Kufuatilia matokeo fuata hii link http://41.188.155.122/csee/matokeo/csee/2014/olevel2014.htm
Matokeo hayo ni ya kwanza tangu kuanza kutumika kwa mfumo mpya wa upangaji wa Wastani kwa Kutumia Pointi (GPA) ambao unaonyesha shule zote 10 za kwanza ni za binafsi.
DISTINCTION | MERIT | CREDIT | PASS | FAIL | |
GPA | 3.6 - 5.0 | 2.6 - 3.5 | 1.6 - 2.5 | 0.3 - 1.5 | 0.0 - 0.2 |
Akitangaza matokeo hayo siku ya Jumamosi jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), Dk Charles Msonde alisema waliofaulu mtihani huo ni wanafunzi 196,805 sawa na asilimia 68.33 ya watahiniwa 288,247 waliofanya mtihani huo, ikilinganishwa na 235,227, sawa na asilimia 58.25 ya waliofaulu mwaka 2013.
Dk Msonde alisema wavulana waliofaulu ni 106,960 sawa na asilimia 69.85 na wasichana ni 89,845 sawa na asilimia 66.61.Kiwango cha ufaulu kimeongezeka kwa asilimia 10 ikilinganishwa na matokeo ya mwaka 2013.Alisema watahiniwa 297,365 waliandikishwa kufanya mtihani huo wakiwamo wasichana 139,400 sawa na asilimia 46.88 na wavulana 157965 sawa na asilimia 53.12. Watahiniwa wa shule walikuwa 244,902 ikilinganishwa na watahiniwa 367,163 walioandikishwa kufanya mtihani huo mwaka 2013.
“Idadi ya watahiniwa wa shule walioandikishwa kufanya mtihani huo ilipungua kwa asilimia 33.3 ikilinganishwa na watahiniwa walioandikishwa mwaka 2013.”
“Mwaka 2012 kati ya watahiniwa 386,355 waliofanya mtihani wa kidato cha pili, watahiniwa 136,243 walirudia kidato cha pili na watahiniwa 250,112 waliendelea na kidato cha tatu ambao ndiyo waliosajiliwa kufanya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2014,” alisema na kuongeza:
“Kati ya watahiniwa 297,365 waliosajiliwa kufanya mtihani wa kidato cha nne 2014, watahiniwa 288,247 sawa na asilimia 96.93 walifanya mtihani na watahiniwa 9,118 sawa na asilimia 3.07 hawakufanya mtihani kutokana na sababu mbalimbali.”
Alisema watahiniwa wa shule, kati ya watahiniwa 244,902 waliosajiliwa watahiniwa 244,410 sawa na asilimia 98.17 walifanya mtihani ambao wasichana walikuwa ni 110,603 sawa na asilimia 98.13 na wavulana ni 129,807 sawa na asilimia 98.19. Watahiniwa 4,492 sawa na asilimia 1.83 hawakufanya mtihani.
Akizungumzia ubora wa ufaulu, Dkt Msonde amesema kuwa jumla ya watahiniwa waliopata ufaulu mzuri wa madaraja ya Distinction, Merit na Credit ni 73,832 sawa na asilimia 30.72 wakiwemo wasichana 27,991 sawa na asilimia 25.32 na wavulana ni 45,841 sawa na asilimia 35.33.
Watahiniwa waliopata daraja la PASS 93,811 sawa na asilimia 39.04 na waliofeli kwa kupata daraja la FAIL 72,667 sawa na asilimia 30.24.
Kuhusu ufaulu wa masomo, Dkt Msonde amesema kuwa ufaulu katika masomo ya msingi umepanda kwa kati ya asilimia 1.28 na 11.22 ikilinganishwa na mwaka 2013.
Ufaulu wa juu kabisa umekuwa katika somo la Kiswahili ambapo asilimia 69.66 ya watahiniwa wote wamefaulu na ufaulu chini kabisa ni wa somo la Basic Mathematics ambapo asilimia 19.58.
Amesema Baraza limefuta matokeo ya watahiniwa 184 baada ya kubainika kufanya udanganyifu, kati yao 128 ni watahiniwa wa kujitegemea na 56 ni watahiniwa wa shule.
Shule 10 bora-Kitaifa
1.Kaizirege-Kagera
2.Mwanza Alliance-Mwanza
3.Marian Girls-Pwani
4. St.Francis-Mbeya
5.Abbey-Mtwara
6.Feza Girls - Dar
7.Canossa-Dar
8.Bethel Sabs Girls-Iringa
9. Marian Boys-Pwani
10.Feza Boys - Dar
1.Kaizirege-Kagera
2.Mwanza Alliance-Mwanza
3.Marian Girls-Pwani
4. St.Francis-Mbeya
5.Abbey-Mtwara
6.Feza Girls - Dar
7.Canossa-Dar
8.Bethel Sabs Girls-Iringa
9. Marian Boys-Pwani
10.Feza Boys - Dar
Shule 10 za Mwisho
1.Manolo-Tanga
2.Chokocho-Pemba
3.Kwaluguru-Tanga
4.Relini-Tanga
5.Mashindei-Dar es Salaam
6.Njelekela Islamic Seminary-Kigoma
7.Vudee-Kilimanjaro
8.Mnazi-Tanga
9.Ruhembe-Morogoro
10. Magoma-Tanga
1.Manolo-Tanga
2.Chokocho-Pemba
3.Kwaluguru-Tanga
4.Relini-Tanga
5.Mashindei-Dar es Salaam
6.Njelekela Islamic Seminary-Kigoma
7.Vudee-Kilimanjaro
8.Mnazi-Tanga
9.Ruhembe-Morogoro
10. Magoma-Tanga
Matokeo yanaonyesha kuwa shule za vipaji maalum za Serikali na za seminari zilizokuwa zinafanya vizuri, zimetupwa nje ya Kumi Bora
Dkt Msonde pia ametaja watahiniwa 10 waliofanya vizuri kuwa ni;
1.Nyakaho Marungu - Baobab Pwani
2.Elton Sadock Jacob - Feza Boys Dar es salaam
3.Samwel M Adam - Marian Boys Pwani
4.Fainess John Mwakisimba - St Francis Girls Mbeya
5.Mugisha Reynold Lukambuzi - Bendel Memorial Kilimanjaro
6.Paul W Jijimya - Marian Boys Pwani
7.Angel Lundgreen Mcharo - St Francis Girls Mbeya
8.Atuganile Cairo Jimmy - Canossa
9.Jenifa Lundgreen Mcharo - St Francis Girls Mbeya
10.Mahmoud Dadi Bakili - Feza Boys.
2.Elton Sadock Jacob - Feza Boys Dar es salaam
3.Samwel M Adam - Marian Boys Pwani
4.Fainess John Mwakisimba - St Francis Girls Mbeya
5.Mugisha Reynold Lukambuzi - Bendel Memorial Kilimanjaro
6.Paul W Jijimya - Marian Boys Pwani
7.Angel Lundgreen Mcharo - St Francis Girls Mbeya
8.Atuganile Cairo Jimmy - Canossa
9.Jenifa Lundgreen Mcharo - St Francis Girls Mbeya
10.Mahmoud Dadi Bakili - Feza Boys.
Source: IPP Media
0 comments:
Post a Comment