Katika hali inayotafsiriwa kuwa ni ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha za umma, Ofisi ya Waziri Mkuu, imeomba Shilingi bilioni moja kwa ajili ya kuwazika viongozi wa kitaifa watakaokufa katika mwaka wa fedha unaoanza Juni, mwaka huu.Iliwasilisha ombi hilo kwenye bajeti yake iliyosomwa bungeni Jumatano wiki hii.
Kufuatia ombi hilo, wabunge Lucy Owenya Viti maalumu (Chadema) na Kange Lugora (CCM) Mwibara, wameishambulia ofisi hiyo na kuhoji ni viongozi gani wa kitaifa watakaokufa mwaka ujao.
Owenya ndiye aliyeibua hoja hiyo wakati akichangia hotuba ya makadirio na matumizi ya ofisi hiyo iliyowasilishwa bungeni Jumatano wiki hii na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Owenya alisema inashangaza kutumia mabilioni kwa watu watakaokufa badala ya kuwekeza fedha hizo kwa maendeleo ya walio hai.
Aliitaka Ofisi ya Waziri Mkuu kupunguza fedha hizo na kujenga chumba cha upasuaji cha hospitali ya Mawenzi na kuisaidia hospitali teule ya St Joseph kununua vitanda vya wodi ya wazazi.
Lugora kwa upande wake akiponda bajeti hiyo alisema licha ya kuwa mbunge wa CCM haungi mkono bajeti ya Waziri Mkuu, akiituhumu kuomba kutengea Sh bilioni kwa ajili ya mazishi ya viongozi watakaokufa ni ubadhirifu.
“Siungi mkono hoja mpaka nione bajeti inaeleza mikakati na dhamira ya dhati ya kumaliza rushwa na dawa za kulevya nchini,” alisema.
“Mazishi gani ya viongozi bilioni moja huu ni wizi, wizi mtupu ndani ya serikali kama wasipokufa tutapata ripoti ya matumizi mengine ya fedha hizo.”
Soma zaidi habari hii http://thedonsimon.blogspot.com/2013/04/serikali-yaomba-shbilmoja-kuzika.html?spref=fb
0 comments:
Post a Comment