Mtoto Aneth akiwa amelazwa katika hospitali ya Rufaa ya Mbeya baada ya kukatwa mkono wake wa kushoto jana
Mtoto mdogo kama huyu wa miaka 4 anakuwa amekosa nini kikubwa jamani mpaka achomwe moto na inasemekana kulazimishwa kula kinyesi cha mtu mzima ambaye anashikiliwa na polisi kwa kumsababishia mtoto maumivu makali namna hii. Hivi ubinadamu umeenda wapi mbona ukatili huu unazidi kuchipua kila kona kila siku.......nini tatizo, nini chanzo jamani....
HALI ya Mtoto Aneth Johanes (4) aliyelazwa katika Hospitali ya
Rufaa ya Mbeya kufuatia kuchomwa moto mkono wake wa kushoto na anayedaiwa kuwa
ni Shangazi yake inaendelea vizuri licha ya kufanyiwa upasuaji uliolazimu
kukatwa kwa mkono huo.
Kwa mujibu wa mama mdogo wa mgonjwa anayemhudumia hospitalini
hapo Silvia Salvatory alithibitisha kuendelea vizuri kwa mtoto huyo ambapo
alisema ilimlazimu kufanyiwa upasuaji kutokana na mkono huo kukosa mawasiliano
na kuonekana kuvunjika.
Alisema taarifa za awali zinaonesha shangazi yake huyo Bahati
Rukangara alianza kumtesa mtoto huyo muda mrefu mara baada ya kumchukua kutoka
kwa wazazi wake wanaoishi Bukoba Mkoani Kagera.
Aliongeza kuwa tangu amchukue kwa wazazi wake Februari Mwaka
huu amewahi kumjeruhi mkono wake wa Kulia hadi kuuvunja ambapo hadi sasa mtoto
huyo alikuwa akitegemea mkono wa kulia ambao nao umekatwa.
Tukio hilo la kisikitisha lilitokea juzi majira ya saa nne
asubuhi baada ya majirani kusikia yowe la mtoto huyo akiomba msaada kutokana na
mateso na maumivu makali aliyokuwa akiyapata kutokana na adhabu hiyo kutoka kwa
Shangazi yake
Muuguzi mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya Thomas Isidori
alisema hali iliyopelekea kukatwa kwa mkono wa mtoto huyo ni siri kati yake na
daktari aliyemhudumia na kwamba sheria ya uuguzi inakataza kutoa taarifa
ambazo ni siri.
Isidori alipoulizwa sababu za mgonjwa huyo kufanyiwa upasuaji
mapema mno hadi kusababisha ulemavu alisema ni suala la kitaalamu ambalo hata
yeye hawezi kulijibu na ni sheria ambayo inawataka madaktari kutunza siri za
wagonjwa.
Baadhi ya wananchi waliofika Hospitalini hapo kumjulia hali
mtoto Aneth aliyelazwa Wodi namba Nane ambao hawakutaka kutaja majina yao
walilaani kitendo cha madaktari kukimbilia kukata mkono mgonjwa badala ya
kujaribu njia zingine za kunusuru hali hiyo.
Habari kwa hisani ya blog ya Mbeya yetu soma zaidi hapa:
Makovu kwa hawa watoto yatapona ila ya kwenye mioyo yao hayaitaisha kamwe....KWANINI JAMANI.....
0 comments:
Post a Comment