Social Icons

Showing posts with label Fundraising. Show all posts
Showing posts with label Fundraising. Show all posts

Tuesday, 31 December 2013

LADIES IN VISION WATEMBELEA KITUO CHA WATOTO - KIMARA.....




Mwanadada ni mmoja wa wanachama wa kikundi cha Ladies in Vision, pichani ni watoto na walezi wa kituo cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Kimara chini ya uongozi wa Evans Tegete ambaye ni mwanzilishi wa kituo hicho nia na madhumuni ni kulea watoto walio katika mazingira magumu bila kujali kama ni yatima au la mradi wanaishi katika mazingira magumu na hatarishi.

Kituo kina watoto 70 kwa sasa umri wao ni kuanzia miaka 19 kushuka chini wengi wapo shule za msingi, sekondari na vyuoni.

Changamoto za kituo ni:

1. Ada za shule za watoto
2. Wagonjwa na matibabu yao
3. Vifaa vya shule na hela za nauli
4. Chakula

Malengo ya kituo kwa mwaka 2014:

1. Wanatayarisha album ya kwaya yao ya kituo ili waweze kukusanya milioni 9 za kupata hati miliki za kiwanja cha kituo kilichopo Bagamoyo ukubwa wa eka 50

Mwanadada tuko pamoja na kituo kusupport uuzwaji wa hii album na kuraise hiyo hela ikiwa tayari





Baadhi ya watoto wa kituo na wanachama wa LIV wakijumuika pamoja kusikiliza kwaya ya kituo

Mwanzilishi na kiongozi wa kituo, Evans Tegete akizungumza na watoto na LIV 






Amon them are future lawyers, doctors, economists, politicians etc etc and they are very determined in their dreams and visions of life.
 


Ladies in Vision tukikabidhi baadhi ya vifaa kwa kituo kwa ajili ya msimu wa shule unaonza Januari


Watoto hawa wana tabasamu angavu licha ya majaribu waliyopitia maishani mwao



These are my new 'adopted kids' they didn't have the best of situations and circumstances in their early lives as some are orphans and come from broken homes but in them I have seen the most widest smiles, they are well disciplined and focused in life.



Ladies in Vision - Tawi la Dar es salaam, tuliwawakilisha wenzetu


Pichani tukiwa na dada Vailet na dada Wensa wakiwa katika pozi na LIV


God bless these kids and everyone that looks after them, I was very touched by this visit and I hope it is the first among the many that I will have to this centre. ....



Monday, 12 November 2012

ELIMU YAO, WAJIBU WETU.....CHARITY WALK.....


 
 
 
Jumamosi tarehe 17/11/2012 kuanzia Mlimani City kupitia Chuo cha Ardhi mpaka viwanja vya michezo vya Chuo Kikuu Dar es salaam.  Saa moja kamili mpaka saa tano asubuhi
 
 
Karibuni tushiriki pamoja tuchangishe pesa za kujenga hosteli za wasichana Tanzania....
 
 
Ni mtoto wako, ndugu yako na wetu sote......
Elimu yao, wajibu wetu

Friday, 19 October 2012

WAFANYE WATABASAMU.......


Watoto wengi walio mahospitalini kwa magonjwa mbalimbali wanakosa nafasi ya kuutumia utoto wao kufanya mambo mbalimbali yanayowahusu laiti kama wangekuwa wazima wenye afya yao.

Mchoraji maarufu wa 'vibonzo' Tanzania, Nathan Mpangala anaendesha mradi wa 'WAFANYE WATABASAMU' kuwezesha watoto kufikisha hisia zao za maumivu, mateso,hofu na woga,  matamanio kwa njia ya michoro kutoka mahospitalini.

 
 
 
 
 
 
 
Big up Nathan Mpangala......kwa habari zaidi na picha za mradi huu mtembelee:
 

Monday, 15 October 2012

DAR ROTARY MARATHON 2012.....

 
Matembezi ya hisani yalikuwa na lengo la kukusanya kiasi cha shilingi milioni 560 zikakusanywa kiasi cha bilioni moja na milioni 12 (1.12bn) kwa ajili ya ujenzi wa kitengo cha saratani ya watoto katika hospitali ya taifa ya Muhimbili.
 
Takwimu zinaonyesha mwaka 2007 uwezekano wa watoto wenye saratani kutibiwa na kupona kabisa ulikuwa kwa asilimia 12 tu ukilinganisha na asilimia 80 kwa nchi zilizoendelea. Mpaka sasa takwimu zinaonyesha uwezekano huo umepanda kwa karibu asilimia 50 katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kama matibabu yatafanyika mapema pale dalili zinapogunduliwa. Changamoto zinazoikabili Muhimbili kwa sasa ni msongamano wa wagonjwa na maambukizi ya magonjwa yanayoepukika kiurahisi. Tatizo hili litakabiliwa kama kitengo kipya cha watoto wenye saratani kitajengwa.
 
