Social Icons

Wednesday, 16 January 2013

HOT TOPIC: WANAUME WANAOJICHUBUA......

Studies have found that men are also beginning to bleach their skin

Tumezoea kuona wakinadada na kinamama wakitumia cream siku hizi wanaita 'kutumia carolight' kujing'arisha (kujichubua) miaka nenda miaka rudi. Wengi wanateseka mno na jua kali la bongo wanakuwa wekundu na ngozi zinatisha na kuweka mabaka mabaka

Ila sasa na wanaume nao wanajichubua, tena idadi yao inaongezeka siku hadi siku. Zamani ilikuwa ni kawaida kwa wanamuziki au wasanii kujichubua siku hizi hadi wafanyakazi wa serikalini na sekta binafsi wanajichubua. Unamkuta mtu uso mweupe na mng'avu mwangalie mikono yake sasa myeusi na ni mwanaume.

 
 

Kuna waliojibadilisha kabisa na kuwa na fair skin complexion kama Michael Jackson na wengine wengi hata Tanzania kwenye entertainment industry ni wengi mno.

Swali la leo: Kwanini wanaume wanajichubua? Upande wa wanawake najua inajulikana kwanini wengi wanafanya hivyo. Ila sijapata jibu bado kwanini mwanaume atumie carolight ili awe mweupe (mara nyingi usoni tu). Hebu tujuzane wajameni.....


Nimependezwa na hii Speech ya Malcom X - May 5, 1962, Los Angeles....I am not trying to judge yoyote kwa maamuzi yake ila napenda kujua chanzo na sababu kwa nini imekuwa trend ya wanaume nao kujichubua hasa siku za karibuni.



“Who taught you to hate the texture of your hair?
Who taught you to hate the color of your skin, to such extent that you bleach to get like the white man?
Who taught you to hate the shape of your nose, and the shape of your lips?
Who taught you to hate yourself, from the top of your head to the soles of your feet?”



0 comments:

Post a Comment