1/2 IMEPITA RUDISHA AKILI TAR 1 JAN
Miezi 6 imeisha na leo ni tarehe moja Julai. Tumeanza kushuka au kupanda miezi 6 mingine mbele. Nakuomba rudisha akili na mawazo yako nyuma hadi tar 1 januari wakati unatoka katika mkesha wa mwaka mpya. Sijajua kama kuna mambo ulijiapia huu mwaka hauishi utakuwa umeyatimiza. Kuna ambao walienda hatua moja zaidi wakayaandika. Lakini kuna ambao hawakuona chochote kwao ilikuwa kawaidia bora liende.
Wakati tunaanza safari katika mwaka huu tulianza wote pamoja lakini sasa tumeimaliza miezi 6 tumeshapishana sana. Ingawa kila mtu ana mwisho na ndoto zake hivyo hakuna haja ya kushindana. Sijajua wewe upo katika kundi lipi.
1) Kuna walioanza vizuri lakini sasa wameshasahau kuwa waliweka malengo.
Hawa inawezekana waliweka malengo kwa hisia walipokuja katika uhalisia wamekata tamaa wameamua kuishi kama mwaka jana. Wamesahau kuwa walikuwa na malengo ya kutimiza ndani ya mwaka huu. Na Leo wameanza nusu nyingine. Kumbuka basi ulikotoka.
2) Kuna walioanza vibaya hawakuwa na malengo yeyote na hadi sasa hawana lengo lolote. Wanaishi jua lichwe jua lizame wao sawa. Ubaya ni kwamba muda huwa hauwasubiri watu wapange mipango ndio uanze kwenda. Kama upo katika kundi hili nakushitua tu unaweza ukapanga sasa. Hautakuwa tofauti sana na wakundi la kwanza.
3) Kuna walioanza vibaya wakashituka na sasa wako vizuri katika kutimiza ndoto na malengo yao. Wakatumia nguvu na kujituma sana maana walijiona wamechelewa. Wanapofika leo wanakuwa wameshusha pumzi kidogo.
4) Walioanza vizuri na bado wako vizuri. Hawa wako wachache sana. Ambao wamebaki wakiongozwa na malengo na mipango walioiweka mwanzoni mwa mwaka.
KUMBUKA
Kuna miezi 6 tena mbele yetu ambayo kila mtu ananafasi sawa ya kufanya vizuri.
Usikae kuangalia au kushangaa ulichokifanya miezi 6 iliyopita jipange zaidi katika 6 ijayo. Yaliyopita huwezi yarudisha umeshatafakari anza upya kwenda mbele.
Unaweza ukahonga watu lakini huwezi kuhonga muda ukusubirie. Usichelewe bado nina imani na wewe. Unaweza ukafanya makubwa katika ngwe hii ya pili.
Source: Internet
No comments:
Post a Comment