Takwimu zinaonyesha kuna maambukizi 2000 mapya ya magonjwa ya saratani kwa mwaka na uwezo wa vitengo vyetu vilivyopo kukabiliana na saratani ni kutibia watoto 400 tu kwa mwaka.
 
 

 
FNB TEAM wakiwakilisha
 
Rais mstaafu wa awamu ya pili, Mh. Ali H. Mwinyi akiwa sambamba na watembeaji wengine

 
Nikiwakilisha FNB na wadau wengine

 
Mwamko ulikuwa mkubwa sana na wengi walijitokeza asubuhi na mapema viwanja vya Police officers mess


 
 
 Wanafunzi toka shule mbalimbali waliwakilisha na mwamko ulikuwa wa hali ya juu.
 

Bravo Rotary Club na taasisi nyingine zote zilizoshiriki katika hili.....Tanzania itajengwa na mimi na wewe......
 


Friday, 12 October 2012

ROTARY DAR MARATHON 2012.....


 
 
T-shirt yangu tayari kwa matembezi ya hisani ya Rotary hiyo Jumapili tarehe 14 october 2012

 
 
Tukutane pale Police officers mess saa kumi na mbili asubuhi kuanza safari yetu
 
Come one.....come all and sponsor this marathon

Thursday, 11 October 2012

ROTARY DAR MARATHON JUMAPILI YA TAREHE 14 OCTOBER, 2012

 
ROTARY CLUB KUCHANGISHA MILIONI 560 KWA AJILI YA KUJENGA HOSPITALI YA SARATANI KWA WATOTO
 
 
 
Shilingi milioni 560 zinatarajiwa kuchangishwa kwa ajili ya kusaidia ununuzi wa vifaa vya hospitali katika wodi ya wagonjwa wa saratani kwa watoto ambayo itajengwa katika hospitali ya taifa ya muhimbili iliyopo jijini dar es salaam.

Tayari ujenzi wa hospital hiyo umeanza kufanyika ambapo upo katika ngazi ya uchoraji wa ramani ambao ujenzi mzima utagharimu shilingi million 750 na itakuwa na ubora mkubwa kuliko nchi nyingine yeyote kusini mwa jangwa la sahara.

Taasisi ya kusaidia jamii ya Rotary Club kwa kushirikiana na wafadhili mbalimbali wameandaa mbio za hisani zitakazo shirikisha zaidi ya wakimbiaji 5000 (mimi pia nikiwa mmoja wao na wafanyakazi wenzangu wa First National Bank) kwa lengo la kuchangisha fedha hizo na baadaye kuzitumia kwa ununuzi wa vifaa hivyo vya hospitali.


Naye mwenyekiti wa mbio hizo ambazo zitafanyika siku ya Kumbukumbu ya siku ya kifo cha baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwezi Octoba tarehe 14 Zainul Dossa amesema kuwa lengo ni kuhakikisha taasisi yake inawafikia wananchi wenye mahitaji mbalimbali ambao kwa kiasi kikubwa hawana uwezo wa kifedha.

Karibuni sana kudhamini mbio na matembezi haya ya hisani tuokoe watoto wanaosumbuliwa na saratani za aina mbalimbali ambapo matibabu yake bado yanaleta changamoto kubwa kwa jamii ya kitanzania.

Tukutane Police officers mess saa kumi na mbili asubuhi jumapili ya tarehe 14 October 2012 kuanza mbio/matembezi haya ya hisani.

 
Kinga ni bora kuliko tiba......watoto wengi wanateseka kwa saratani ambazo kama zingegundulika na kutibiwa mapema kwa vifaa husika madhara makubwa yangeweza kuepukika. Tanzania ni mimi na wewe katika kuijenga Tanzania yetu......



Monday, 13 August 2012

JANGWANI GIRLS' SEC SCHOOL.......





Je, ulisoma Jangwani Girls' Secondary School.......au una mapenzi mema na Jangwani......


Ukikumbuka Jangwani nini kinakujia kichwani............



Unakumbuka madarasa yetu? Uniform zetu ambazo zilitutambulisha kwa madaha barabarani......



Mazingira haya yanakukumbusha nini?.......

Tumekutana na marafiki wa kudumu maisha na wengine tumekuwa kama ndugu sababu ya Jangwani.....

Najivunia kuwa 'Jangwani Product' .......wewe je........

Stay tuned........