Social Icons

Sunday, 13 May 2012

Happy Mother's Day.......


Najua unanitizama kutoka angani, natumai malaika watakufikishia ujumbe wangu kuwa nakukumbuka na nakukosa mno maishani mwangu, Yasinta William Mwakabaga, labda ungekuwepo ningekununulia utakacho hasa pochi, nguo na viatu kama yalivyokuwa mapendeleo yako, ningekupeleka utakako ili kukufanya ujisikie una mtoto anayekujali, LAKINI wapi ni pazuri zaidi ya MBINGUNI ulipo? Ukaona haitoshi kukaa peke yako hadi umwite na mumeo mpenzi William Mwakabaga muwe wote pamoja mkiangalia watoto wenu tokea mliko.

Mama nakupenda, nakukosa, nakumiss na nakuhitaji mno maishani mwangu. Hasa katika siku hii ya leo inaposherehekewa siku ya mama duniani najua haupo na mimi kimwili ila kiroho uko pamoja nami.

Mwambie baba, nitadumisha yale yote mliyonifundisha huku nikiepuka mliyoniasa niyaache na nitafuata nyayo zenu kufikia malengo yangu duniani.

Tunawakumbuka wote na wanao wapendwa wanakukumbuka ila tunapata faraja kujua kuwa uko mahali pema na umezungukwa na wanaokupenda. Siku moja tutaonana tena.

Happy Mother's Day mum........and all mothers out there....

2 comments:

  1. am reading your post with tears my Dear Bupe very sorry, but bible says we have to thank for everything that happen hata kama yatakuwa yakuumiza coz everything happen with reason. Pole sana na Mungu hatawaacha peke yenu kwani yeye ndio baba na mama yetu hata milele na milele.

    ReplyDelete
  2. this is really touching

    ReplyDelete