Social Icons

Monday 3 December 2012

R.I.P SHARO MILIONEA.....


 
 
Marehemu Hussein Ramadhani Mkieti a.k.a. Sharo Milionea enzi za uhai wake
 
 
 
Binafsi nilivutiwa sana na sanaa yake na vimbwanga vyake vya kisharobaro. Alileta mapinduzi ya sanaa ya maigizo kwa kuonyesha kuwa si lazima uwe mchafu mchafu ili uweze kuchekesha watu kama ilivyozoeleka.
 
 
Kifo chake kimetokea mapema mno, wakati nyota yake ikianza kung'ara na kukubalika hapa Tanzania.
 
R.I.P Sharo Milionea.....Mungu akupumzishe kwa amani safari yetu wote ni hiyo hiyo.
 
 
 
Hivi ndivyo Baadhi ya Vitu vilivyoibiwa baada ya Sharo milionea kupata Ajali na Kupoteza Maisha , Jitahada za Police ndio imefanya vitu hivi kupatikana.....
 
Pichani ni baadhi ya vitu vilivyoporwa eneo la tukio la ajali ya marehemu sharo milionea ambavyo vimepatikana kwa msaada wa jeshi la polisi.
 
Hii ni aibu kubwa ubinadamu wetu uko wapi jamani mpaka kumvua nguo mtu na kuondoka nazo. Ikitokea ajali watu wa maeneo jirani wanajihusisha na uporaji mpaka kwa maiti na majeruhi ......Mungu tusamehe ni aibu kubwa mnoooo.......

0 comments:

Post a Comment