Social Icons

Wednesday, 11 January 2012

Urembo wa Nyusi/ Shaping Your Eyebrows

eyebrow design, tips for designing brows, eyebrow shaping

Nyusi ulizonazo kabla ya kutumia wanja zitatengeneza base ya kushape na kudefine.
Mfano nyusi hizo kwenye picha mwishoni ni nyembamba zinahitaji kupunguzwa kidogo na kuzipa mkunjo kidogo.

Nyusi zianzie wapi?

eyebrow design, tips for designing brows, eyebrow shaping

Zisianze mbali na macho yako yanapoanzia, unapozipunguza uwe makini na hili.

Mkunjo/Arch ya nyusi ianzie wapi?

eyebrow design, tips for designing brows, eyebrow shaping

Mkunjo wa nyusi zako uanzie karibu na nusu ya nyusi zako kama nyuzi 90 (90 degrees) kutoka kwenye pua .Usipandishe mkunjo wa nyusi sana, haitapendeza na nyusi zitakupa muonekano tofauti kidogo.

Nyusi iishie wapi?

eyebrow design, tips for designing brows, eyebrow shaping
Nyusi isipitilize sana mwisho wa macho yako kwa mtazamo wa uhalisia zaidi (natural look).
Kunyoa nyusi mno mara nyingi inasababisha zipoteze kujaa kwake na kupungua ujazo.
Jazia sehemu ambazo hazina nyusi kwa kutumia wanja unaoendana na rangi ya nyusi zako, make-up ni kwa ajili ya kuongezea uzuri wako wa asili na si kubadilisha mwonekano wako wa uhalisi. Hakuna mwenye nyusi nyekundu, kijani au bluu jitahidi utumie wanja wa brown au mweusi unaoendana na rangi ya nyusi zako kwa kuchora kwa mbali kiasi na si kwa mgandamizo ili uvutie zaidi.

eyebrow design, eyebrow shaping tips

Nyusi zikitengenezwa vizuri uzuri wa macho na shape ya macho inaonekana sawia kama picha hapo juu.
Ikiwa unakutana na mtu na kitu cha kwanza unachokiona kwake ni nyusi zake, hakika zitakuwa hazipo katika shape inayotakiwa au ametumia wanja wa kupitiliza.

Till next time......

2 comments:

  1. nice post...keep it up

    i appreciate the info and the fact that u seem to know what you are talking about, coz i know you i can witness that u know what ur talking about girl

    Much love

    SecretAdmirer

    ReplyDelete
  2. Think I need a private class on this lol...

    ReplyDelete