Social Icons

Showing posts with label Wema Sepetu. Show all posts
Showing posts with label Wema Sepetu. Show all posts

Monday, 5 May 2014

KTMA 2014: HONGERA DIAMOND PLATNUMZ...



 

Diamond1




WIMBO BORA WA AFRO POP – DIAMOND PLUTNUM
 
 
MWIMBAJI BORA WA KIUME KIZAZI KIPYA – DIAMOND PLUTNUMZ
 
 
MTUNZI BORA WA MWAKA KIZAZI KIPYA – DIAMOND PLUTNUMZ
 
 
WIMBO BORA WA KUSHIRIKIANA – MUZIKI GANI NEY WAMITEGO ft DIAMOND
 
 
VIDEO BORA YA MWAKA – NUMBER ONE DIAMOND
 
 
WIMBO BORA WA MWAKA – NUMBER ONE DIAMOND
 
 
MTUMBUIZAJI BORA WA KIUME – DIAMOND
 
 
 
Diamond_Pltnumz
 
 
The saying stays soo true "Behind a successful man, is a strong woman"
 
 
 
Wema looking divinely beautiful in her Eve Collections dress


Tuesday, 26 March 2013

SPOTTED: WEMA SEPETU.....


 
 
 
She is a beauty with a beautiful and kind heart.....to Kajala she will always be a true friend and a hero #Endless Fame indeed...
 
 
By our names so we shall be....#Big up Wema Sepetu

Monday, 25 March 2013

MSANII KAJALA AACHIWA HURU....


 
SHAHIDI wa nne Monika Timber (41), amedai mahakamani katika kesi ya kula njama, kuhamisha umiliki wa nyumba na utakatishaji wa fedha inayomkabili msanii wa filamu nchini Kajala Masanja na mume wake Faraja Chambo kuwa nyumba hiyo ya washtakiwa iliuzwa wakati zuio lililotolewa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) bado muda wake haujamalizika.
Kadhalika, shahidi huyo ambaye ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kunduchi Salasala, amedai kuwa Takukuru walitoa zuio la nyumba hiyo kufanyiwa chochote ikiwamo kuuzwa hadi uchunguzi wa kesi ya utakatishaji fedha haramu inayomkabili mshtakiwa Chambo utakapomalizika.
Timber alitoa ushahidi wake leo mbele ya Hakimu Mkazi Sundi Fimbo anayesikiliza kesi hiyo.
Akiongozwa na Mwendesha Mashtaka Takukuru, Leonard Swai shahidi huyo alidai kuwa taasisi hiyo ilitoa zuio la kwanza Julai 15, mwaka 2009 ikimtaka mmiliki kutofanya kitu chochote ndani ya miezi 6 kwa kuwa inafanyiwa uchunguzi.
Alidai kuwa baada ya muda wa zuio lile kumalizika, Takukuru waliwasilisha zuio la pili Februari 18, mwaka 2010 lakini kabla muda wake kumalizika nyumba iliuzwa.
 
"Nyumba ile ilipouzwa ofisi yangu haikuhusishwa na muuzaji wala mnunuaji ...nilihojiwa na Takukuru baada ya ile nyumba kuuzwa nikawaeleza sikuwa na taarifa kwa sababu zuio bado lilikuwa halijamalizika muda wake," alidai Timber.
Katika kesi hiyo, Kajala na Chambo, wanakabiliwa na shtaka la kula njama ya kuhamisha umiliki wa nyumba iliyoko Kunduchi Salasala jijini Dar es Salaam kinyume na kifungu cha 34 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007 wakijua ni kosa kwani tayari Mwanasheria Mkuu wa serikali alishazuia kuuzwa kwa nyumba hiyo.
Shtaka la pili, ilidaiwa kuwa Aprili 14, mwaka 2010 washtakiwa hao walihamisha isivyo halali umiliki wa nyumba hiyo kwenda kwa Emiliana Rwegarura huku wakijua imepatikana kwa njia ya rushwa kinyume na kifungu cha 34(2)A(3) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007.
Katika shtaka la tatu ilidaiwa kuwa siku na mahali hapo washitakiwa hao walitakatisha fedha huku wakijiua ni kinyume na sheria hiyo.
Washtakiwa walikana mashtaka yote kwa nyakati tofauti kutokana na mashtaka yanayowakabili kutokuwa na dhamana kisheria. Washtakiwa wako mahabusu mpaka kesi itakapotolewa uamuzi.
 
KAJALA AHUKUMIWA MIAKA 5, MUMEWE MIAKA 7

 HUKUMU ya kesi iliyokuwa inamkabili staa wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja na mumewe imetolewa leo na Hakimu Sundi Fimbo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar. Katika hukumu hiyo Kajala amehukumiwa kwenda jela miaka mitano au kulipa faini ya shilingi milioni 13 na mumewe kwenda jela miaka saba au kulipa faini ya shilingi milioni 200.
Kajala alikuwa anakabiliwa na kesi ya kuuza nyumba iliyowekwa kizuizini na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) baada ya mumewe, Faraji Agustino kukumbwa na msala wa kutakatisha fedha haramu.
 
 
Ashukuriwe Mungu
 
Anaonekana akiwa haamini lililotokea
 
Speechless.
Wamuache apumzishe kichwa kwanza jamaniiii
 
 
Akiwa na msanii mwenzake Wema Sepetu