Social Icons

Tuesday 24 July 2012

KUEPUKA KUSALITIWA FUATA YAFUATAYO......


MAMBO MUHIMU YA KUYAFAHAMU ILI KUEPUKA KUSALITIWA.

Photo: MAMBO MUHIMU YA KUYAFAHAMU ILI KUEPUKA KUSALITIWA.

1.Amini Hawezi Kukusaliti
Jambo La Kwanza Kabisa Ni Kujenga Imani Kwamba Mpenzi Wako Anakupenda, Anakuheshimu Na Kukuthamini Hivyo Hawezi Kushawishika Kwa Namna Yoyote Ile Kukusaliti.

Hii Itakufanya Kuwa Na Furaha Na Yeye, Pia Utamfanyia Mambo Ya Kumfurahisha. Ukiwa Huna Imani Na Mpenzi Wako, Unaweza Kujikuta Unapunguza Mapenzi Kwake Na Matokeo Yake Ukachochea Yeye Kuanza Kukusaliti.

2.Mtosheleze
Mpenzi Wako Mchukulie Kama Mtoto. Unapomlisha Unahakikisha Ameshiba Ndiyo Unamuacha. Akitaka Pipi Unamnunulia. Vivyo Hivyo Kwa Mpenzi Wako. Mtoshelezea Katika Kila Nyanja.

3.Muoneshe Upendo Wa Hali Ya Juu, Mpe Heshima Anayostahili Na Pale Mnapokuwa Kwenye Mambo Yetu Yalee, Mpe Hadi Aseme Nimeshiba Mpenzi Wangu. Ukifanya Hivyo Aende Nje Kutafuta Nini? Akienda, Huyo Ana Tamaa Zake Za Kijinga Na Ukibaini Muache Haraka.

4.Zungumza Naye
Ndiyo, Vunja Ukimya, Zungumza Naye! Si Vibaya Ukawa Unazungumza Na Mpenzi Wako Juu Ya Mambo Yahusuyo Uhusiano Wenu. Muulize Ni Mambo Gani Ukimfanyia Anasikia Furaha, Akikuambia Na Mambo Hayo Yakawa Ndani Ya Uwezo Wako, Jitahidi Kumtimizia.

5.Muulize, Anachukizwa Na Mambo Gani, Akikuambia Basi Jiepushe Nayo. Hata Asipokuambia, Ukimchunguza Utayabaini Tu.
Hayo Ni Baadhi Tu Ya Mambo Ambayo Ukiyazingatia Yanaweza Kukusaidia Katika Kumfunga ‘Spidi Gavana’ Kimtindo Mpenzi Wako Ili Asikusaliti. Kama Itatokea Akakusaliti Licha Ya Kumfanyia Yote Hayo, Huyo Siyo Mtu Wa Kuendelea Kuwa Naye.

Usaliti unauma, unaumiza unaweza ukakutia kichaa au ukakutoa roho hivihivi.....

Dr Love anatuambia ya kufanya ili kupunguza au kuepuka kusalitiwa na wandani wetu.

Karibuni........http://mwanadada.blogspot.com/p/the-dondr-love.html

0 comments:

Post a Comment