na kkupoteza nguvuzetu kwa Kuwa washabiki wa mambo yasiyo tuhusu,na mwisho wake tuwe ombaomba...KARIBUNI SANA IRINGA. MY PERSONAL GOAL IS: ADDING VALUE FOR THE PEOPLE OF THIS GENERATION AND THOSE THAT FOLLOW.

0 comments:

Post a Comment