Kuvaa viatu virefu kunakufanya unasimama wima, miguu yako inanyooka zaidi, tumbo linaonekana flat, na muondoko wako unakuwa wa madaha zaidi ili uweze kubalance hatua zako kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Kutembea na viatu virefu si kitu ambacho kila mtu anaweza ila ukifanya mazoezi na practise zaidi inawezekana kujifunza.
Hatua/Steps za kufuata:
- Anza na viatu virefu kiasi inchi 2 - 3 na ukiweza kuvimudu unaenda ukiongeza urefu wake, usijaribu kutoka kutokuwahi kuvaa viatu virefu na kuanza na vile virefu labda vya inchi nne na zaidi ni hatari na hutaweza kumudu. Hii itasaidia kuizoesha miguu yako kupata nguvu ya kutembelea viatu virefu.
- Ukiweza kumudu mfano wa viatu hapo juu anza na vile vyenye urefu kiasi / kitten heels ili uweze kuizoeza miguu yako kuwa na balance ya kutosha
- Jaribu kuvaa viatu vyenye wedge/ wedge heel hivi viatu kisigino chake kimeunganishwa madhubuti na soli yake ili kukupa balance na comfort unapovaa huku kikikupa uzoefu wa kuvaa viatu vyenye kisigino kirefu
Miondoko ya viatu virefu:
- Tembea kwa hatua ndogo, taratibu huku ukihakikisha haukunji magoti yako na unatembea ukiwa straight yaani uti wako wa mgongo uko straight. Mara nyingi viatu virefu vinakufanya utembee hatua fupi fupi na pole pole kiasi ili upate balance, ni jambo la kawaida usishtuke!
- Jaribu kutembea huku miguu yako ikiwa karibu karibu hii ni ili balance yako ya mwili isiwe matatani na hatimaye kuanguka catwalk models wanatembea huku wakipishanisha miguu yao kufanya umbo la X inahitaji mazoezi zaidi lakini ukipenda kuongeza ujuzi wako wa kutembea katika heels.
- Fanya mazoezi ya kutembea na viatu vyako ndani kabla ya kutoka nje ukitaka uzoee kirahisi zaidi. Waweza kuvaa ukiwa unapika, unanyoosha na ukiwa unafanya shughuli mbalimbali ili kujifunza kuhusu kubalance mwili wako na kuwa comfortable. Jitahidi kufanya yafuatayo kama kugeuka, kusimama, kupiga hatua ili kuzoesha miguu yako na mwili wako. Pia jitahidi kutembea katika sakafu tofauti ile ya mbao, yenye tiles au yenye kapeti ili kujifunza zaidi mbinu za kuweza kuubalance mwili na miguu yako.
- Jaribu kucheza/dance ukiwa umevaa viatu vyako hii ni kama zoezi pale utakapovaa viatu virefu na ukaenda sehemu ya muziki!
- Muhimu....Kwenye ngazi,weka mguu wako mzima kwenye step za ngazi ukiwa unashuka chini ila inua kisigino chako na kanyagia sehemu ya mbele ya kiatu chako ukiwa unapanda ngazi na shikilia rails za ngazi ili kujipa support na kuzuia kuanguka
- Weka cushion/viongezeo vinavyowekwa kwenye kiatu ili kukupa urahisi wa kutembelea viatu vyako vinakuja katika shape mbalimbali na size kukidhi mahitaji yako
- Ipe miguu yako mapumziko kwa kubadili urefu wa viatu vyako na aina yake sio kila siku aina moja na urefu mmoja
Angalizo ukivaa viatu virefu:
- Kuendesha gari na viatu virefu ni hatari kwa usalama wako jitahidi uwe na sandals au viatu vya kawaida ambavyo si rahisi kuteleza na ukaishia kupata madhara barabarani.
- Tembea kwa uangalifu hasa sehemu zenye majani, mawe, matofali au mifereji angalia unapokanyaga na uwe mwangalifu sababu madhara ya kuumia vibaya ukiwa na viatu virefu ni makubwa zaidi kuliko ukiwa na viatu vifupi.
- Hata kama viatu vyako ni vizuri kiasi gani usivae sana viatu virefu vya aina moja muda wote 24/7/365 ni hatari kwa mwili wako na umbo lako sababu utapata maumivu ya mgongo na ya miguu.
- Heels over 5 inches tall aren't really meant for daily walking......but special wearing! Be wise and dont try to juggle the unseen by the way you walk......
0 comments:
Post a Comment